Uchaguzi 2020 Marekani: Kuanzia leo, tunaweka vizuizi kwa waliohusika na kuvuruga Uchaguzi nchini Tanzania

Uchaguzi 2020 Marekani: Kuanzia leo, tunaweka vizuizi kwa waliohusika na kuvuruga Uchaguzi nchini Tanzania

..hilo sina uhakika nalo kwasababu mikutano ya WB na IMF huwa haiko public kama ya UN.

..hatua zilizochukuliwa naamini zimetokana na mapendekezo ya balozi wa US aliyeko hapa Tz.

..serikali inapaswa kurekebisha hali hii isifikie kiwango cha nchi kuwekewa vikwazo vikali zaidi.

Hapo inatakiwa diplomacy ya hali ya juu sana hasa kwa serikali ya Biden!!! Kabudi hana diplomacy ni mtu wa maguv na hapo ndio tunawakumbuka watu kama marehemu Mahiga na uzoefu wao!!
 
Tatizo la hawa wakubwa sio wao , watakaoumia ni WATOTO wao ....wengi wana watoto na ndugu wanaoishi ..huko , na marekani hapao ndio huwa wankomoa , washirika wao wa kibishara etc
Watoto wao,wake zao,jamaa zao ni sehemu ya wanufaika wa dhuluma hivyo ni sahihi kukinywea kikombe.
 
Nikiziangalia sura zilizojazana NEC na kwa msajili wa Vyama vya Siasa kwa hakika wamejaa wazalendo watupu na wengi wao hata huko Marekani hawakujui.

Ningepata mashaka kama viongozi wa Chadema au CCM ndio wangezuiliwa kwenda Marekani kwa sababu kwenye vyama vya siasa ndio kumejaa wazururaji.

Au kwa mfano wangezuiliwa wabunge wa bunge letu la JMT akina mheshimiwa Makamba Jr, hapo ingekuwa tatizo.

Maendeleo hayana vyama!
 
Kama kuna massive voter suppression waliwezaje kuchagua wewe kiazi mbatata.
Maandiko hayo yanaeleza kuwa Ingawa kuna massive voter suppression wamarekani weusi /latino waliweza kuchagua wawakilishi wao!!! Is that a contradiction you empty skull!!
 
Nimependa agizo hilo kwamba WACHUKULIWE HATUA vinginevyo Marekani haitasita kuchukua hatua zaidi
 
Hii kauli ni ukiwa verified ile ID yako nyingine nimeisoma umemponda Sana guma nijo
Na sisi sijui tuwawekee vikwazo walomuibia kura Trump,ila tuache tu maana nyani haoni kundule kwa sababu kundule lipo upande ambao kisogo kipo.
Huyu jamaa kama kuna kitu alivutishwa akiwa mtoto,kha,
 
Kupitia akaunti yake ya Twitter, Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje, Mike Pompeo ameandika "Kuna matokeo ya kuingilia mchakato wa kidemokrasia. Kuanzia leo, tunaweka vizuizi vya visa kwa wale wanaohusika na uvurugaji wa uchaguzi nchini Tanzania. Tunabaki kujitolea kufanya kazi pamoja kuendeleza demokrasia na ustawi wa pande zote kwa nchi zetu zote mbili."

View attachment 1681412

Soma pia: Visa Restrictions on Tanzanians for Undermining the Democratic Process and Human Rights - United States Department of State
___________________________________________________

Marekani imetangaza kuwawekea vikwazo vya vya kuingia nchini humo maafisa wa Tanzania ambao nchi hiyo inawatuhumu kwa kile wanachokitaja kuwa kuharibu uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, mwaka 2020.

Maofisa hao wanatajwa kuhusika kuingilia mchakato wa uchaguzi na kuminya utekelezaji wa demokrasia.

Hata hivyo taarifa hiyo ya wizara ya mambo ya nje ya Marekani haijabainisha ni viongozi gani hasa kutoka Tanzania waliowekewa vikwazo vya kuingia Marekani.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na waziri wa mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo, Waangalizi wa uchaguzi na mashirika ya kiraia wanadai kuwepo kwa udanganyifu katika uchaguzi huo pamoja na uvunjifu wa haki za binadamu wakati na baada ya uchaguzi.

Marekani inasema kuzimwa ama kuzimika kwa mitandao, kuminywa kwa waandishi wa habari na nguvu kubwa iliyotumiwa na jeshi la Polisi kunafanya uchaguzi huo kutokua huru na wa haki.

Katika uchaguzi huo, baadhi ya wagombea kutoka vyama vya upinzani walienguliwa kwa sababu mbalimbali na wengine kukamatwa.

Tume ya uchaguzi nchini humo na hata Serikali kupitia waziri wake wa mambo ya nje, Palamagamba Kabudi ilieleza kwamba uchaguzi ulikua huru na wa haki.

Marekani inasema pamoja na hatua hii iliyochukua dhidi ya maafisa wa Tanzania, inaendelea kufuatilia kwa karibu maendeleo ya hoja hiyo, huku ikisema haitasita kuchukua hatua zaidi dhidi ya wale wanaominya demokrasia na kuvunja haki za binadamu.

''Tunaitaka Tanzania, kuwachukulia hatua wale wote waliohusika kuvuruga uchaguzi, kufanya vurugu na kuleta vitisho'' ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Juhudi za kumpata msemaji wa serikali ya Tanzania kuzungumzia suala hilo mpaka sasa hazijazaa matunda, na tutaendelea kuwatafuta kwa ajili ya kuzungumzia suala hilo

Haya ni moja ya maamuzi ya mwisho ya utawala wa rais Donald Trump ambaye amebakiza saa chache kuachia mamlaka ya urais. Mpaka sasa haijafahamika iwapo utawala wa rais mpya Joe Biden kama utatekeleza maamuzi hayo. Tayari ofisi ya Biden imetangaza kuwa itatengua sera kadhaa za Trump mara tu baada ya kuingia ofisini kesho.

BBC.
LUKA. 6:41-45 "Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe, ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi kilichomo katika jicho la ndugu yako".

“Why do you look at the speck in your brother's eye, but pay no attention to the log in your own eye? How can you ...
 
Kama kuna massive voter suppression waliwezaje kuchagua wewe kiazi mbatata.

"Massive" does not mean " Total" hence waliweza kuchagua you NUT! Ndio maana Democrats walishindwa TEXAS ambako voter suppression ilikuwa very significant compared to Georgia ambako Stacey Abrahams na network yake waliweza kuthibiti voter suppression significantly na hivyo Democrats kushinda!!
 
Kwa Taarifa yako waliozuiliwa wengi ni viongozi wako japo wa Tume nao wamo , kuna lundo la viongozi wanaokutumikisha , halafu kingine unachopaswa kufahamu ni kwamba ukizuiliwa na USA , basi kuna mataifa mengine kama 10 hivi hutakanyaga , omba Mungu msiugue Tezi dume au maradhi mengine ya kukata viungo kama naniliuu aliyekatwa vidole
 
Kwani demokrasia yetu lazima ifanane na yao? Nyerere alisema, democracy is not like a bottle of Cocacola that you can just import from some other place, democracy should be self grown to suite the needs of our country, they can shove their sanctions up their stinky azz holes
kama umepokea misaada mbali mbali,matundu ya choo kwa hisani ya watu wa marekani! ...kuwa mpole
 
Back
Top Bottom