Marekani yaandaa na kutuma vikosi barani Asia kwa ajili ya vita na China

Marekani yaandaa na kutuma vikosi barani Asia kwa ajili ya vita na China

SaintErick

Member
Joined
Aug 7, 2013
Posts
90
Reaction score
53
Miaka michache iliyopita ilikuwa huwezi kuzungumzia vita kati ya Uchina na Marekani lakini hivi sasa tayari hilo halipo na kinachozungumzwa ni vita kati ya mataifa mawili makubwa zaidi duniani kiuchumi na kijeshi kwa maana ya Marekani na China.

Mapema mwezi huu (Oktoba) wanajeshi 864 wa Marekani walionekana wakiwa kwenye ndege kubwa za kivita za C-17 wakipelekwa kwa ajili ya mazoezi maalumu ya kupelekwa Asia tayari kwa vita. Hata hivyo, ni wanajeshi 492 tu ndio walifanikiwa kufikia lengo huku wengine washindwa kwa sababu mbalimbali.

Pentagon (Wizara ya Ulinzi ya Marekani) inaita vita hii kama Great Power War inaandaa wanajeshi kwaajili ya Vita na China ambavyo mpka sasa ni ngumu kuepuka. Wanaamini katika Jeshi lao la Marine kwa kua na utayari wa kufika mahali popote wakati wowote watakao hitajika. Jeshi lao majini (US NAVY) wana maisha yao katika bahari ya Atlantic na mpango mkakati wa mapigano huko uko kwenye DNA zao kwamba wamekua wakijifunza kila siku tangu wakati na baada ya vita vya pili vya dunia.

Lakini wanajeshi wa ardhini wanahitaji mafunzo zaidi kwani watakutana na jeshi la China ambalo liko na uelewa mpana zaidi wa Jiografia ya huko. Walipata somo wakati wakipigana na Talibani huko Afghanistan.

Sasa tofauti na Talibani, jeshi la China liko imara zaidi. Wana teknolojia ambayo sio sawa lakini inaikaribia kwa kiasi flani teknolojia ya Marekani ikiwa ni pamoja na vita vya kielektroniki (electronic warfare), Satelite na Drones. Hivyo jeshi la Marekani litakua likionekana kuanzia kwenye kujipanga (formation) hadi kwenye utekelezaji (excution) ya mission yao.

Kwa hio kwa sasa wanajeshi wa Marekani wanafanya mazoezi magumu na makali ili kua na uwezo wa kuishinda China katika vita hio ambayo kwa Marekani ni kama haizuiliki haijalishi nani atakuwa Rais baada ya uchaguzi wa November 5, 2024.

Xi Jin Ping anafukuza mwizi kimya kimya. Mshauri wake muhimu katika msawala mbalimbali kwa sasa amepewa mission ya Taiwan na jeshi la China limearifiwa kufanya mazoezi ili kuichukua Taiwan kwa nguvu mwaka 2027.

Hata hivyo kiasi cha makomandoo kutoka kikosi hatari zaidi cha SEAL NAVY kiko Taipei -Taiwan kwa ajili ya kulinda maeneo muhimu ya kimkakati kijeshi ikiwemo viwanja vya ndege na vituo vya mawasiliano.

NYT.png

Kwa hio ni wazi kwamba ikiwa China itaivamia Taiwan basi Marekani ni lazima kuingia vitani na China kwa sababu wakiacha basi China atapata nguvu kubwa Asia na mataifa mengi yatapiga goti kumtii na kuomba ushirika kwa hivyo ni lazima Marekani aipige China kuonyesha ubabe wake.

Source: New York Times
 
Umeandika utumbo
Wanajeshi mia nane waandaliwe kupambana na China?
Kakojoe endelea kulala.
Sisi ni mabingwa wa ku judge bila kuelewa. Nmeandika kuhusu Wanajeshi wa Ardhini wako katika Special Training wanafanya kwa awamu.

Nmeandika kua US MARINES wako tayari pamoja na US NAVY hasa Pacific Command wako tayari.

Asa kwako wewe shida iko wapi labda? Yaani unachukulia kwamba 894 tuu ndio Jeshi Kamili?

Soma elewa. Unaweza kupata nafasi ya kukosoa lakini pale ambapo una hoja yenye mashiko.
 
aaiseee ukisikia pumba miksa shudu ndo izi sasa
Naam, ungeleta hoja kinzani au ushahidi kinzani ingefaa sio kwangu tuu na wadau wengine wanaofuatilia. Hatuwezi kuandika habari au makala kwa kuku favour wewe hapana. Ila kilicho cha kweli basi kinaandikwa. Ni ruksa kua na nitazamo kinzani lakini kubeza hoja bila hoja hivyo ni vioja. Karibu kwa hoja
 
Sisi ni mabingwa wa ku judge bila kuelewa. Nmeandika kuhusu Wanajeshi wa Ardhini wako katika Special Training wanafanya kwa awamu.

Nmeandika kua US MARINES wako tayari pamoja na US NAVY hasa Pacific Command wako tayari.

Asa kwako wewe shida iko wapi labda? Yaani unachukulia kwamba 894 tuu ndio Jeshi Kamili?

Soma elewa. Unaweza kupata nafasi ya kukosoa lakini pale ambapo una hoja yenye mashiko.
Tatizo hadithi yako uliyotunga imekosa ufanisi
 
Trump alikua na changamoto kubwa na China. Trump hataburiki lakini kwa sababu ni swala la usalama wa faifa, yeyote atayeshinda ni ngumu kuzuia vita na China endapo mambo yataendelea hivi hivi.
Ki mtazamo, kwa sasa si afya kuanzisha vita na nchi ambayo haiko vitani, hasa china ambayo ina wanajeshi wengi na wako tayari kuifia nchi.

Kuhusu huyu mzee, uongozi wake uliopita aliweza kuunganisha dunia, na aliifanya dunia ikachangamka.

Kuna uwezekano akirudi tena madarakani anaweza kuutumia ushawishi wake mambo yakarudi vile vile, kwa kila mshirika kulinda maslai yake.​
 
Back
Top Bottom