Marekani yajitoa rasmi Shirika la Afya Duniani WHO

Marekani yajitoa rasmi Shirika la Afya Duniani WHO

You spelt wrong! Global Fund inamilikiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) ikiwa imeasisiwa na mataifa ya G8 huku makao yake makuu ni jijini Geneva, Schweiz.
Nilikuwa na maana mfadhili Mkuu yaani anaechangia hela nyingi ni Nchi gani.
 
Halafu USA kujitoa WHO haimaanishi ndo haitajihusisha na WHO!

Hao wakuda siyo wanachama wa mahakama ya ICC lakini ndo wanatoa budget ya hiyo mahakama.

Bado wanahiitaji kuwa na ushawishi duniani kupitia mashirika kama haya.
 
Nilikuwa na maana mfadhili Mkuu yaani anaechangia hela nyingi ni Nchi gani.
Andorra, Australia, Austria, Azerbaijan, Bill & Melinda Gates, Canada, China, European Union, France, Germany, Italy, India, Japan, Netherlands, Sweden, South Africa, United Kingdom na United States.
 
Kwa watu wanaofuatilia mienendo ya siasa za dunia, maamuzi haya ya utawala wa Trump yanaiweka Marekani umwali na kuipunguzia uwezo au nguvu ya ushawishi duniani. Uamuzi huo ni msiba kwa ‘dunia ya Magharibi’ na kicheko kikubwa kwa China na Urusi. Rais Trump ataingia katika kitabu cha historia ya Marekani kama kiongozi aliyeidhoofisha Marekani na kuiondolea heshima ya kile kijulikanacho kama ‘kiongozi wa dunia huru’.
Exactly, ukitaka kuheshimika na majirani zako masikini ebu waruhusu wachote maji bure bomba la nje wapatie hata sukari kilo moja kwa mwezi ukichinja mbuzi wapelekee hata utumbo utaona watavyokuheshimu.

Trump has made America weak again, instead of great again.
 
Naona watu wana comment kiushabiki na wanasahau uhalisia kwamba wa kwanza kuathirika ni sisi huku nchi zisizo "jielewa" hasa viongozi wetu.

Nikifikiria magonjwa yenye udhamini wa taifa la USA, TB, HIV na malaria sioni hawa ndugu zetu watapata wapi msaada wa madawa haya kwa urahisi na wakati sahihi.

Nikikumbuka mwaka jana nina ndugu namuuguza ana TB kuna kipindi dawa ziliadimika dozi ikawa haipatikani kwa ukamilifu hii ni baada ya mdhamini kumaliza muda wake wa kutoa huduma.

Kiukweli kama haujui changamoto za haya magonjwa ya muda mrefu na upatikanaji wa dawa ukojekwa nchi zetu hizi utajua ni nini kinafata kwa ndugu zetu.

Serikali pekee sidhani kama wataweza kikombe hiki ukizingatia janga la corona ndio kwanza linaanza kuchanganya.

Sioni mchina kama ataweza kuingiza hizo $m400 WHO ili kuendeleza huu ufadhili, tuache masihara baniani mbaya ila kiatu chake dawa.
 
Dah!.. zile dola million 400 inazopokea WHO kutoka Marekani kila mwaka kuimarisha sekta ya afya huku dunia ya tatu ndio zimeyeyuka.

Kiburi cha tajiri hicho hamna namna tena.
 
Hizo ni mbinu za uchaguzi za kaburu Trump. Katika kupambana na Korona ameboronga (kama kawaida yake) na matokeo yake leo USA inaongoza dunia kwa vifo zaidi ya laki moja. Sasa anatafuta mchawi na mchawi ni WHO na China
 
Kwanini nchi za Afrika zisichukue hiyo nafasi ?

Hizi akili za utegemezi zitaisha lini ?
Tutachukua nafasi hiyo subiri kwanza tuingie kwenye uchumi wa kati halafu tuwe na uchumi mkubwa ili tuweze kuwa wenye kutoa mikopo na misaada kwa nchi nyingine.
 
Ndo mda wa kuacha kula tunda kimasihala kama huna hela maana soon ARV zitaanza kuuzwa na asilimia kubwa ya maskini wanaugua ukimwi
 
Waongo hao! USA ijitoe WHO? wapi na wapi, WHO ni Branch ya UNO,pande wa Afya, UNO Ni genge la nchi tajiri km USA kunyonya Maskini km Africa, wanapotezea/ zuga kisiasa kwa sababu Africa wanaipuuza WHO na kuisema ni genge la Wahuni! kwa WHO kuto ijali dawa ya Madagascar imewaumiza sana waafrica. USA ita boost WHO tu.
 
Weakness kuu ya Trump ni pale anaposhindwa kuinfluence jumuia ya kimataifa. Dunia yote inamwona kuwa ni clown tu, ndiyo maana kwenye mikutano yao wanamcheka. Kwa hiyo ndiyo maana amekuwa anatumia vitisho kwa vile hana uwezo kabisa wa kushawisi.

Kwa hili la WHO, alitakiwa ainfluence WHO kusudi interests za Marekani zipewe kipaumbele, lakini yeye akwa wa kulaumu na kutoa vitisho tu; hayo haletoi influnece hata siku moja
 
Back
Top Bottom