MAREKANI: Rwanda inahatarisha Usalama wa eneo la Afrika Mashariki

MAREKANI: Rwanda inahatarisha Usalama wa eneo la Afrika Mashariki

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,112
Reaction score
34,951
1765654477169.png

Haya yanajiri siku chache tu baada ya kusainiwa makubaliano ya amani yaliosimamiwa na Marekani.

Awali balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Mike Waltz, aliliambia Baraza la Usalama la Umoja huo kwamba, badala ya kupiga hatua kuelekea amani, Rwanda inaongoza eneo hilo kuelekea ukosefu wa utulivu na vita.

Pia amesema Marekani ina wasiwasi mkubwa na inazidi kukatishwa tamaa kwa kuzuka upya kwa ghasia Mashariki mwa Kongo.

Waltz anadai kuwa vikosi vya ulinzi vya Rwanda vimetoa msaada wa vifaa, mipangilio na mafunzo kwa M23 pamoja na kuisadia vitani. Hata hivyoRwanda imeendelea kukanusha kuliunga mkono kundi hilo la waasi.
Chanzo. DW Kiswahili
 
kumuamini mtu kama huyu you must be high on something ilegal
 

Attachments

  • 020fb9b738fc094928887e8de02a7353_1765250875397.mp4
    977.4 KB
View attachment 3515273
Haya yanajiri siku chache tu baada ya kusainiwa makubaliano ya amani yaliosimamiwa na Marekani.
Awali balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Mike Waltz, aliliambia Baraza la Usalama la Umoja huo kwamba, badala ya kupiga hatua kuelekea amani, Rwanda inaongoza eneo hilo kuelekea ukosefu wa utulivu na vita.
Pia amesema Marekani ina wasiwasi mkubwa na inazidi kukatishwa tamaa kwa kuzuka upya kwa ghasia Mashariki mwa Kongo.
Waltz anadai kuwa vikosi vya ulinzi vya Rwanda vimetoa msaada wa vifaa, mipangilio na mafunzo kwa M23 pamoja na kuisadia vitani. Hata hivyoRwanda imeendelea kukanusha kuliunga mkono kundi hilo la waasi. Chanzo.DW Kiswahili

Rwanda wanajielewa hawana RASIMALI za kutosha lakini jirani anazo, hasaidii wananchi wake kunufaika nazo kwa Nini M23 wasiingize kuchukua mzigo

Hata hapa TZ ipo siku M23 itazaliwa maana RASIMALI zilizopo hazimsaidii Mwananchi masikini kupunguza ugumu wa Maisha Bali zinauzwa kama njugu...hii Hali itafikia hatua watu watachoka na wakichoka hizo risasi zenu hazitawatisha tena ndiyo hapo utakuta ndani ya Jeshi uasi utakapotokea na ukitokea uasi ndani ya Jeshi basi tumekwisha
 
Kwa hali iliyopo mitaani kikitokea kikundi kama m23 vijana asilimia 90 watajiunga ..Vijana huku mtaani wamekosa silaha tuu, wakizipata hali itakua tete sana, Nashauri muafaka upatikane kwenye hili, mianya ya kupata silaha hata izuiwe vipi kama wananchi wanakinzana na serikali lazima tuu kuna mianya ya kupata silaha itatokea ..
 
usichojua ni kwamba
TRUMP kasaini DEAL na KAGAME deal kubwa la 40% kwa 60%

anachofanya TRUMP ni kutuchezea akili anadhami watu ni watoto wadogo
kile walichokubaliana na KAGAME anakifahamu

yake makaratasi waliotunesha makubaliano ya kumaliza vita ni ujinga
KAGAME si mpuuzi hvyo aingie makubaliano na MAREKANI kisha ageuke

muda si mrefu MAREKANI atajitia kwenda kulinda kile atakachokiita UKWIUKAJI WAMAKUBALIANO CONGO

kama kweli alikuwa na nia ya AMANI africa kwanza angewaita WASUDANI wakae chini wayamalize kati ya RSF na SAF kule ndiko kunahitaji msaada wa haraka zaidi wa AMANI

Vita CONGO haiwezi kuisha mpaka kwanza wenyewe WACONGO watakapoungana na kuwa kitu KIMOJA na kuacha kuamini MATAIFA kutoka nje watamaliza hvyo VITA
hayo mataifa huko nje wanafuata RASILIMALI hata wale MUNOSCO wanajeshi wanasikitika MAJESHI kuondolewa

mana ZAMANI ilikuwa ukienda CONGO kulinda AMANI ukirudi basi mwanajeshi lazima ujenge bonge la JUMBA na ufungua biashara ndio mana kila MWANAJESHI alikiwa anatamani kwenda CONGO kulinda AMANI

sasa unadhani kwamantiki hii kuna anayetamani VITA iishe kutoka CONGO kwa mataifa yanayotoka nje kujidai kwemda kulinda AMANI CONGO
 
Divide and Rule

USA ndiye master mind wa hiyo game waache kucheza na Akili za watu

Period
 
Angalau Marekani wanaongeza ukweli kwa kiasi kikubwa juu y sakata la DRC.
Ana tuzuga tu 😀

Anajifanya kukemea ili asijulikane kuwa ni muhusika
Waweza kukuta hata tshekedi pia ana husika katika Upigaji so Wana jifanya Wana conflict ili kuzubaisha watu
 
View attachment 3515273
Haya yanajiri siku chache tu baada ya kusainiwa makubaliano ya amani yaliosimamiwa na Marekani.

