Washington, Serikali ya Marekali imeridhia maombi ya Austalia ya kununua makombora ya masafa marefu ya JASSM-ER yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 235 ili kuweza kukabiliana na kitisho cha China Asia Pacific.
Makombora haya ya kimkakati yana uwezo wa kusafiri hadi umbali wa kilometa 935 kwa kurushwa kupitia ndege za kivita za Austalia chapa F-35 na F/18 .
Idhinisho hili la uuzaji wa silaha litaisaidia pakubwa Australia kupambana na China endapo mgogoro mkubwa utaibuka kati ya China na Taiwani na hivyo kuzifanya ndege za Australia kuweza kuishambulia Uchina bila kuhitaji ujazaji wa mafuta angani.
Picha ya F-35 ikiwa imebeba kombora la masafa marefu la JASSM-ER.
JASSM-ER ni kombora la masafa marefu linalotengenezwa na Lockheed Martin, ambalo lina kilogram 450 na uwezo mkubwa wa kushambulia lengo pasipo kuonekana kwenye rada.
Makombora haya yametengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu ili kuweza kukabiliana na kitisho cha mifumo imara ya ulinzi wa anga kama S300, S400, na S500.