Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Siku za karibuni Marekani imejifanya ina huruma na wapalestina na huku anapeleka silaha na anahimiza Israel iendeleze kazi yake.
Kuanzia raisi Biden ,Blinke mpaka wairi wa ulinzi Lord Austin wote wmejifanya wana huruma na kurudia ziara za mazungumzo ya siri na Israel.Wakiibuka hadharani wanasema Israel ina haki ya kuendelea kupigana kwa nguvu ili kuwamaliza wapiganaji wa Hamas.Muhimu ni kuchukua tahadhari ili wasiendelee kuua watu kwa wingi kama vile.
Hiyo si huruma bali ni ujanja wa kutaka kuzuia hasira za waislamu na waarabu wanaoizunguka Israel.Na upande mwengine ni kama kuhofia kumuua mtu kwa bunduki na badala yake ukamuwekea sumu itakayomuua mwaka ujao.
Kwa vile Hamas hawajulikani walipo kwa uhakika Gaza yote,kuiambia Israel iendelee kuua Hamas ni kuipa kibali ifanye mauwaji kwa kiwango chochote na mwishowe itasema ilikuwa inapiga Hamas japo watakaoonekana kufa wengi ni watoto na akinamama.Kwa maana hiyo Marekani haitakuwa na kusema Israel itakavyosema hivyo na yeye atakuwe amejiwekea kinga kwa waislamu na waarabu
Kwa upande mwengine hata kama Hamas itatajwa wamemalizwa wote,jee wapalestina watakaobaki hai watakuwa wamepata nini na jee watabaki salama.Hapana.
Kitakachotokea ni kuwa atakayesema ameua Hamas ataendelea kuua waliobaki kwa visingizio hivyo hivyo mpaka neno taifa la Palestina na masjid Aqsa iwe si vitu vya kuzungumzwa tena.
Hiyo ina maana huruma za Marekani za sasa ni kama kuua kwa kutumia sumu.Kama wana huruma kweli basi wangeacha kuisaidia Israel na ikaunga maazimio ya UN ya kusitisha vita moja kwa moja.
Kama waislamu na waarabu wangezinduka na kuwa na la kufanya basi ilikuwa ni kufanya sasa kuokoa wapalestina.Na kwa upande wa Hamas kwa nguvu yoyote waliyonayo wana sababu ya kutumia nyenzo zao hizo kupigana mpaka tone la mwishjo na Mwenyezi Mungu atawapa ushindi kuliko kubweteka na kufikiria huruma za Marekani kwa watu wao.