Marekani yakataza Afrika Kusini kuhudhuria mkutano wa G20

Marekani yakataza Afrika Kusini kuhudhuria mkutano wa G20

Yoyo Zhou

Senior Member
Joined
Jun 16, 2020
Posts
199
Reaction score
322
VCG31N2251737485.jpg
Waziri wa Fedha wa Afrika Kusini Enoch Godongwana hivi karibuni amethibitisha kuwa, yeye na Gavana wa Benki Kuu ya nchi hiyo Lesetja Kganyago hawajapata idhini ya Marekani ya kuingia kwenye nchi hiyo, ikimaanisha kwamba watashindwa kuhudhuria Mkutano wa Mawaziri wa Fedha na Wakuu wa Benki Kuu wa G20 utakaofanyika kuanzia tarehe 16 mwezi huu nchini Marekani.

Je, ni kwa sababu gani Marekani ilikataza Afrika Kusini kuhudhuria mkutano huo? Jibu ni sera ya ardhi. Kwa usahihi zaidi, ni sera ya ndani inayotekelezwa na serikali ya Afrika Kusini ili kurekebisha mgao usio sawa wa ardhi uliobaki kutokana na ubaguzi wa rangi. Marekani imeielezea sera hii kama “ubaguzi mpya wa rangi dhidi ya watu weupe”, na kutokana na sera hiyo, Marekani imekata kutoa misaada kwa Afrika Kusini, imemfukuza balozi wake, na kususia mkutano wa kilele wa G20 uliofanyika nchini Afrika Kusini.

Msemaji wa Hazina ya Afrika Kusini amethibitisha kwamba, licha ya Godongwana na Kganyago, maafisa wengine wa nchi hiyo pia hawataweza kuhudhuria mkutano huo. Hii inamaanisha kwamba Afrika Kusini ambayo ni nchi kubwa ya kiuchumi na kisiasa barani Afrika itakosa kabisa mkutano huo.

Tukio hili pia linaonesha kurudi nyuma kwa sera ya Marekani kuhusu mambo ya Afrika. Wakati ushawishi wake unapopungua barani Afrika, Marekani inajaribu kuadhibu nchi za Afrika ambazo hazitoi kipaumbele kwake. Ikiwa moja ya nchi kubwa zaidi ya kiuchumi na kisiasa barani Afrika, na mwakilishi muhimu wa Afrika katika masuala muhimu yakiwemo mabadiliko ya tabianchi, na mageuzi ya mfumo wa kifedha duniani, Afrika Kusini kushindwa kuhudhuria mkutano wa G20 ni hasara kubwa kwa Afrika.

G20, ikiwa ni moja ya majukwaa makuu ya usimamizi wa mambo ya uchumi duniani, sababu yake ya kuanzishwa na kuendelea hadi leo ni kwamba, baada ya msukosuko wa fedha wa mwaka 2008 duniani, jamii ya kimataifa iligundua kuwa hakuna nchi yoyote ambayo inaweza kushughulikia changamoto za kimataifa peke yake, na ushirikiano wa pande nyingi ni njia pekee. Lakini sasa, wakati nchi yenye nguvu inaweza kuwatenga wawakilishi wa taifa lingine huru kutokana na sera zake za ndani, asili ya pande nyingi ya jukwaa hili iko katika hatari ya kuachwa.

Bila shaka, Marekani haifikiri kuwa imefanya kosa lolote. Kwa mtazamo wake, majukwaa ya pande nyingi kamwe si majukwaa ya mashauriano yenye usawa, bali ni “klabu za kibinafsi” ambazo zinaweza kubadilishwa kama ipendavyo kulingana na maslahi yake ya kibinafsi. Bila shaka hii ni dharau kwa sheria za kimataifa na inastahili kufuatiliwa kwa makini na jamii ya kimataifa.
 
haya sasa tuone kama hao China, Russia, Brazili na Saudi Arabia watampigania mwafrika, afrika tunaongozwa na watu wajinga sana, unakwenda kujiingiza kwenye ugomvi na USA kisa arabs ambao hata hawaishi afrika? kwa nini siyo Egypt, uae au katar wasigombane na USA kuipigania palestina au irani? sasa kapigwa biti je, Saudi Arabia atasusia g20 kushinikiza afrika kusini aruhusiwe? sisi ni very low iq folks kwa kweli, afrika kusini yenyewe hata kwenye bric(s) haikuwa raihisi kuingizwa kwa maana original members ilikuwa ni bric tu na sasa afrika kusini nchi pekee ya afrika imeingizwa, wanaanza kuleta usenge kwa kugombana na super power.

sijui ni kwa nini tunashindwa ku-prioritize kwa kujua mambo yapi ni muhimu kwetu na yapi siyo muhimu sana, ningeelewa kama angegombana na USA kwa sababu ya kuipigania darfur sudani, kongo au central afrika republic, lkn unakwenda kugombana na Super power kisa palestina na iran from another continent, another culture, another race? sisi waafrika ni hadi huruma ...
 
😂😂😂😂 bongo bhana
 
Waendelee kususa tu, wakati CHINA anazidi kuzikumbatia nchi za Africa, Baadae yanakuja kushtuka yamepoteza fursa, yana aanza kutumia millitary intervention kama Kwa Maduro.

Anguko la USA lipo karibu.
China haina msaada wa maana kwa Afrika.
China yenyewe inainyenyekea USA, na kila leo viongozi wao wapo Europe na America kusaka wawekezaji.
Mauzo ya China nchini USA ni zaidi ya mauzo yote ya China kwa nchi za Afrika zikiwekwa pamoja. Lakini mauzo hayo hutokana na makampuni ya Marekani yaliyowekeza China. Bila Ulaya na America, uchumi wa China si chochote. Ndiyo maana China huwa haitaki kugombana na USA na Ulaya. Makampumi ya America na Ulaya yaliyopo China ndiyo yameibadilisha China kimapato. Kuna makampuni zaidi ya 70,000 ya Marekani yamewekeza China, na zaidi ya makampuni 40,000 ya nchi za Ulaya yapo China. Na haya ndiyo yameinua sana mauzo ya nje ya China.
 
Back
Top Bottom