Marekani yaahidi dola milioni 10 kwa atakayetoa taarifa za wadukuzi 6 wa Urusi

Marekani yaahidi dola milioni 10 kwa atakayetoa taarifa za wadukuzi 6 wa Urusi

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Marekani imesema itatoa kiasi cha hadi dola milioni 10 kwa atakaetoa habari kuhusu watu 6 wanaotambulishwa kuwa ni maafisa wa ujasusi wa Jeshi la Urusi, wanaodaiwa kuwa waliendesha mashambulizi ya mtandaoni yaliyoathiri miundombinu muhimu ya Marekani.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imesema maafisa hao wanafanya kazi katika kitengo cha Idara Kuu ya Ujasusi ya Urusi kinachohusika na masuala ya mtandaoni (GRU) ambao walihusika katika shambulio la mwaka wa 2017 kwenye ngazi ya kimataifa, walisambaza kirusi kilichoharibu kompyuta za makampuni kadhaa ya kibinafsi ya Marekani, ikiwemo mfumo wa hospitali.

Shambulio hilo la mtandaoni maarufu “NotPetya” la 2017 lilidumaza sehemu ya miundombinu ya Ukraine na kuharibu kompyuta katika nchi kote ulimwenguni, ikiwemo Ufaransa, Ujerumani, Italia na Marekani, na kusababisha hasara inayokadiriwa kuwa ya mabilioni ya dola.

Pamoja na hivyo, Urusi ilikanusha kuhusika katika shambulio hilo.


Source: Reuters


==============================


U.S. Offers $10 Million Reward for Information on Russian Intelligence Officers -State Dept

WASHINGTON (Reuters) - The United States on Tuesday offered a reward of up to $10 million for information on six people it described as Russian military intelligence officers who had conducted cyber attacks affecting critical U.S. infrastructure.

The six officers work in a cyber-focused unit of Russia's Main Intelligence Directorate (GRU) and were involved in a 2017 global malware attack that infected the computers of several private U.S. entities, including a hospital system, the U.S. State Department said.

The 2017 "NotPetya" cyber attack crippled parts of Ukraine's infrastructure and damaged computers in countries across the globe including France, Germany, Italy and the United States, causing billions of dollars in estimated damage.


Russia denies any involvement in the incident.

A U.S. federal grand jury in 2020 indicted the six "Sandworm" unit officers on counts of conspiracy to conduct computer fraud and abuse, among other charges, the State Department said.

An award of up to $10 million would be rewarded for information leading to the "identification or location of any person who, while acting at the direction or under the control of a foreign government, participates in malicious cyber activities against U.S. critical infrastructure," it added.
 
Marekani imesema itatoa kiasi cha hadi dola milioni 10 kwa atakaetoa habari kuhusu watu 6 wanaotambulishwa kuwa ni maafisa wa ujasusi wa Jeshi la Urusi, wanaodaiwa kuwa waliendesha mashambulizi ya mtandaoni yaliyoathiri miundombinu muhimu ya Marekani...
Usaidie kuokoa mabilioni kwa kupewa Dola milion 10
 
Hivi Tanzania tumejipangaje kwenye cyber war?
Ipo usingizini ndo kwanza wataalamu wetu wa taifa wanajifunza mbinu za PUBG game,

Kufikia kwny cyber bado sana,kingine wanachoweza, unakumbuka (uchaguzi 2020)?

Wali freeze Internet kama sio ku shut down baasi ya sehemu,hicho ndo kinachowezekana kwa sasa.
 
Hivi Tanzania tumejipangaje kwenye cyber war?
Ni janga mkuu, kama uliifuatilia vizuri case iliyokuwa ikimkabiri Mbowe na wale makomandoo kwenye ushahidi wa kitehama upande wa jamhuri utaona jinsi tulivyo na rasilimali watu empty headed idarani.
Wapo raia wengi tu mtaani wenye utaalamu wanaachwa.
 
Back
Top Bottom