Uchaguzi 2020 Marekani: Kuanzia leo, tunaweka vizuizi kwa waliohusika na kuvuruga Uchaguzi nchini Tanzania

Kwani demokrasia yetu lazima ifanane na yao? Nyerere alisema, democracy is not like a bottle of Cocacola that you can just import from some other place, democracy should be self grown to suite the needs of our country, they can shove their sanctions up their stinky azz holes
Kwani Nyerere ndiye mmiliki wa ili Taifa?
Je,bado anaishi?
 
Mbona Rais Trump amelalamika sana kuibiwa kura, wamefunga account zake ili asiwasiliane na watu wake, na hakuna mahakama, wala Vyombo vya uchunguzi vilivyochukua hatua yeyote hata kumsikiliza kama mwananchi wa kawaida licha yeye kua ni Raisi.

Watanzania wanaweza kumaliza changamoto zao wenyewe, washughulike Madai ya Rais Trump na watoe matokeo ya uchunguzi hazarani ili Dunia ijifunze kutoka kwao, kwa sasa Marekani haina uhalali wa kushauri wala kukemea nchi nyingene.waje wajifunze namna ya kufanya uchaguzi na kuheshimu viongozi.
Kumbe nawe ni box tupu namna hii?
Hivi Tweeter ni serikali ya Marekani? Unataka ukipigwa ban hapa JF kwa lugha zako zinazoenda tofauti na masharti basi ilaumiwe serikali?
Soma uelimike kwanza kabla ya kubwabwaja hadharani!
 
Upuuuuzi mtupu.

Wanahamasisha uhuru wa kujieleza, huku wameifungia acc ya twitter ya Trump.

Wanacho kihamasisha wao hawakiishi, wadeal na hali yao wanaiyoipitia sasa baada ya uchaguzi.
Mngekuwa mnaongea hivyo halafu mna uwezo wa kujisimamia mambo yenu mngeheshimiwa sana na hata uchaguzi wenu ungekuwa kioo.

Sasa mnaongea hivyo halafu mnatembeza tena bakuli kama kawaida mnaonekana mafala tu kwa kauli hizi za kijinga.

Wekeni demokrasia acheni unafiki. Bure kabisa.
 
Bora kama umeliona hilo. Wako kadhaa humu JF, we wasome mabandiko yao. Wanadhani kuvuruga uchaguzi kunaishia kwenye visa ban, watatupiga spana mpaka kwenye uchumi na afya. Kwa mfano wakizuia pesa za afya, nadhani wizara nzima ita paralyze, kwa sababu 70% ya miradi ya afya ni pesa za Wamarekani.
Usizunguke mbuyu kusema wako kadhaa humu JF, sema washabiki wengi wa CCM ni majuha kalulu ambao kujibishana nao wanaweza kukuambukiza ujinga.
Wapo wapo tuu na kufuata upepo unakoelekea hasa yule wanayemwamini kama mungu akitamka kitu
 
Kupitia akaunti yake ya Twitter, Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje, Mike Pompeo ameandika "Kuna matokeo ya kuingilia mchakato wa kidemokrasia. Kuanzia leo, tunaweka vizuizi vya visa kwa wale wanaohusika na uvurugaji wa uchaguzi nchini Tanzania. Tunabaki kujitolea kufanya kazi pamoja kuendeleza demokrasia na ustawi wa pande zote kwa nchi zetu zote mbili."

View attachment 1681412

Soma pia: Visa Restrictions on Tanzanians for Undermining the Democratic Process and Human Rights - United States Department of State
___________________________________________________

Marekani imetangaza kuwawekea vikwazo vya vya kuingia nchini humo maafisa wa Tanzania ambao nchi hiyo inawatuhumu kwa kile wanachokitaja kuwa kuharibu uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, mwaka 2020.

Maofisa hao wanatajwa kuhusika kuingilia mchakato wa uchaguzi na kuminya utekelezaji wa demokrasia.

Hata hivyo taarifa hiyo ya wizara ya mambo ya nje ya Marekani haijabainisha ni viongozi gani hasa kutoka Tanzania waliowekewa vikwazo vya kuingia Marekani.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na waziri wa mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo, Waangalizi wa uchaguzi na mashirika ya kiraia wanadai kuwepo kwa udanganyifu katika uchaguzi huo pamoja na uvunjifu wa haki za binadamu wakati na baada ya uchaguzi.

