Marekani kutoa pipa milioni 1 za mafuta kwa siku

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Rais wa Marekani, Joe Biden ametangaza kuwa pipa milioni 1 za mafuta zitatolewa kutoka kwa hifadhi ya mafuta ya taifa hilo kila siku kwa kipindi cha miezi sita ili kusaidia kupunguza bei ya mafuta ambayo imekuwa ghali kwa waendesha magari wa nchi hiyo.

Biden amesema mapipa milioni 180 kutoka ghala hilo la mafuta linalotumiwa wakati wa dharura, zitasaidia kukabiliana na athari za uvamizi wa Ukraine ulioamrishwa na Rais wa Urusi, Vladmir Putin kwenye soko la kimataifa la mafuta.

“Bei zetu za mafuta zinaongezeka kutokana na vitendo vya Putin. Hakuna usambazaji wa kutosha wa mafuta. Na kikomo ni kwamba, ikiwa tunataka kupunguza bei za mafuta, tunahitaji usambazaji wa kutosha wa mafuta sasa hivi,” - Biden.

Baadhi ya wataalamu wa masuala ya nishati wanasema mafuta hayo kutoka kwenye hifadhi hayatapunguza vya kutosha athari za bei ghali ya mafuta kwenye soko la kimataifa.

Wabunge wa Chama cha Republican wanadai sera kuhusu nishati za utawala wa Rais Biden ndizo za kulaumiwa kutokana na gharama kubwa ya mafuta na gesi badala ya vitendo vya Rais wa Urusi.

Source: Aljazeera
 
Baada ya hio miezi 6 tutaendelea kuteseka!!?
VIVA PUT IN
 
Huyu babu ajiandae kuwajibishwa tu, kawaingiza wananchi wake kwenye matatizo kwa tamaa za serikali yake......
 
Mafuta ghafi yanampa sana jeuri Putin. Lakini hawa wazungu hawakuyajua haya ya mafuta kuja kuleta shida?
 
Huyu babu ajiandae kuwajibishwa tu, kawaingiza wananchi wake kwenye matatizo kwa tamaa za serikali yake......
Miscalculations
Walijua vikwazo vitamuumiza zaidi Putin.
Badala yake vikwazo vimewakwaza wenyewe
Literally speaking huwe kuweka vikwazo vikali kiasi kile kwa taifa ambalo ni member wa G7..G20 kama Mrusi halafi msiumie. Mchango wake kwenye uchumi wa taifa ni mkubwa kiasi kwamba hauzibiki kwa haraka
 
Rais wa Marekani, Joe Biden ametangaza kuwa pipa milioni 1 za mafuta zitatolewa kutoka kwa hifadhi ya mafuta ya taifa hilo kila siku kwa kipindi cha miezi sita ili kusaidia kupunguza bei ya mafuta ambayo imekuwa ghali kwa waendesha magari wa nchi hiyo.

Biden amesema mapipa milioni 180 kutoka ghala hilo la mafuta linalotumiwa wakati wa dharura, zitasaidia kukabiliana na athari za uvamizi wa Ukraine ulioamrishwa na Rais wa Urusi, Vladmir Putin kwenye soko la kimataifa la mafuta.

“Bei zetu za mafuta zinaongezeka kutokana na vitendo vya Putin. Hakuna usambazaji wa kutosha wa mafuta. Na kikomo ni kwamba, ikiwa tunataka kupunguza bei za mafuta, tunahitaji usambazaji wa kutosha wa mafuta sasa hivi,” - Biden.

Baadhi ya wataalamu wa masuala ya nishati wanasema mafuta hayo kutoka kwenye hifadhi hayatapunguza vya kutosha athari za bei ghali ya mafuta kwenye soko la kimataifa.

Wabunge wa Chama cha Republican wanadai sera kuhusu nishati za utawala wa Rais Biden ndizo za kulaumiwa kutokana na gharama kubwa ya mafuta na gesi badala ya vitendo vya Rais wa Urusi.

Source: Aljazeera
Tanzania kutoa mapipa manne kwa wiki katika jitihada za kupunguza kupanda kwa bei ya mafuta barani Asia.
 
Back
Top Bottom