Marekani: Trump atishia kufunga mitandao ya kijamii nchini Marekani

Marekani: Trump atishia kufunga mitandao ya kijamii nchini Marekani

KINACHONISHANGAZA WATU WENGI HUKU KWETU BADO WANADHANI Eti MATAIFA YA MAGHARIBI YAPO KTK DEMOKRASIA KWA ASILIMIA MIA !! HAYA SASA MNAONA ?
Demokrasia ni nini?
Trump anatukanwa kwenye mitandao ya kijamii kuliko anavyotukanwa Rais yeyote duniani and he's doing nothing to them.
.
Trump anasemwa vibaya mno na Dems na wala hajawapiga pin wasiendelee na campaigns zao wala chochote kwa kisingizio cha uchumi Hivi Tanzania nini kinaendelea?
.
Trump alitaka kuondolewa madarakani na Dems na alituliza mshono. hivi Tanzania unaweza kuthubutu kutaka kumuondoa Magu kwanza hiyo sheria ipo?
.
Kwenye air times za media Dems wanafanya watakavyo, hivi Tanzania wanaweza kuthubutu kufanya haya?
.
kumkosoa mfalme wa Tanzania ni jinai, kumkosoa Trump ni kama kunywa chai na mkate.
 
Amina.

Social media sio publishing media.

Kazi ya kuhariri maoni ya watu ni ujuha wa kiwango cha juu sana.
Likazi la JF hilo na walivyo wa ajabu hatuna hata uwezo wa ku-edit heading tu ahahaha.
.
Kuna mdau kasema JF ni sawa na ITV tu
 
Donald Trump anatarajia leo Alhamisi kutia saini kwenye agizo linalolenga mitandao ya kijamii, maafisa wa Ikulu ya White House wamesema, saa chahe baada ya rais huyo kutishia kudhibiti au kufunga makampuni ya mitandao yote ya kijamii, akiyatuhumu kujaribu kuzuia uhuru wa kujieleza.


Wawakilishi hao hawakutoa maelezo zaidi kuhusu yaliyomo kwenye agizo hilo la rais Trump. Haijulikani kwa wakati huu jinsi Donald Trump kupitisha tishio lake la kufunga kampuni binafsi, ikiwa ni pamoja na Mtandao wa Twitter.

Mzozo huo uliibuka Jumanne wakati Mtandao wa Twitter ulihakiki ukweli wa baadhi ya ujumbe wa Rais wa Marekani Donald Trump alioundika katika ukurasa wake. Ni mara ya kwanza mtandao huo ambao Trump anapendelea zaidi kuutumia unafanya hivyo.

Rais wa Marekani alighadhibishwa na jambo hilo na kushumu mtandao huo kwa kile alichokiita ‘kuingilia kati' uchaguzi wa urais wa mwezi Novemba pamoja na uhuru wa kujieleza.
Twitter ilichukua hatua hiyo ambayo haraka ilichochea mvutano kati yake na Trump, baada ya rais huyo wa Marekani kuandika Tweet mbili akidai kwamba mtindo wa kupiga kura kwa njia ya posta huwa una udanganyifu mwingi.

Ilichofanya Twitter ni kuweka kiungo kingine chini ya ujumbe wa Trump kinachosema "Pata taarifa za ukweli juu ya kura ya njia ya posta,” na baadae kiungo hicho kinampeleka mtumiaji kwenye makala ya habari inayompa taarifa za ukweli kuhusu suala hilo, na orodha ya maelezo yanayopinga madai ya Trump.

Trump mwenye wafuasi wapatao milioni 80 katika ukurasa wake wa Twitter, anasema anautumia mtandao huo wa kijamii kupinga kile anachodai kuwa ni taarifa za upendeleo zinazotolewa na vyombo vya habari.

Trump amekuwa akidai kwamba mtindo wa kupiga kura kwa njia ya posta, una viwango vya juu vya udanganyifu katika wakati ambapo majimbo mengi yanazingatia kuitumia njia hiyo ili kulinda afya ya raia dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19 wakati taifa hilo likiwa linaelekea katika uchaguzi wa rais wa mwezi Novemba
This idiot and loon duh,kweli tunatofautiana kufikiri.
 
Kumbe Trump angekuwa na id hapa JF ingekuwa kisanga
 
Trump ametunga sheria ya kuyabana zaidi makampuni ya mitandao ya kijamii baada ya kuyatuhumu kuingilia uhuru wa kujieleza.

