Marekani: Mtoto wa miaka miwili afariki kwa kula nepi

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,455
Reaction score
5,134
​

Tukio la kusikitisha limeripotiwa kutoka katika Jimbo la Indiana Nchini Marekani ambapo Mtoto wa miaka miwili amefariki dunia kutokana na hali mbaya ya malezi na ukosefu mkubwa wa chakula Nyumbani kwao, taarifa za awali zinaeleza kuwa Wazazi walikuwa wakiwanyima chakula Watoto wao hali iliyosababisha mateso makubwa kwa Watoto hao.

Kwa mujibu wa taarifa ya Polisi na nyaraka za Mahakama Mtoto huyo aliyefahamika kwa jina la Erik Reichard alikutwa akiwa na uzito mdogo sana wa takribani kilo 6.8, pamoja na majeraha mwilini na alama za kung’atwa na wadudu, wachunguzi wanaeleza kuwa kutokana na njaa kali Mtoto huyo alifikia hatua ya kula vipande vya nepi na ukuta wa Nyumba.

Hata hivyo, inaelezwa kuwa Wazazi hao walichelewa kwa takribani saa 14 kabla ya kupiga simu ya dharura baada ya kugundua Mtoto wao hana uhai hali iliyozua maswali mazito kuhusu uzembe na uangalizi mdogo ndani ya Familia hiyo, Polisi walipofika walijaribu kumuokoa Mtoto huyo lakini alithibitishwa kufariki tayari.

Uchunguzi zaidi ulibaini kuwa Nyumba hiyo ilikuwa katika hali mbaya sana ikiwa imejaa uchafu kinyesi wadudu pamoja na mabaki ya nepi na vipande vya ukuta ndani ya Vyumba vya Watoto, huku Watoto wengine waliokutwa humo waliondolewa mara moja huku mmoja wao akipelekwa hospitali kutokana na utapiamlo mkali na upungufu wa maji mwilini.

Pamoja na hayo, taarifa zimeonyesha kuwa Chumba cha Wazazi kilikuwa katika hali safi na nadhifu tofauti kabisa na mazingira ya Watoto jambo linaloashiria uwezekano wa Wazazi hao kuwa na hali nzuri lakini wakishindwa au wakipuuzia kuwapatia Watoto wao mahitaji ya msingi ikiwemo chakula hali iliyopelekea Watoto kufikia hatua ya kula nepi hatimaye kusababisha kifo cha mtoto huyo na sasa Wazazi wanakabiliwa na mashtaka ya mauaji na kutelekeza Watoto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…