Marekani yaishutumu Urusi kutumia Chakula Kama silaha ya kivita Ukraine

Marekani yaishutumu Urusi kutumia Chakula Kama silaha ya kivita Ukraine

DeepPond

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2017
Posts
41,728
Reaction score
103,997
Maneno hayo ya secretary wa US- Antony blinken yanakuja baada ya Russia kushikilia moja kwa moja miji ya bandari na viwanda ya Odesa na mariupol.

Russia ilizuia usafirishaji wa bidhaa za Chakula na mazao kwa kile kilichodaiwa kua Chakula na mazao hayo yamekua yakienda kwenye maghala ya nchi za maadui wa russia.

Badala yake Russia ilisema kuanzia sasa Russia ndie atakua mgawaji na msambazaji mkuu wa Chakula hicho kwa nchi marafiki, na nchi maadui akiwemo Ukraine na baadhi ya nchi za nchi za ulaya Sasa watalazimika kununua Chakula hicho kutokea KREMLIN-MOSCOW kwa pesa cash ya Kirusi,yaani RUBO.

Secretary Antony blinken alisema "Russia WAMEAMUA kutumia Chakula Kama silaha ya kivita kwa kushikilia na kuzuia mamilioni ya Tani za ngano na mafuta ya alizeti zisisafirishwe kwa nchi zinazoitegemea Ukraine moja kwa moja kwa Chakula"

"Hii haikubaliki, na huu Ni uhalifu dhid ya maisha ya binadamu. Duniani nzima pamoja na umoja wa mataifa inapaswa kusimama na kulaani vitendo hivi maana vinakwenda kuumiza hata wasiohusika Moja kwa Moja"

"Kuna wazee,akina mama na watoto walioko Ukraine,ulaya na nchi tegemezi kwa chakula Cha ukraine wanakwenda kuathirika na baa la njaa kwa sababu Russia kaamua kushikilia Chakula Kama silaha yake ya kivita. Hii haikubaliki. Huu sio ubindamu. Huu Ni uhalifu wa kivita"

Chanzo: Al Jazeera english

Screenshot_20220521-103728.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
... inaonesha Ukraine ni nchi muhimu sana kwa maisha ya binadamu duniani; hadi Tanzania tumeathirika na upungufu mkubwa ngano kutoka Ukraine. Dikteta siku zake zinahesabika; hawezi kuichezea dunia kwa kiwango hiki!
 
Hakuna rais kilaza kama huyu kmmke, nchi kashaiharibu thn analeta ujinga wake
Je hakuliona hilo tokea mwanzo[emoji116][emoji116][emoji116]

Ukraine conflict can only be resolved through "diplomacy", Ukrainian President Volodymyr Zelenskyy says amid deadlock in negotiations between Kiev and Moscow https://t.co/NOkV2Ta6oi
 
... inaonesha Ukraine ni nchi muhimu sana kwa maisha ya binadamu duniani; hadi Tanzania tumeathirika na upungufu mkubwa ngano kutoka Ukraine. Dikteta siku zake zinahesabika; hawezi kuichezea dunia kwa kiwango hiki!
Dictecta walivamia Iraq, Libya, Syria wakaleta vitimbu Venezuera, wakaenda Iran wakaja mpk Sudan hapo.
 
... inaonesha Ukraine ni nchi muhimu sana kwa maisha ya binadamu duniani; hadi Tanzania tumeathirika na upungufu mkubwa ngano kutoka Ukraine. Dikteta siku zake zinahesabika; hawezi kuichezea dunia kwa kiwango hiki!
Nadhani kama sikosei Ukraine ndiyo inayoongoza duniani kwa uzalishaji wa ngano ikifuatiwa na Russia! Yaani hapo Russia kashika kwenye mpini.
 
Boss wa WFP (World food programe) amemuomba Putin Kama anakweli ana moyo wa kibinadamu, afungue bandari hizo.

Maana WFP inategemea kulisha watu mil.125 ambapo 50% ya chakula kinategemewa kutoka Ukraine.

Kitendo Cha Russia kuzuia chakula hicho itasababisha watu zaidi ya milioni 62.5 kufa kwa njaa.

Source: reuters
2022-05-21-12-33-42.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom