Tetesi: Marekani na Ulaya hazitautambua Uchaguzi Mkuu 2025 ikiwa CHADEMA haitashiriki!!

Tunachagua Rais wa JMT na SMZ kwa hiyo wasituchoshe na kiherehere cha mambo ya nchi yetu wakae mbali na sisi maana wamezidi sana.

OCTOBER 2025 TUNASIMAMA NA MAMA DR. SAMIA SULUHU HASSAN TUNATIKI ZOTE✅✅✅🇹🇿
 
Sisi Tanzania ni nchi huru, hatuhitaji hao wazungu kutambua au kutotambua viongozi wetu.. Wao wakitambuana wenyewe kwa wenyewe inatosha.
 
Mtajadili na nani wakati mtu anayepaswa kuongoza majadiliano hana muda wa kusikiliza mawazo kinzani ya kujenga nchi badala yake anaishi kwa kuwasikiliza machawa ?
 
CCM wanasema hata wasipotambua, China, Korea Kaskazin, Urusi wapo.

Kanyaga twende wajomba - kunakaribia kupambazuka.
 
Wewe umebahatika kuwa karibu na mama Abdul. hauna tatizo hata kidogo. Wengine tuna shida kubwa sana.
Sipo karibu na Mama Abdul, nayaona mengi anayoyafanya Samia. Ameendeleza pale alipoishia RIP Magufuli.

Daraja la Busisi limemalizika, Uwanja wa ndege Msalato unakaribia kumalizika.
 
Ukigusa maslahi yao hao wanaokusaidia ndipo yote hayo yatakapokuja ila kama unakula nao ata uchinje kijiji au vhama kizima cha upinzani watabweka tu kudanganya wajinga nakukaa kimya.Zimbabwe walipowafukuza wazungu ndipo mugabe akakutana na rungu lao ila uko nyuma walikua marafiki wakubwa pamoja nakwamba mugabe alikua mbabe kwa wapinzani wake.
 
Sipo karibu na Mama Abdul, nayaona mengi anayoyafanya Samia. Ameendeleza pale alipoishia RIP Magufuli.

Daraja la Busisi limemalizika, Uwanja wa ndege Msalato unakaribia kumalizika.
Daraja la Busisi linakusaidia nini? Uwanja wa ndege wa Msalato unakusaidia nini wewe mlala hoi? Kuna mambo mengi ya kusaidia watu waweze kujisaidia wenyewe, including upholding rule of law, kuondoa corruption na mengineyo mengi. Tatizo la watanzania siyo Daraja la Busisi au Msalato airport.....hizo zilikuwa zinatakiwa ziwepo baada ya miaka kumi ya uhuru. Mambo muhimu ni kuimarisha Elimu yetu, kutengeneza ajira, utawala wa sheria na kufuata katiba na haki. Hayo yote mengine yangekuja tu. Nchi imekuwa na ufisadi mkubwa wewe unazungumzia kiwanja cha ndege na daraja.....Vipi kuhusu maisha ya watu? Bado watu wanaishi maisha duni kwenye nyumba za nyasi, ukiwa na uwezo wa kujenga nyumba nzuri utafuatwa na misururu ya kodi, ukitaka kujenga ghorofa ndiyo utakoma. Bado nchi yetu imekuwa ya ovyo.
 
Wewe ni wale wale mnaoshinda nyuma ya keyboard mkirusha picha na matukio ya ajabu yanayoendelea dunia nzima.

Daraja la Busisi linaunganisha Afrika ya Mashariki, ni muhimu kwenye sekta ya uchukuzi. Msalato kufunguliwa ni hatua kubwa kwenye uchukuzi.

Ajira zinakuwepo katika taifa lenye maendeleo ya viwanda, na vinafunguliwa kama uyoga kila kona ya TZ kwa sasa. Nyumba za nyasi zinapungua kadri siku zinavyopita.

Bila kodi hata hivyo viwanja vya ndege na madaraja huwezi kujenga, hakuna mahali penye maendeleo pasipo na ufuatiliaji wa ulipaji wa kodi.
 
Hizo ni doto tu za Alinacha.
 
Tunachagua Rais wa JMT na SMZ kwa hiyo wasituchoshe na kiherehere cha mambo ya nchi yetu wakae mbali na sisi maana wamezidi sana.

OCTOBER 2025 TUNASIMAMA NA MAMA DR. SAMIA SULUHU HASSAN TUNATIKI ZOTE✅✅✅🇹🇿
Eeehh Oktoba mkatiki tu ,ila mishe kusema, sisi tulosemà sio Wazalendo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…