#COVID19 Marekani: Rais Biden ataka kutolewa Dola 100 kwa kila atakayepata chanjo ya COVID-19

Subirini kuna siku utakuja ugonjwa kama Ndui kisha akili za watu kama wewe zitakaa sawa.

Ugonjwa wa Ndui ulitishia kuangamiza entire population ya dunia kipindi hicho lakini chanjo iliingilia kati na ku-rescure situation.Siku zote katika maisha yako heshimu sana vitu viwili:
1.Mungu
2.Sayansi
 
Hii ni biashara ya upaku iliyoboreshwa....mnamkumbuka yule jamaa wa songea na biashara yake ya mahindi...yaani nipe nikupe pesa tupate,ikiwezekana ata watu wafee..

Kwa kifupi ni kwamba kuna watu tayari wamesha poteza pesa zao nyingi katka kuwekeza ktka hii biashara Sasa watatumia kila mbinu warudishe pesa zao kwa faida (RETAIN ON PROFIT)....
 
Sio hongo....ni motisha ili wakachanjwe
 
Gwajima anapata umarufu kwa kupotosha umma ya wa Tanzania wengi wasio jielewa hi ni cheap popularity au political capital inayo tafutwa wengine wameanza kumpendekeza apewe Uraisi 2025......hapo hapo CCM inagawanyika, TISS izuie upotofu wa Gwajima una mazara zaidi ya chanjo,.....ila najiuliza laiti angekua Sh Ponda na msimamo kama huo sijui kama wange ka kimya kiasi hiki
 
Mwenzangu na mimi mwingjne aliyeingizwa mkenge huyu hapa!
Your browser is not able to display this video.

Sisi Tz yatuhusu Nini?
Si mnapenda kusema Tanzania sio kisiwa?, Mzigo wa chanjo milioni moja ulitoka marekani! Na mbinu anayoitumia kushawishi chanjo ameiweka wazi! Tafakari!
 
Sio hongo....ni motisha ili wakachanjwe
Nenda Takukuru ukapate maneno mengine yanayotafisiriwa kuwa ni rushwa!! Haya tukubali kuwa ni "motisha", basi unajisikiaje viongozi wapewe "motisha" ya kuwahamasisha watu kuchanjwa ya dola 100 kwa kila mtu atakayekubali kuchanjwa! Zikiisha chanjo zote 1,000,000 wanapewa "motisha" ya dola 1,000,000 × 100 = $100,000 000!
 
Unajua huko marekani wataalam kama hawa waliobobea wamewafungua watu macho watu macho na si rahisi kurubuniwa. Anaanza kwa kukumwagia CV yake kwanza ili usidhani kuwa ni mbumbumbu mwenzio. Ukitaka kujibu hoja zake na wewe tupe CV yako kwanza! Walioingizwa mkenge saa hii wanajuta!! Halafu huna pa kulalamika na wanakuambia " si ulikubali mwenyewe? si ulisaini mwenyewe? Baada ya kuona kasi ya kujitokeza kuchanja imepungua sana ndio amekuja na plan 2 ya kupewa kitu kidogo, na kuna kila dalili hata hiyo plan 2 ya kutoa kitu kidogo atashindwa!! Zaidi ya nusu ya wamarekani wamegomea chanjo!! Elimika bure toka kwa daktari bingwa huyu hapa!!
 

Attachments

  • 2782210-62048362544228fdaa1c25b4a6a16ef4.mp4
    5.1 MB
Mimi wanipe chanjo tu hela zao si lazima 😂
 

Sipati picha kwa sh ponda wangemfanya nini 😱 kama hakuitwa gaidi 😂
 
We jamaa nenda kachanjwe acha kupotosha watu. Leo kuna dose milioni 1 mnahangaika kumbwela mbwela ipo siku mtazigombania dose na hazitotosha

Acha kushikiwa akili kijinga. Vaa nguo nenda kachanjwe
 
Gwajima yupi unamzungumzia hapa!?
 
Wamarekani wenyewe wanakataa kichanjwa kwa sababu wanazozijua wao kwann sis tumeletewa na tumeanza kuitumia ?
 
Ni kweli na ikumbukwe waziri mkuu wa Uingereza alipata maambukizi juu ya kichanjwa ila haikusaidia ukiniambia chanjo zao ni fek nakubali
 
Sasa tatizo lipo wapi ikiwa corona nayo ni hatari watu wanakufa na ikiwa chanjo imeoneka ndio kuzuia hivyo vifo kwanini watu wakatae kutumia kitu kama hicho cha kuzuia vifo? ni kwamba wamekubali tu kufa?
 
Sasa tatizo lipo wapi ikiwa corona nayo ni hatari watu wanakufa na ikiwa chanjo imeoneka ndio kuzuia hivyo vifo kwanini watu wakatae kutumia kitu kama hicho cha kuzuia vifo? ni kwamba wamekubali tu kufa?
Kwani wewe huamini kuwa duniani kuna wajinga na wapumbavu au?
 
Marekani anagawa hela huko ili kushawishi watu kuchanjwa ila sisi huku tunaangaika na Gwajima halafu ushawishi zero.
 
Kwani wewe huamini kuwa duniani kuna wajinga na wapumbavu au?
Wajinga ni watu wa aina gani ambao umewakusudia wewe? Kwa sababu nikiangalia kwa wanaopinga na wanao kukubali chanjo kunapatikana makundi yote ya watu yani huwezi kusema kwamba kundi fulani lina msimamo fulani kuhusu chanjo kwa sababu ni aina fulani ya watu tofauti na upande mwengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…