Rais wa Marekani, Donald Trump, ameliarifu Bunge la nchi hiyo kuhusu mpango wa kuiondoa Rwanda na Afrika Kusini katika mpango wa upendeleo wa kibiashara wa Afrika (AGOA), kuanzia Januari 01, 2027.
AGOA ni mpango unaozipa nchi za Afrika zinazokidhi vigezo fursa ya kuuza maelfu ya bidhaa nchini Marekani bila kutozwa ushuru wa forodha.
Katika taarifa yake, Mwakilishi wa Biashara wa Marekani, Jamieson Greer, amesema tathmini ya kila mwaka imebaini kuwa Rwanda na Afrika Kusini zinajihusisha na vitendo vinavyokiuka masharti ya mpango huo. Ameongeza kuwa utawala wa Trump tayari umezitaarifu nchi hizo kuhusu uamuzi huo.
Sababu zilizotolewa na Marekani ni pamoja na vikwazo katika biashara na uwekezaji wa Marekani, pamoja na wasiwasi kuhusu masuala ya usalama wa taifa na maslahi ya sera za kigeni katika eneo hilo.
Kwa upande wa Rwanda, Marekani pia imeeleza wasiwasi kuhusu hali ya haki za binadamu, uwepo wa vyama na mitazamo mbalimbali ya kisiasa, utawala wa sheria na haki za wafanyakazi.
Hatua hiyo inakuja takribani wiki moja baada ya Marekani kuiwekea vikwazo Wizara ya Ulinzi ya Rwanda, kupitia Wizara yake ya Fedha, kwa madai ya kuhusika katika uasi wa makundi yenye silaha mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Wizara ya Fedha ya Marekani ilidai kuwa Wizara ya Ulinzi ya Rwanda ilielekeza maelfu ya wanajeshi kushirikiana na waasi wa M23 katika mapigano mashariki mwa DRC, huku ikiwasambazia silaha, vifaa, msaada wa usafirishaji, mahitaji ya kijeshi na mafunzo.