Marekani kuongoza ugawaji misaada Gaza ikiitaka Israel isisogelee karibu.Hamas na UN wanawasi wasi na mpango huo.

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
10,509
Reaction score
16,734
Mwanadiplomasia wa Marekani nchini Israel amefichua mpango ambao utaanza hivi punde wa kuingiza misaada eneo la Gaza ili kuokoa maisha.
Huckabee amesema mpango huo utashirikisha makampuni binafsi na kwamba Israel haitohusika isipokuwa kwenye ulinzi tu kwani hilo ni eneo la vita bado.Mpango huo unakwenda sambamba na ziara ya Trump inayoanza hivi karibuni mashariki ya kati.
Maafisa kutoka Hamas na mashirika ya umoja wa mataifa wamesema mpango huo unafanana sana na ule uliotajwa na Israel hivi karibuni ambao utakuwa ukitoa misaada hiyo kibaguzi na kuwanyima wahitaji wengi misaada hiyo.
Hamas na UN wamesema mpango huo unaweza usifanikiwe bila wao kushirikishwa kikamilifu kutokana na uzoefu wao.
Kwa vyovyote vile mpango huu utaleta nafuu kwa malaki ya wapalestina wanaokaribia kufa kwa njaa na itakuwa ni pigo kiasi fulani kwa malengo Israel iliyojipangia mwanzoni mwa vita.
Makundi ya kihafidhina ya kiyahudi tayari nayo yamelaani mpango huo bila kuhusisha na masharti ya kuachiwa mateka wote waliobaki.
 
Teh! Hamas wanataka wao washirikishwe! Sijui huo ubaguzi wanaouzungumzia wa mgao wa chakula toka kwa makafir ni nani wanahisi atabaguliwa? Majambazi kweli hao.
 
Hao magaidi ndio hupora chakula cha msaada na kutokomea nacho kusikojulikana huku wakiacha watu wanaosingizia kuwapigania wakifa na njaa.
 
Mwanadiplomasia wa Marekani nchini Israel amefichua mpango ambao utaanza hivi punde wa kuingiza misaada eneo la Gaza ili kuokoa maisha.
Huckabee amesema mpango huo utashirikisha makampuni binafsi na kwamba Israel haitohusika isipokuwa kwenye ulinzi tu kwani hilo ni eneo la vita bado.Mpango huo unakwenda sambamba na ziara ya Trump inayoanza hivi karibuni mashariki ya kati.
Maafisa kutoka Hamas na mashirika ya umoja wa mataifa wamesema mpango huo unafanana sana na ule uliotajwa na Israel hivi karibuni ambao utakuwa ukitoa misaada hiyo kibaguzi na kuwanyima wahitaji wengi misaada hiyo.
Hamas na UN wamesema mpango huo unaweza usifanikiwe bila wao kushirikishwa kikamilifu kutokana na uzoefu wao.
Kwa vyovyote vile mpango huu utaleta nafuu kwa malaki ya wapalestina wanaokaribia kufa kwa njaa na itakuwa ni pigo kiasi fulani kwa malengo Israel iliyojipangia mwanzoni mwa vita.
Makundi ya kihafidhina ya kiyahudi tayari nayo yamelaani mpango huo bila kuhusisha na masharti ya kuachiwa mateka wote waliobaki.
Acheni uongo, nimeiona hii taatifa kwenye Aljazira, markani itagawa vyakula chini ya ulinzi wa askari kutoka Israel lakini Israel haitajihusiha na ugawaji huo " Israel itatoa ulinzi kuhakikisha midaada haijibiwi na magaidi
 
Ngoja tuone itakavyokuwa.
 
Hapi vyakula vishawekewa sumu kama zote.

Hawatazaliana hovyo,wengine hawatadisa
Akili kama zako ndio zimesababisha hadi leo vita haiishi..
Hakukua na vita wanajiona wana nguvu wakavamia na kuteka.

Walipoambiwa achieni mateka wakakataa wakaambiwa tutapigana vita wakasema njoeni tuna uwezo.. wakapata bichwa kutoka kwa Iran na waarabu wenzao.

Wakalia njaa wakapewa chakula waliposhiba wakaanza kulalamika wanauliwa na njaa chakula hawapati wakati kihesabu wamepata chakula kingi kuliko kabla ya vita.. sasa wana matumbo kumi kumi sijui.. Israel akasema mnakufuru kazuia.. mbwai mbwai tu.. andha kanoon huwezi mhukumu kwa kosa moja mara mbili.

Sasa wanataka kuwapa tena chakula mnasema kina sumu.. huku hamjui chakula kinatokea nchi za waarabu na bara ulaya na asia na Marekani na Africa pia huwa vinapimwa.

Alafu si mnasema Genocide mmeisha chakula cha nini sasa wakati mnasema mmeuliwa wote kumbuka Idadi ya Raia Gaza imeongezeka kwa wingi tokea October 7 2023. Vice verse Genocide
 
Ujinga kweli, yaani wanakupiga halafu wanakwambia wanakusaidia... Waliibomoa Libya iliyokuwa na Deni 0 halafu baadae wanasema wanaijenga ikiwa na Deni sawa na 100% ya GDP yake...
 
Mkuu wanasema bora kujaribu, kuliko kujaribu kushindwa.
Msaga sumu sili chakula chake, kifo kipo tu lakini bora nichelewe.
Hawa watu wanampango kuwahamisha raia wa palestina kutoka gaza ili waijenge kama mji wa biashara.
Leo wagawe chakula Gaza halafu wapokee hicho chakula watakuwa wajinga.
 
Mwanadiplomasia wa Marekani nchini Israel amefichua mpango ambao utaanza hivi punde wa kuingiza misaada eneo la Gaza ili kuokoa maisha.
Huckabee amesema mpango huo utashirikisha makampuni binafsi na kwamba Israel haitohusika isipokuwa kwenye ulinzi tu kwani hilo ni eneo la vita bado.Mpango huo unakwenda sambamba na ziara ya Trump inayoanza hivi karibuni mashariki ya kati.
Maafisa kutoka Hamas na mashirika ya umoja wa mataifa wamesema mpango huo unafanana sana na ule uliotajwa na Israel hivi karibuni ambao utakuwa ukitoa misaada hiyo kibaguzi na kuwanyima wahitaji wengi misaada hiyo.
Hamas na UN wamesema mpango huo unaweza usifanikiwe bila wao kushirikishwa kikamilifu kutokana na uzoefu wao.
Kwa vyovyote vile mpango huu utaleta nafuu kwa malaki ya wapalestina wanaokaribia kufa kwa njaa na itakuwa ni pigo kiasi fulani kwa malengo Israel iliyojipangia mwanzoni mwa vita.
Makundi ya kihafidhina ya kiyahudi tayari nayo yamelaani mpango huo bila kuhusisha na masharti ya kuachiwa mateka wote waliobaki.
Nyani wale wale isipokuwa tu pori ndiyo tofauti.
Ubinadamu ni kazi/The humanity is work.
 
Msaga sumu sili chakula chake, kifo kipo tu lakini bora nichelewe.
Hawa watu wanampango kuwahamisha raia wa palestina kutoka gaza ili waijenge kama mji wa biashara.
Leo wagawe chakula Gaza halafu wapokee hicho chakula watakuwa wajinga.
Hivi we umepata kujua kwanini taifa takatifu km israel, linashirikiana na taifa la marekani ambalo ndo kinara wa kupushi ajenda za kishetani, je! kweli mungu na shetani wanaweza kushirikiana?.
 
Back
Top Bottom