Trump anayatuhumu hayo makampuni hasa twitter kuingilia uhuru wa kujieleza baada ya kuanza kuhariri mawazo na mada za watu wanazoweka kwenye hiyo mitandao

Kwa sheria ya sasa ya Marekani mitandao ya kijamii inalindwa na sheria kwamba haiwezi kushitakiwa kwa kuondoa mada za watu kwenye mitandao yao bila hata ruhusa ya alieweka hiyo mada na wala haitashitakiwa kwa mtu kuandika chochote kwenye hiyo mitandao

Trump anasema mitandao hiyo sasa imegeuka na kua wahariri wa mawazo ya watu na maoni ya watu kwenye mitandao yao hivyo kuondoa uhuru wa watu kutoa maoni wakati ilipaswa kua katikati(neutral ground).

Sheria mpya inasemekana itawapa watu uhuru wa kushitaki mtandao ambao utaondoa maoni yake bila ridhaa ya mwandishi. Na mwanasheria mkuu wa Marekani anasema sheria ya kuyalinda hayo makampuni ilidhamiria makampuni madogo yanayo chipukia ila sio haya ya sasa.
Trump to sign executive order about social media
Hiyo Executive Order aliyosign ni kama takataka tu, hakuna Mmarekani mwenye akili timamu ataitambua hiyo takataka, hakuna taasisi yoyote nchini Marekani itakayoitii hiyo takataka wala chombo chochote nchini Marekani kitakachoitekeleza hiyo amri takataka. Ni mtu mjinga tu na mwendawazimu anayeweza kuwaza kufanya kitendo kama hicho na hii imeonesha huyo Rais alivyo mtupu kichwani.
 
Hiyo Executive Order aliyosign ni kama takataka tu, hakuna Mmarekani mwenye akili timamu ataitambua hiyo takataka, hakuna taasisi yoyote nchini Marekani itakayoitii hiyo takataka wala chombo chochote nchini Marekani kitakachoitekeleza hiyo amri takataka. Ni mtu mjinga tu na mwendawazimu anayeweza kuwaza kufanya kitendo kama hicho na hii imeonesha huyo Rais alivyo mtupu kichwani.
Mkuu haya unaandika ukiwa unafikiria sawasawa ama uko maji? Kwamba rais aagize watu wasitekeleze?

Nipe mfano wa executive order ambayo rais aliwahi kusaini na hakuna mtu wala taasisi hata moja iliyokataa kutekeleza.

Mitandao ya kijamii iliyotangaza kwenda mahakamani kuipinga hiyo takataka ni wajinga? Si wangeacha takataka ijifie yenyewe huko?
 
Watu hawajui tu, hii hali ya watu kuhariri content ya post ya mtu inakers sana. Iliwahi kunitokea humu JF, nilipost comment baadaye nikaona kuna mtu ameni wuote nikipokwenda kusima nikahisi kuna mtu ame hack account yangu, kwani kile nilicho post nikskuta kimehaririwa na kwa jinsi aliyeni quote alivyinielewa mimi nikashindwa kujibu maana yupo sahihi ku quote vile kulingana junsi uhariti ulivyofanyika
 
Mkuu haya unaandika ukiwa unafikiria sawasawa ama uko maji? Kwamba rais aagize watu wasitekeleze?
Labda aliyekuwa maji ni huyo Rais wa Marekani kwani mamlaka hayo hana. Mitandao ya kijamii inalindwa na sheria zilizo juu ya uwezo wake. Rais wa Marekani si mungu-mtu kama huyu wa kwetu TZ na hayuko juu ya sheria. Alichofanya ni usanii tu.
 
Mleta mada umegeuza ukweli wa kilichotokea.

Actually alichokifanya Trump ni kutaka mitandao mikubwa iache tabia za kufuta maoni ya watu, kupiga ban watu hovyo na kujifanya kufact check watu.

Kasema hayo makampuni yamepewa leseni kama platforms ya watu kurusha maoni yao na siyo Editorial boards zenye opinion maalum, kasema kama yanaanza kuwa kama bodi za uhariri basi yakaombe leseni yatambulike hivyo.

Siku hizi Youtube imekuwa ikifanyia censoring maoni ya watu sana, kuwafungia kurusha content zao, Na hichi ndicho Trump amekizuia kupitia hiyo Executive order.

Muwe mnafuatilia vitu kiundani kabla ya kukurupuka
 
Back
Top Bottom