Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Kwa ushamba wa nchi za kiafrika hawatendi mpaka kitu kiwe kimeanzia kwa wazungu na hawaachi kutenga mpaka wazungu waseme kina madhara.
Michezo ya kamari katika michezo imekuwepo kwa miaka mingi nchini Marekani na hata kutungiwa sheria na majimbo mbali mbali ili ifanyike bila matatizo.Hata hivyo kwa vile jambo hilo ni haramu hizo sheria hazijaweza kuzuia athari za ubaya wake.
Ili kufanyika kwa wepesi baadhi ya majimbo ya Marekani yametenga fungu maalum la kusuluhisha matatizo yatokanayo na ubashiri wa michezo. Hata hivyo majimbo hayo yamejikuta yakiishiwa na pesa na huku matatizo yakiongezeka.
Watu binafsi wamepata uraibu wa kubeti mpaka wanashindwa kufanya kazi za maana.Wengi wao wanaishi kwa wasi wasi na majonzi baada ya kujikuta wameshinda kidogo katika ubashiri na baada wakawa wakishindwa mfululuzo mpaka wakapoteza kila kitu na kushindwa kuanzisha mradi wowote wa kujipatia angalau chakula chao.
Unaweza ukajisomea zaidi hapo chini.