mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,897
- 18,477
Marekani imesusia mafuta ya urusi bado urusi inapeta! Nchi za magharibi zimeiwekea urusi vikwazo vya kiuchumi zaidi ya 6,000 lakini ndo sasa inapata pesa zaidi! Marekani inaumiza kichwa kuwaza waifanyieje Urusi ili kuikomoa kiuchumi?
Marekani imekuja na wazo lisilotekelezeka!! Inasema itaweka ukomo wa bei ya mafuta ya urusi!! Yaani mafuta ni ya Urusi, lakini bei kiduchu apange Marekani!!
Ingewezekana labda bkama marekani ingekuwa mnunuzi pekee wa mafuta hayo!! Watu husema "ukisusa sie twala". Nchi za magharibi zimesusia lakini India na China zimeyachangamkia!! Sasa bila aibu marekani inasema itazishawishi China na India zikubali!! Hicho kitu hakiwezekani.
China na India wanajua kuwa Marekani si rafiki wa kweli, hawawezi kuiunga mkono kudhulumu mchana kweupe!! Zinajua pia leo mlengwa ni Urusi, lakini kesho mlengwa anaweza kuwa China hasa kutokana na mgogoro wa Taiwan na China ambapo Marekani inataka kuitumia Taiwan kuidhoofisha China kama ambavyo inaitumia ukraine kutaka kuidhoofisha Urusi.
India pia sera yao ni ya kukataa kuchaguliwa marafiki na maadui na nchi za nje! Haiiamini marekani hata kidogo. Kwa mfano Marekani ilikuwa inaizuia India isinunue makombora ya ulinzi wa anga ya S400 toka Urusi. Lakini India ikaigomea!!
Marekani italazimika kuiona Urusi inapeta kiuchumi!! Vikwazo walivyoweka vimewaumiza wao zaidi na kuifanya pesa ya Urusi ruble iwe na nguvu zaidi kuliko kabla ya vikwazo!