Dalton elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 373
- 829
Moto mkali umezuka katika eneo la juu la Pacific Palisades huko Los Angeles, na kusababisha uhamishaji wa hofu.
Moto huo, unaosababishwa na upepo mkali wa Santa Ana , tayari umeteketeza karibu ekari 3,000 (hekta 1,200) na kuharibu nyumba nyingi.
Takriban wakaazi 30,000 wameamriwa kuhama huku wengi wakitelekeza magari yao na kukimbia kwa miguu.
Eneo hilo, ambalo lina nyumba za watu mashuhuri, limeathiriwa vibaya na moto huo unaoenea kwa kasi.
Gavana wa California, Gavin Newsom, ametangaza hali ya dharura na kuwataka wakazi kufuata maagizo ya uhamishaji ili kuhakikisha usalama wao. Tayari kikosi cha Zimamoto cha Los Angeles kiko kwenye eneo hilo kupambana na moto huo na kuokoa maisha na mali.