Marekani inasema kuzimwa ama kuzimika kwa mitandao, kuminywa kwa waandishi wa habari na nguvu kubwa iliyotumiwa na jeshi la Polisi kunafanya uchaguzi huo kutokua huru na wa haki.

Katika uchaguzi huo, baadhi ya wagombea kutoka vyama vya upinzani walienguliwa kwa sababu mbalimbali na wengine kukamatwa.

Tume ya uchaguzi nchini humo na hata Serikali kupitia waziri wake wa mambo ya nje, Palamagamba Kabudi ilieleza kwamba uchaguzi ulikua huru na wa haki.

Marekani inasema pamoja na hatua hii iliyochukua dhidi ya maafisa wa Tanzania, inaendelea kufuatilia kwa karibu maendeleo ya hoja hiyo, huku ikisema haitasita kuchukua hatua zaidi dhidi ya wale wanaominya demokrasia na kuvunja haki za binadamu.

''Tunaitaka Tanzania, kuwachukulia hatua wale wote waliohusika kuvuruga uchaguzi, kufanya vurugu na kuleta vitisho'' ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Juhudi za kumpata msemaji wa serikali ya Tanzania kuzungumzia suala hilo mpaka sasa hazijazaa matunda, na tutaendelea kuwatafuta kwa ajili ya kuzungumzia suala hilo

Haya ni moja ya maamuzi ya mwisho ya utawala wa rais Donald Trump ambaye amebakiza saa chache kuachia mamlaka ya urais. Mpaka sasa haijafahamika iwapo utawala wa rais mpya Joe Biden kama utatekeleza maamuzi hayo. Tayari ofisi ya Biden imetangaza kuwa itatengua sera kadhaa za Trump mara tu baada ya kuingia ofisini kesho.

BBC.
Walivyomfungia Trump account yake ya Twitter haikuwa kuminya uhuru wa kujieleza? Trump aliibiwa kura, je kwa wao ni sawa kumuibia Trump kura? Wamarekani weusi wanauliwa kila kukicha, je ni sawa tu kuondoa uhai wa mtu mweusi ndani ya USA?
 
Wasipige PIN tu ARV's, maana tutampoteza kiongozi mkuu pale ufipa.
 
Na huyu si anaondoka na Trump, sasa aache kiherehere, uchaguzi tu wa US ulikuwa na matatizo kibao, na sisi Tanzania tunaanzisha kuwanyima visa wamarekani wote waliharibu uchaguzi wa mwaka jana huko Marekani, sisi wao wakiharibu tunakaa kimya tu, ila wao wanatuangalia sisi, huko US kulitokea ghasia na vurugu kubwa sana, na sisi tunawanyima visa akiwemo Mike Pompeo mwenyewe..
 
Mikwala tuu huo ni wivu kwa sababu tunakaribisha wachina kwetu na uwekezaji
 
Mngekuwa mnaongea hivyo halafu mna uwezo wa kujisimamia mambo yenu mngeheshimiwa sana na hata uchaguzi wenu ungekuwa kioo.

Sasa mnaongea hivyo halafu mnatembeza tena bakuli kama kawaida mnaonekana mafala tu kwa kauli hizi za kijinga.

Wekeni demokrasia acheni unafiki. Bure kabisa.
Wewe chaka kabisa, uhuru wa mtu hauchagui kipato chake bali ndo demokrasia
 
Mbona Rais Trump amelalamika sana kuibiwa kura, wamefunga account zake ili asiwasiliane na watu wake, na hakuna mahakama, wala Vyombo vya uchunguzi vilivyochukua hatua yeyote hata kumsikiliza kama mwananchi wa kawaida licha yeye kua ni Raisi....
Sema waje wajifunze namna wizi unavyofanyika
 
Upuuuuzi mtupu.

Wanahamasisha uhuru wa kujieleza, huku wameifungia acc ya twitter ya Trump.

Wanacho kihamasisha wao hawakiishi, wadeal na hali yao wanaiyoipitia sasa baada ya uchaguzi.
Kama Tanzania imefanya uchunguzi na kugundua hayo iweke vikwazo kwa wamiliki wa tweeter
 
Watu hawaelewi wanafikiri ni kuzuiliwa kwenda US tu - hii ngoma inakwenda mbele zaidi kwamba US haitapokea traces zozote za ndugu zako wa damu, watoto wako, mzigo ama order yoyote toka Marekani kwa jina lako milele - hadi watakapoifuta hatua hii

Kumbuka kwamba hii ni individual - hata ukiacha kazi serikalini leo bado adhabu ipo palepale mpaka itakapotenguliwa ! - kwa hiyo kama ulikuwa na mtoto wako, ndugu yako wa damu anasema unakwenda na maji - jiandae kumpokea
 
Kupitia akaunti yake ya Twitter, Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje, Mike Pompeo ameandika "Kuna matokeo ya kuingilia mchakato wa kidemokrasia. Kuanzia leo, tunaweka vizuizi vya visa kwa wale wanaohusika na uvurugaji wa uchaguzi nchini Tanzania. Tunabaki kujitolea kufanya kazi pamoja kuendeleza demokrasia na ustawi wa pande zote kwa nchi zetu zote mbili."

