Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Marekani inapanga kupunguza kwa kiasi kikubwa idadi ya balozi zake barani Afrika zinazoshughulikia maombi ya visa, hatua inayotarajiwa kuongeza udhibiti kwa wanaotafuta vibali vya kuingia nchini humo.
Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Habari la Associated Press (AP), mpango huo utaifanya Marekani kupunguza balozi zinazotoa huduma za visa kutoka takriban balozi 50 zilizopo sasa hadi kufikia 20.
Iwapo hatua hiyo itatekelezwa, waombaji wa visa katika baadhi ya nchi za Afrika watalazimika kusafiri kwenda mataifa jirani kufuata huduma hiyo, jambo linaloweza kuongeza gharama na muda wa kusubiri huduma.