Awali balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Mike Waltz, aliliambia Baraza la Usalama la Umoja huo kwamba, badala ya kupiga hatua kuelekea amani, Rwanda inaongoza eneo hilo kuelekea ukosefu wa utulivu na vita.

Pia amesema Marekani ina wasiwasi mkubwa na inazidi kukatishwa tamaa kwa kuzuka upya kwa ghasia Mashariki mwa Kongo.

Waltz anadai kuwa vikosi vya ulinzi vya Rwanda vimetoa msaada wa vifaa, mipangilio na mafunzo kwa M23 pamoja na kuisadia vitani. Hata hivyoRwanda imeendelea kukanusha kuliunga mkono kundi hilo la waasi.
Chanzo. DW Kiswahili
Rwanda sio Russia, Kama Russia, ilivyoivamia ukraine, Rwanda haina uwezo wa kiuchumi wa kuendesha Vita ndani ya DRC bila Msaada wa, kifedha, ki logistic, kutoka mataifa, makubwa, na, makampuni makubwa, wanapata pesa ya kuendesha Vita kutokana naauzo ya madini ya Congo, cobalt, platinum, uranium nk, Rwanda hawachakati hayo madini, wanayauza nje, hao wanaonunua ndio wanataka Vita uendelee, Trump anajua, Macron anajua, Africa inajua, Anayechezwa shele ni Tchisekedi Rais wa, Congo,
Endgame North and South Kivu zitamegwa, zitafanywa nchi huru!
Mbinu zilizotumika kuivunja Sudan, kwa story kuwa watu weusi/wakaristo wanateswa na Arabs, dawa wape weusi nchi yao! South Sudan ikazaliwa! Ndio huko kuna visima vikubwa vya mafuta! Jumuiya ya ki mataifa inajua kabisa, idadi ya weusi waliouliwa na weusi wenzao South Sudan ni maradufu ya waliouliwa, na Arabs,
Sasa Kongo, Watusi, wa Congo, banyamulenge wanateswa, na kubaguliwa na DRC, dawa, wape nchi yao! Is it a, coincidence kwamba manner yanayotekwa na m23, ni, Yale yenye madini kibao!
 
Ni bahati mbaya sana kwamba waafrika hawakosi kutafuta mchawi kwa ajili ya masaibu yao, iwe umaskini wao, iwe vita vya wenyewe kwa wenyewe, iwe utawala mbovu, iwe ufisadi, iwe matatizo ya kiuchumi na mengine mengi tu.

Na kadiri watakavyozidi kuendekeza hii tabia ndio bara hili litaendelea kuwa kichekesho cha dunia pamoja na rasilimali lukuki ilizonazo.

Tatizo pekee linalolisumbua bara hili ni kukosekana kwa uongozi na kwa bahati mbaya sana waafrika hawana kipawa au karama ya uongozi na hii pamoja na rasilimali lukuki bado Afrika inabaki kuwa ombaomba wa kudumu duniani huku watawala wakipigana kufa na kupona kung'ang'ania madarakani hata kwa umwagaji damu uliyokithiri.
 
Haya mambo yangeweza kuwa na hatma nzuri kama viongozi wa EAC wangekuwa sio wanafki na waroho.
 
usichojua ni kwamba
TRUMP kasaini DEAL na KAGAME deal kubwa la 40% kwa 60%

anachofanya TRUMP ni kutuchezea akili anadhami watu ni watoto wadogo
kile walichokubaliana na KAGAME anakifahamu

yake makaratasi waliotunesha makubaliano ya kumaliza vita ni ujinga
KAGAME si mpuuzi hvyo aingie makubaliano na MAREKANI kisha ageuke

muda si mrefu MAREKANI atajitia kwenda kulinda kile atakachokiita UKWIUKAJI WAMAKUBALIANO CONGO

kama kweli alikuwa na nia ya AMANI africa kwanza angewaita WASUDANI wakae chini wayamalize kati ya RSF na SAF kule ndiko kunahitaji msaada wa haraka zaidi wa AMANI

Vita CONGO haiwezi kuisha mpaka kwanza wenyewe WACONGO watakapoungana na kuwa kitu KIMOJA na kuacha kuamini MATAIFA kutoka nje watamaliza hvyo VITA
hayo mataifa huko nje wanafuata RASILIMALI hata wale MUNOSCO wanajeshi wanasikitika MAJESHI kuondolewa

mana ZAMANI ilikuwa ukienda CONGO kulinda AMANI ukirudi basi mwanajeshi lazima ujenge bonge la JUMBA na ufungua biashara ndio mana kila MWANAJESHI alikiwa anatamani kwenda CONGO kulinda AMANI

sasa unadhani kwamantiki hii kuna anayetamani VITA iishe kutoka CONGO kwa mataifa yanayotoka nje kujidai kwemda kulinda AMANI CONGO
Uko sahihi mkuu, hata huyo rais wao anafaidika na hii vita kuliko kungekuwa na amani. Sema kosa alilolifanya ni kwenda kuiomba marekani usaidizi, kwa akili yake akiendelea kuukuza huu mgogoro watamla kichwa. Ila pia kama viongozi wa ukanda huu na huu umoja wao hewa ungekuwa hauendekezi unafki huu mgogoro ungeshaisha ila kwa sababu kila kiongozi anapokea bahasha basi hakuna anaeongelea tatizo bali wanaongelea madini. Na hili la kuwagawanya viongozi wao wanalifanya makusudi. Rais badala atengeneze jeshi imara anawapa raia bunduki. Kama kuna kipindi 🇹🇿 inatakiwa kuwa macho ni sasa. Hizi bunduki baada ya vita kumalizika zitaenea mpaka huku.
 
Back
Top Bottom