Marekani yafunga njia zote zilizokuwa zinatumiwa na Russia kwa kulipa madeni yake

Marekani yafunga njia zote zilizokuwa zinatumiwa na Russia kwa kulipa madeni yake

Annunaki

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2021
Posts
2,042
Reaction score
3,674
Baada ya Urusi kufungiwa njia zote ilizokuwa inatumia kulipa madeni yake na Marekani, wawekezaji watazidi kuikimbia Urusi.

Urusi kwa sasa ni kama kisiwa, imetengwa na Mataifa yote yenye uchumi mkubwa duniani, hata China yupo naye kinafiki tu.

Je, Moscow kujibu mapigo?
____________________

Marekani yafunga njia zote zilizokuwa zinatumiwa na Russia kwa kulipa madeni yake

Marekani imesema itafunga njia ya mwisho kwa Russia kulipa mabilioni ya dola ya deni lake kwa wawekezaji wa kimataifa leo Jumatano, na kufanya Russia kushindwa kulipa madeni yake kwa mara ya kwanza tangu wakati wa mapinduzi yajulikanayo kama ya Bolshevik ya mwaka wa 1917.

Wizara ya fedha ya Marekani imesema katika taarifa kwamba haina mpango wa kutoa leseni mpya ili kuiruhusu Russia kuendelea kuwalipa wakopeshaji wake kupitia benki za Marekani.

Tangu awamu ya kwanza ya vikwazo, wizara ya fedha ya Marekani ilizipa benki leseni ya kushughulikia malipo yoyote ya dhamana kutoka Russia. Muda wa fursa hiyo unakamilika saa sita usiku Mei 25.

Kumekuwa pia ishara kwamba utawala wa Biden hauna niya ya kuongeza muda huo wa kikomo.

Bila leseni ya kutumia benki za Marekani kulipa madeni yake, Russia haitakuwa na uwezo wa kulipa dhamana za wawekezaji wake wa kimataifa.

Kremlin imekuwa ikitumia Benki ya JPMorgan Chase na Citigroup kama njia ya kulipa madeni yake.

Chanzo RT, Reuters, Aljazeera, DW, CNN & BBC.
Screenshot_20220525-145154_1.jpg
Screenshot_20220525-150631_1.jpg
 
Dunia ya sasa tayari imeendelea sana. Si lazima u-trade na kila nchi ili uwe na mustakbali mzuri wa uchumi. Pia kuna namna nyingi za biashara kufanyika ktk hali yoyote ile (ukizingatia kuwa hata wao Russia wanategemewa na mataifa mengi kwa bidhaa zake)
 
Subir wajuzi wa Mambo
Hizo ni hasira za panzi furaha ya kunguru!! Wakati Marekani inaiwekea vikwazo Urusi vya kuzuiwa kufanya miamala kwa kutumia dola au euro, iliacha dirisha au kibali maalumu cha kufanya miamala kwa dola au euro kama inalipa madeni ya wafanya biashara walioko ndani ya Marekani.

Lengo la Marekani ni kwamba vikwazo visisababisha wamarekani wanaoidai urusi wakashindwa kulipwa pesa yao!! Pesa za urusi zilizokuwa kwenye mabenki ya nchi za magharibi zikazuiwa! Kwa hiyo lengo pia lilikuwa kumlazimisha urusi klutumia dola na euro zilizokuwa benki kuu nchini urusi kuzitumia kulipia madeni tu na wala si vinginevyo!! Marekani ilitegemea Urusi haitaweza kulipa madeni na kutangazwa kuwa imefilisika!

Kilichoishangaza Marekani ni kuwa Urusi iliendelea kulipa madeni bila shida na bila kukwama kwa kuwa bado inafanya biashara vizuri tu pamoja na vikwazo ilivyowekewa! Kwa hiyo marekani akaona atafute njia ya kuilazimisha urusi ishindwe kulipa madeni yake hata kama pesa inazo! Tatizo ni kwamba Marekani imeamua raia wake wanaoidai urusi WASILIPWE PESA ZAO!! Ni sawa na baba kumzuia mwanao asilipwe pesa yake anayomdai "adui yako". Hapo utakuwa unamuumiza mwanao, ndicho anachokifanya marekani.

Matokeo yake Urusi imefurahia sana na kusema itawalipa wadeni wake waliopo marekani kwa ruble! Hii itazidi kuipandisha chati pesa ya urusi ruble na ni sawa na marekani kujipiga risasi mwenyewe mguuni!!

