Kitwa-Mulomoni
JF-Expert Member
- Oct 25, 2016
- 1,779
- 1,119
Beberu Marekani Ametoa Msaada wa Shilingi Tilioni 15 Nchini Tanzania Kwa miaka 20 iliyopita katika Mpango Mmoja tuu wa.kupambana na Magonjwa hasa Ukimwi na Kifua Kikuu na kuokoa maelfu ya maisha ya Watanzania kwenye sekta ya Afya.
Hapo sijagusia MCCL,USAid Wala Wakfu wa Bill & Melinda Gates Foundation kwenye Kifua Kikuu,Malaria nk.
My Take; Sielewi Mnaoshobokea Russia Huwa mnafanya hivyo Kwa Maslahi yapi hasa?
Anaejua kiasi ambacho Russia amewahi toa Kwa Tanzania of any kind anijuze.
Nawashukuru sana beberu USA na nitasimama na Marekani mda wote na wakati wote.
Mungu ibariki Tanzania na Wabariki Mabeberu America.
Enzi za utumwa, mtumwa asiye na akili za kumtosha, alikuwa na mawazo kwamba aliyemnunua ana haki naye! Na alikuwa anaeleza kuwa bwana wake katumia hela nyingi kumnunua! Hata alipo kuwa akiadhibiwa, alikuwa anafurahia adhabu, Kwa sababu anazihurumia zile gharama boss wake alizotumia kumpata! Wewe ni yule mtumwa unayeishi Leo, ambaye hajakombolewa. Na fikra zako hizo utazitetea mpaka unakufa! Eti Bill Gate na mkewe - Fanya utafiti ujue nia ya hao maboss wako Kwa waafrika.