Kada Mzalendo
Senior Member
- Oct 9, 2024
- 142
- 97
KATIKA kipindi ambacho CHADEMA imekuwa ikieneza propaganda potofu kuhusu hali ya demokrasia nchini Tanzania, ukweli umeonekana wazi kupitia matamshi ya Shirika la Changamoto za Milenia (MCC) la Marekani.
Viongozi wa juu wa CHADEMA, akiwemo Freeman Mbowe na Tundu Lissu, wamekuwa wakiandika barua za kuomba Tanzania inyimwe ufadhili kutoka kwa mashirika ya kimataifa, wakijaribu kuonyesha taswira mbaya ya Serikali ya Rais Samia.
Hata hivyo, juhudi hizo zimegonga mwamba, kwani Marekani, nchi ambayo mara nyingi CHADEMA hukimbilia kulalamika na kuwasilisha madai ya uongo kuhusu ukosefu wa demokrasia na haki za binadamu, sasa imeipongeza Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa mageuzi makubwa ya kiutendaji, yanayolenga kuimarisha demokrasia, utawala bora, na haki za binadamu.
Kupitia mkutano uliofanyika jijini Dodoma tarehe 17 Oktoba 2024, Mkurugenzi wa Sera na Tathmini wa MCC, Bw. Dan Barnes, ameweka wazi kuwa: "Katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Sita, wameridhishwa na hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Tanzania ambazo zimechangia kuongeza kasi ya maendeleo ya kiuchumi nchini."
Aidha Bunge la Marekani limeidhinisha kuendelea kuipatia Tanzania ufadhili wa miradi ya maendeleo, ishara kwamba jitihada za Rais Samia zimeleta matokeo chanya na kuimarisha msingi wa uchumi na demokrasia nchini.
Bw. Barnes alisisitiza kuwa: "Kutokana na kuridhishwa na mageuzi hayo, Bunge la Marekani limeridhia Tanzania kuendelea kunufaika na ufadhili wa Shirika la MCC."
Hali hii inakinzana moja kwa moja na madai ya uongo ambayo CHADEMA wamekuwa wakiyasambaza, wakijaribu kuonesha taswira potofu kuhusu Serikali ya Tanzania.
Lakini, kupitia mafanikio haya yaliyoidhinishwa na Marekani, Tanzania inathibitisha kuwa ni nchi yenye demokrasia imara na utawala bora, ikishinda propaganda za Chadema ambazo hazina msingi.
Rais Samia, kupitia falsafa yake ya 4Rs (Maridhiano, Ustahimilivu, Mageuzi, na Ujenzi Mpya), ameleta mshikamano na kuimarisha demokrasia, jambo linalokubalika kimataifa.