Hivi karibuni makundi ya Fatah na Hamas ya Palestina yalifanya mazungumzo ya mardhiano mjini Beijing, mazungumzo ambayo yaliitwa na chombo cha habari cha Marekani, Associated Press, kuwa juhudi za karibuni za China kujiweka katika nafasi ya upatanishi katika Mashariki ya Kati kama mbadala wa Marekani na wenza wake wa Magharibi, na kupuuza juhudi za amani za China kwa nadharia ya ‘zabibu chungu’ na kujikita zaidi katika ushindani wa siasa za kijiografia.
Tangu kuanza kwa mapigano mapya kama sehemu ya mgogoro unaoendelea kati ya Israel na Palestina, mara nyingi maofisa wa Marekani wameitaka China kutumia ushawishi wake katika Mashariki ya Kati ili kupunguza mvutano katika kanda hiyo. Lakini mara wajumbe wa makundi ya Hamas na Fatah wanapoonesha utayari wa kisiasa wa kufikia makubaliano, ni Marekani ambayo haifurahishwi kuona China inapiga hatua chanya katika kuboresha amani na umoja. Ni wazi kwamba hatua hii ya ‘kuuma nma kupuliza’ ni mfano wa karibuni zaidi wa ubinafsi wa Marekani na vigezo viwili katika uwanja wa kimataifa.
Ukweli ni kwamba, sio bahati mbaya kuwa China imeweza kuwezesha mazungumzo kati ya makundi ya Fatah na Hamas. China daima imekuwa kwenye upande wa usawa na haki katika suala la Mashariki ya Kati, na hivyo kutambuliwa na pande nyingi katika kanda hiyo. Kwa makundi ya Fatah na Hamas kutafuta mazungumzo yanayoratibiwa na China, hili limewezekana kutokana na imani yao kwa China.
Wakati huohuo, Marekani inajaribu kufikia makubaliano ya kusimamisha vitahivi karibuni kwa kulitaka kundi la Hamas kukubali pendekezo bora la Israel la kumaliza vita katika Ukanda wa Gaza, ambalo limekataliwa na maofisa wa ngazi ya juu wa Hamas ambao wamesema ‘shambulio lenyewe ni uhalifu’ na ‘kusimamisha mashambulio dhidi ya Wapalestina sio ukarimu.’ Ni wazi kwamba hatua ya Marekani inachochea zaidi mvutano badala ya kupooza hali katika eneo hilo.
Marekani, chini ya kivuli cha ‘kutafuta amani,’ imezoa kushughulika na masuala magumu ya kimataifa kwa namna ya upendeleo na mara nyingine kwa kutumia mabavu. Hata hivyo, hatua ya China ya kuboresha amani na maridhiano inakinzana vikali na mkakati wa Marekani katika suala la Mashariki ya Kati. Ikulu ya Marekani, yenye matamanio makubwa lakini kiasi kidogo cha uwajibikaji, haijafanya juhudi zozote za kuleta amani, lakini imeongeza zaidi vurugu katika kanda hiyo.
Tunaweza kusema kuwa, mpango wa Marekani hauwezi kufanya kazi, na si ajabu kwamba nchi hiyo imejikuta katika hali yah ii ya kufedhehesha. Sera ya Marekani kuhusu Mashariki ya Kati imeendelea kuwa ya kujinufaisha yenyewe, na kimsingi inatimiza mkakati wake wa ushindani wa nguvu kubwa, kiasi kwamba hatua zake zinaleta maendeleo kidogo, lakini inasababisha hali katika eneo hilo kukosa ufumbuzi. Matokeo yake, inakuwa vigumu kwa Marekani kudumisha mamlaka yake katika masuala ya Mashariki ya Kati, na inajikuta katika wakati mgumu ikipata matokeo duni na kushuka kwa ushawishi wake.
Ufunguo wa amani katika Mashariki ya Kati ni kufuata njia sahihi, na sio kwenda mrama ama hata kurudi nyuma. Mwezi Machi mwaka jana, Iran na Saudi Arabia zilirejesha uhusiano wa kidiplomasia, hatua iliyowezekana kutokana na upatanishi ulitimizwa na China.
Marekani imekuwa na wasiwasi wa China kuziba ufa ambao nchi hiyo imeuacha katika Mashariki ya Kati, na hivyo imeendelea kutia doa hatua za China kuhusu masuala ya Mashariki ya Kati, na kujaribu kushusha ushawishi wa China katika kanda hiyo kwa kutumia njia mbalimbali. Sasa, ukweli umedhihirisha zaidi kitendo cha China cha kuunga mkono kithabiti na kiufanisi juhudi za nchi za kanda hiyo kutatua masuala tete kupitia njia za kisiasa.
Zaidi, China haitajihusisha na siasa za kijiografia katika Mashariki ya Kati, bali ushawishi unaoongezeka wa China unatokana na nia nzuri na ushirikiano, bila ya hila yoyote. Uhusiano kama huu ni nadra na wa kudumu, na bila shaka utakuwa maarufu zaidi na zaidi katika Mashariki ya Kati. Huu pia ni wakati kwa Marekani kujifanyia tathmini na kujaribu kujizuia, na kuacha sera zake kali katika kanda ya Mashariki ya Kati.