Marekani inazuia wenye VIZA kutoka Tanzania kuingia

Marekani inazuia wenye VIZA kutoka Tanzania kuingia

Kati ya Marekani na Tanzania ni wapi palipoathirika zaidi na korona, kuna jambo linatafutwa hapa....kuna shirika moja la ndege limeshatoa sharti la kuchanjwa covid-19 ndo uweze kupanda ndege zao, ngoja tuone....
 
Marekani ilifunga mipaka yake kwa nchi karibia zote Ulimwenguni na sio Tanzania tuu, wanaruhusu Raia wao tuu kuingia na kutoka
 
Mimi nashindwa kuelewa. Inaingiaje akilini kwamba corona imetokomea kwa maombi lakini kansa, kisukari, ukimwi na magonjwa mengi hatari bado yapo. Kwa nini maombi yasiwe extended kutokomeza magonjwa yote na ifike wakati bajeti ya afya isiwepo na hata hospitali zisiendelee kujengwa.
Ina Mungu kaona tu korona ndiyo hatari na magonjwa mengine yaendelee?
Halafu kama corona haipo tunaogopa nini kupima ili kuuthibitishia ulimwengu jambo hili?
Naona hapa ni akili za kuambiwa... Kama si ujinga
Hakuna maombi yaliyoondoa corona.
Corona ipo kwenye kupima.
Usipopima huoni corona.
 
Nadhani kwetu raia wa kawaida wenye VISA, tusipoteze hela zebu kwa kujaribisha. Tusubirie hadi hali ile sawa maana gharama kwenda Marekani siyo kidogo matokeo yake turudishwe Eapoti
Unachotakiwa kufanya ni kuwa na health certificate inayoonesha kuwa huna covid. Mbona wamarekani wenyewe kibongobongo hata mask hawavai!
 
Wanabodi,

Nina Ndugu ambaye yuko serikalini (Paspoti ya Utumishi) na alikuwa na VISA ya miaka 5 ya kuingia Marekani. Wiki iliyopita pamoja na Mkewe waliondoka kwenda Marekani kuwaona watoto wao wanaosoma kule, lakini bahati mbaya pamoja na watanzania wengine wawili, wakiwa uwanja wa Chicago, walizuiliwa kuingia nchini humo kutokana na matatizo ya COVID-19.

Na hata walipofika Holland, walilazimika kupimwa kabla ya kupanda ndege ya kwenda Marekani wakidai Tanzania haishirikiani na WHO.

Aliloambiwa ni kwamba wanaoruhusiwa kuingia ni Diplomats tu na pia kwa masharti. Hawaruhusu wenye VISA za kawaida kutoka Tanzania kuingia. Sina hakika ni kwa watanzania tu au pia mataifa mengine nao wanaathirika na hili janga?

Nadhani kwetu raia wa kawaida wenye VISA, tusipoteze hela zebu kwa kujaribisha. Tusubirie hadi hali ile sawa maana gharama kwenda Marekani siyo kidogo matokeo yake turudishwe Eapoti !
Tulieni kwenu,mnafuata nini huko?
 
Wasitutishe hao mabeberu, sisi tutakuwa donor country siku zijazo.
Kwa pesa ipi? Wakati pesa zote za walipa kodi inatumika kuidhoofisha chadema kuua upinzani kudidimiza demokrasia badala ya maendeleo
 
Back
Top Bottom