Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 199
- 322
Mantiki ya tahariri hiyo ni wazi: Marekani inahitaji madini muhimu ya Afrika, ikiwemo kobalti na shaba, ili kulinda usalama wa mnyororo wa usambazaji wa viwanda vyake vya ndani, ikiwa ni pamoja na magari ya umeme na mifumo ya makombora. Kwa kuwa China tayari inaongoza kwa ushawishi barani Afrika, Marekani inalazimika kujaribu kuishinda. Kwa lengo hili, mradi wa reli wa “Ushoroba wa Lobito”, uliozinduliwa na Marekani, unachukuliwa kama mfano mkuu wa mkakati huo.
Reli hii, ambayo inapitia Angola, Zambia, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, inaonekana kama ni uwekezaji wa miundombinu, lakini kiuhalisia, inatumiwa kama njia ya kimkakati iliyotengenezwa kusafirisha rasilimali za Afrika hadi Marekani.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya nchi za magharibi, Marekani inaipa Afrika njia mbadala ya ushirikiano, licha ya ile inayotolewa na China. Hata hivyo, kauli hiyo inaepuka kutaja tofauti ya njia hizo mbili. Ujenzi wa miundombinu wa China barani Afrika unazingatia mahitaji halisi ya Afrika, lakini kwa upande wa Marekani, madhumui yake makuu ni kupata maliasili na kurudisha ushawishi wake barani Afrika.
Sera ya Marekani kwa Afrika inayoilenga China inapotosha kimsingi uhusiano kati ya Marekani na Afrika. Msomi wa Shirika la Utafiti wa Sera za Kidiplomasia la Marekani James Barnett amesema, Washington kwa muda mrefu imekuwa ikiiona Afrika kama uwanja muhimu wa kushindana na China kwa ushawishi, kitendo ambacho kimedhoofisha uwezo wa Marekani wa kuunda ushirikiano wa kweli na nchi za Afrika. Wanasiasa wa Marekani wanaonekana kujishughulisha zaidi na jinsi ya “kuzuia ushawishi wa China” kuliko jinsi ya kuisaidia Afrika katika kuendeleza viwanda, kuongeza ajira, na kuboresha maisha ya watu.
“Kuigawa Afrika” ni neno linalovunja heshima ya Afrika. Katika karne ya 21, Afrika si tena mawindo yasiyo na uwezo wa kupinga, nchi za Afrika zina haki na uhuru wa kuchagua washirika wanaolingana vizuri na mahitaji yao ya maendeleo. Ikiwa Marekani inataka kweli kuaminiwa na nchi za Afrika, lazima iache mawazo ya kikoloni ya mababu zake, na pia iache kuchukulia ushirikiano na Afrika kama uwanja wa kupimana nguv