Russia to pay foreign debt in rubles​

The announcement comes after the US blocked payments to American bondholders

Russia to pay foreign debt in rubles

© Getty Images.
Moscow plans to make foreign debt payments in rubles, Russian State Duma Speaker Vyacheslav Volodin said on Wednesday. This comes after the US blocked Russia from servicing its debt to American bondholders.
Volodin added that the country has all the necessary monetary resources for payments.

Tukisema marekani imechanganyikiwa muwe mnatuelewa!! Urusi imewachanganya hadi wanafanya maamuzi ya kujiumiza wenyewe!
 
Kwa mara nyingine,Wawekezaji kukosa dhamana ni pigo kubwa sana hilo kwa Urusi. Hadi RT wameripoti, ndo ujue hiki kikwazo ni kizito sana kwa Urusi.
Hujui unachokizungumza!! wawekezaji gani wamekosa dhamana? Kilichotokea ni kwamba wawekezaji raia wa marekani wanaoidai urusi ndio waliopata pigo maana hawataweza kulipwa pesa zao!! Ni pigo kwa raia wa marekani na si pigo kwa urusi!!

Hata hivyo Urusi haina hatia wala haiwezi kuaibika maana haijashindwa kulipa deni lake!! Ila kilichotokea ni kwamba baba mwenye nyumba huko marekani amezuia watoto wake wasilipwe pesa wanazoidai urusi!! Hiyo ni akili matope!! Na urusi imesema SAFI nitawalipa kwa pesa ya kirusi RUBLE!! Halafu kwa kejeli urusi inasema katika mazingira hayo naweza nisiwalipe kabisa na pesa hizo nikazitumia kwa matumizi ambayo yule kizee wa marekani (Rais Biden) hatapenda sana!! akimaanisha atatumia pesa hizo kwenye vita ya ukraine: Jisomee mwenyewe hapa:

Medvedev also said Russia was willing to pay the debt in rubles, but noted it might choose “not to pay at all and use the unspent money for precisely those purposes that those senile Americans will not like very much.”
 
EU na USA walimvizia Putin ajichanganye wammalize. Na yeye alivyo mjinga kweli kajichanganya.
Ukraine NI chambo tu.

Kwa aliyesikiliza hotuba ya rais wa European Commission Jana kwenye mkutano wa WEF atanielewa.
Watammalizaje sasa wakati wenyewe hawawezi kuthubutu kusogeza pua zao uwanja wa mapambano! Waliombwa waweke air free zone WAKAGWAYA! Wanaishia kupeleka silaha tu ambazo mara nyingi urusi huziharibu hata kabla hazijatumika!
 
Watammalizaje sasa wakati wenyewe hawawezi kuthubutu kusogeza pua zao uwanja wa mapambano! Waliombwa waweke air free zone WAKAGWAYA! Wanaishia kupeleka silaha tu ambazo mara nyingi urusi huziharibu hata kabla hazijatumika!
SASA MBONA VITA HAIISHI WEWE MRUSI WA BUGURUNI?

HEBU TUAMBIE MBONA VITA HAIISHI??
 
EU na USA walimvizia Putin ajichanganye wammalize. Na yeye alivyo mjinga kweli kajichanganya.
Ukraine NI chambo tu.

Kwa aliyesikiliza hotuba ya rais wa European Commission Jana kwenye mkutano wa WEF atanielewa.
Pro Putin hats kuangalia ule mkutano hawana habari ili wajifunze,wao wako busy na kusifia vile vifaru vinavyogeuzwa kirahisi kuwa scraper na Javeline
 
EU na USA walimvizia Putin ajichanganye wammalize. Na yeye alivyo mjinga kweli kajichanganya.
Ukraine NI chambo tu.

Kwa aliyesikiliza hotuba ya rais wa European Commission Jana kwenye mkutano wa WEF atanielewa.
Russia sio chato mkuu, usidhani Russia ina ina akina kibajaji, msukuma, magufuli nk nk!
 
Ukraine aliahidiwa kusaidiwa kijeshi akichokoza 'mzinga wa nyuki ' badala yake watu wanazunguka. mbuyu
Huoni huo ulikua mtego?
Anachofanyiwa Mrusi hukioni....?
Unadhani Ukraine kama hasaidiwi,angeendelea kupigana hadi sasa?
 
Back
Top Bottom