Kuna njia nyingi na tofauti tofauti sana Marekani inanufaika na misaada inayotoa.
Mfano misaada mbalimbali inayotoa kwa nchi jirani yake kama Mexico, Colombia na nyingine za America Kusini ni ili kupunguza mazingira hasi katika hizo nchi yanayochochea raia wengi masikini wa hizo nchi kukimbilia na kuzamia Marekani kama wahamiaji haramu. Pia ni kuchochea uchumi wa hizo nchi kukua na kuwa stable ili wazalishe malighafi na bidhaa kama Kahawa, sukari,ndizi, parachichi, mbao n.k zinazohitajika Marekani kwa wingi na pia wawe na pesa wanunue bidhaa za viwandani za Marekani. Wayape makampuni ya Marekani tenda mbalimbali, Wasiwakaribishe maadui wa US kama Urusi na China.
Ukija kwa nchi kama Misri, Jordan na Lebanon misaada wanayoipata kutoka Marekani ndio inawalainisha wasiibughudhi au kuisumbua Israel ambaye ni mshirika namba moja na wa kuaminiwa wa muda wote wa Marekani hapo Mashariki ya kati. Hiyo misaada ndio inawafanya waipe taarifa za intelejensia za makundi ya Kiarabu yanayotoka kudhuru raia wa Western.
Misaada kwa nchi kama Tanzania, Uganda na Kenya ni ku check na kufanya counter kwa ushawishi wa mataifa kama China na Urusi ni kuwezeshwa kuwa soko zuri la bidhaa, ni kuwekwa akiba kutumiza maslahi yake pale inapohitajika(Marekani leo ikitaka kupigana na taifa la Kiarabu anawapigia simu to Djibouti wawe tayari kupokea manowari zaidi za jeshi lake).
Marekani ana vituo vya kijeshi zaidi ya 700 vilivyotapakaa duniani kote, inahitaji washirika wengi sana kumudu kusimamia mtandao wote huu na njia mojawapo ya kupata huo ushirika ni kutoa misaada.
Pia tofauti na China, makampuni mengi ya Marekani na West kwa ujumla ni nadra sana kutoa 10% direct kwa watawala kupata tenda mbalimbali au fursa za uwekezaji kwenye nchi zenye mazingira ya rushwa, hiyo misaada ndio inayotumiwa na serikali zao kama mbadala kuhakikisha wanapewa kipaumbele na wanapata hizo fursa.
Msemo wa Kiswahili wa mikono mitupwi hailambwi ni sahihi kabisa.