View attachment 1681412

Soma pia: Visa Restrictions on Tanzanians for Undermining the Democratic Process and Human Rights - United States Department of State
___________________________________________________

Marekani imetangaza kuwawekea vikwazo vya vya kuingia nchini humo maafisa wa Tanzania ambao nchi hiyo inawatuhumu kwa kile wanachokitaja kuwa kuharibu uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, mwaka 2020.

Maofisa hao wanatajwa kuhusika kuingilia mchakato wa uchaguzi na kuminya utekelezaji wa demokrasia.

Hata hivyo taarifa hiyo ya wizara ya mambo ya nje ya Marekani haijabainisha ni viongozi gani hasa kutoka Tanzania waliowekewa vikwazo vya kuingia Marekani.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na waziri wa mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo, Waangalizi wa uchaguzi na mashirika ya kiraia wanadai kuwepo kwa udanganyifu katika uchaguzi huo pamoja na uvunjifu wa haki za binadamu wakati na baada ya uchaguzi.

Marekani inasema kuzimwa ama kuzimika kwa mitandao, kuminywa kwa waandishi wa habari na nguvu kubwa iliyotumiwa na jeshi la Polisi kunafanya uchaguzi huo kutokua huru na wa haki.

Katika uchaguzi huo, baadhi ya wagombea kutoka vyama vya upinzani walienguliwa kwa sababu mbalimbali na wengine kukamatwa.

Tume ya uchaguzi nchini humo na hata Serikali kupitia waziri wake wa mambo ya nje, Palamagamba Kabudi ilieleza kwamba uchaguzi ulikua huru na wa haki.

Marekani inasema pamoja na hatua hii iliyochukua dhidi ya maafisa wa Tanzania, inaendelea kufuatilia kwa karibu maendeleo ya hoja hiyo, huku ikisema haitasita kuchukua hatua zaidi dhidi ya wale wanaominya demokrasia na kuvunja haki za binadamu.

''Tunaitaka Tanzania, kuwachukulia hatua wale wote waliohusika kuvuruga uchaguzi, kufanya vurugu na kuleta vitisho'' ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Juhudi za kumpata msemaji wa serikali ya Tanzania kuzungumzia suala hilo mpaka sasa hazijazaa matunda, na tutaendelea kuwatafuta kwa ajili ya kuzungumzia suala hilo

Haya ni moja ya maamuzi ya mwisho ya utawala wa rais Donald Trump ambaye amebakiza saa chache kuachia mamlaka ya urais. Mpaka sasa haijafahamika iwapo utawala wa rais mpya Joe Biden kama utatekeleza maamuzi hayo. Tayari ofisi ya Biden imetangaza kuwa itatengua sera kadhaa za Trump mara tu baada ya kuingia ofisini kesho.

BBC.

Ndg zangu kuna mwenye taarifa ya majina ya waliokatazwa kwenda Marekani? Makonda alipokatazwa tulitangaziwa! Mbona leo ni maneno matupu na yamesababisha malumbano mitandaoni?

Jambo hili linapunguza mahusiano ya kidiplomasia ya nchi hizi mbili. Kwanini nchi kubwa kama Marekani iiagize nchi nyingine kwenye mtandao wa kijamii? Tena kwenye ma suala very sensitive ya diplomasia.

Naomba tulikadili hili.
 
Na huyu si anaondoka na Trump, sasa aache kiherehere, uchaguzi tu wa US ulikuwa na matatizo kibao, na sisi Tanzania tunaanzisha kuwanyima visa wamarekani wote waliharibu uchaguzi wa mwaka jana huko Marekani, sisi wao wakiharibu tunakaa kimya tu, ila wao wanatuangalia sisi, huko US kulitokea ghasia na vurugu kubwa sana, na sisi tunawanyima visa akiwemo Mike Pompeo mwenyewe..
[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Back
Top Bottom