Hatuwezi kuacha kufanya nao kazi, sababu hatujitoshelezi katika SCIENCE & TECHNOLOGY.
Taifa Kubwa ni lile Taifa ambalo linalojiweza sana katika Science & Technology.
Ukiwa na Sayansi na Teknolojia bora basi itakufanya uendelee katika nyanja zifuatazo :-
• MILITARY (Ukiwa na Teknolojia bora basi utakuwa na zana bora za kisasa unazoziunda mwenyewe iwe ni Computerized & Software Systems, Jet-fighters, Drones, Biological Weapons etc.)
• INDUSTRIAL REVOLUTION (nchi kubwa zote ni nchi zilzoendelea kiviwanda, hususani Manufacturing industries)
• HEALTHCARE SYSTEM ( sayansi na teknolojia bora itakufanya uwe na Mfumo Bora wa Afya, Vifaa-Tiba Bora, Taaluma Bora ya Afya pia)
• AGRICULTURAL SECTOR (kilimo kinaleta chakula, chakula ni Uhai.. Sayansi na Teknolojia bora husaidia sekta ya kilimo na kuongeza Uzalishaji kwa mbinu za kisasa)
• RESEARCH & DEVELOPMENT (nchi kubwa duniani huwa ni zile zinazofanikiwa katika Tafiti zao za Kisayansi)
• ENERGY (sayansi na teknolojia bora itasaidia katika Uzalishaji wa Nishati, Nishati ni muhimu katika Viwanda, Matumizi ya Majumbani etc. Umeme wetu bado wa kusuasua na haujasambaa nchi nzima)
Nchi za Kiafrika badooooo sana hazijafinikiwa katika Sayansi na Teknolojia. Hahahah!! Tumeachwa nyuma miaka kama Mia Moja Tisini (190) hivi....
Ukifanikiwa katika sekta hizo basi VIWANDA (Manufacturing industries na Processing Industries) utakuwa navyo vingi na Mzunguko wa Pesa utakuwa Mkubwa, Sekta ya Afya itakuwa Bora, Umaskini wa Kipato kwa Mwananchi Mmoja Mmoja Utapungua Sana, na FURSA ZA BIASHARA na AJIRA zinakuwa nyingi pia sababu MZUNGUKO WA PESA utakuwa mkubwa.