Marekani inazuia wenye VIZA kutoka Tanzania kuingia

Marekani inazuia wenye VIZA kutoka Tanzania kuingia

Mwingereza

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2014
Posts
1,115
Reaction score
2,771
Wanabodi,

Nina Ndugu ambaye yuko serikalini (Paspoti ya Utumishi) na alikuwa na VISA ya miaka 5 ya kuingia Marekani. Wiki iliyopita pamoja na Mkewe waliondoka kwenda Marekani kuwaona watoto wao wanaosoma kule, lakini bahati mbaya pamoja na watanzania wengine wawili, wakiwa uwanja wa Chicago, walizuiliwa kuingia nchini humo kutokana na matatizo ya COVID-19.

Na hata walipofika Holland, walilazimika kupimwa kabla ya kupanda ndege ya kwenda Marekani wakidai Tanzania haishirikiani na WHO.

Aliloambiwa ni kwamba wanaoruhusiwa kuingia ni Diplomats tu na pia kwa masharti. Hawaruhusu wenye VISA za kawaida kutoka Tanzania kuingia. Sina hakika ni kwa watanzania tu au pia mataifa mengine nao wanaathirika na hili janga?

Nadhani kwetu raia wa kawaida wenye VISA, tusipoteze hela zebu kwa kujaribisha. Tusubirie hadi hali ile sawa maana gharama kwenda Marekani siyo kidogo matokeo yake turudishwe Eapoti !
 
Ngoja wawazuie tu. Hakuna namna. Lissu akipeleka watoto wake mnalalamika eti ana watoto kwa mabeberu! Wawazuie si tu kwa covid-19, bali kuzima demokrasia na kushindwa kuandamana baada ya CCM kuiba uchaguzi kupitia kura za kwenye mabegi.
Wiki iliyopita pamoja na Mkewe waliondoka kwenda Marekani kuwaona watoto wao wanaosoma kule, lakini bahati mbaya pamoja na watanzania wengine wawili , wakiwa uwanja wa Chicago, walizuiliwa kuingia nchini humo kutokana na matatizo ya COVID-19.
 
Back
Top Bottom