Marekani yamuua Mkuu wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Iran katika shambulio la roketi la uwanja wa ndege wa Baghdad

Marekani yamuua Mkuu wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Iran katika shambulio la roketi la uwanja wa ndege wa Baghdad

Kwa mara nyingine tena nikushukuru kwa maelezo yako hayo ndugu na pia kwa mara nyingine tena bado kuna 'Ukakasi' katika baadhi ya hoja zako.

Nitauelezea vyema 'Ukakasi' huo:

Niliuliza hapo awali kabisa kuwa;

Taifa lenye nuclear triad linaweza kushindwa kukabiliana na taifa ambalo ni non-nuclear?

Kwa sasa umelijibu swali hili kama ifuatavyo hapo chini;


Kwa jibu hilo ndugu, kwa kiasi fulani tumepaweka sawa pale mwanzoni kabisa nilipouliza hilo swali lenye wino mzito katika post #664.

Nilielezea katika bandiko langu lililopita angalau kidogo kuhusiana na mfumo wa Nuclear Triad. Maelezo ya kirefu zaidi nakumbuka nilishawahi kuyatoa humu humu jukwaani miaka ya nyuma.

Kwa taifa lililojizatiti kwa kufanya research & developments za kutosha kwa miaka zaidi ya 50 katika masuala haya ni factor kubwa sana ya uimara wake katika masuala ya kivita.
***

Twende sasa moja kwa moja katika 'Ukakasi':


"Real Battle" ni battle ya namna gani?

Nina-assume kuwa unamaanisha vita ya ana kwa ana kati ya mataifa hayo mawili. Yaani 'Direct Military Confrontation'.

Nilishazungumzia kuhusu hili hapo awali na niligusia vita ya silaha za kawaida kabla ya kuhusisha silaha za nyuklia na nilihoji kama ifuatavyo:


Katika masuala ya kivita ya kinyuklia (Nuclear Warfare), kila nchi yenye kumiliki silaha za nyuklia ina sera ama policies ilizojiwekea kuhusiana na matumizi ya silaha hizo. Hizi ni facts zilizopo!

Kuna mataifa ambayo yana policies zinazoainisha matumizi ya silaha za nyuklia dhidi ya mataifa yenye silaha hizo za nyuklia pekee. Yaani nchi husika itatekeleza shambulizi la kinyuklia endapo itakuwa imeshambuliwa na taifa jingine kwa silaha hizo za nyuklia na wala haitazitumia dhidi ya taifa lisilo na silaha hizo.

Lakini, Je unazifahamu vizuri policies za kinyuklia katika mataifa mbalimbali hususani Israel?

Kuna kitu kinaitwa Samson Option ambacho kimejaribu kuainisha kuhusu matumizi ya silaha za nyuklia za Israel na wakati ambapo matumizi yake yatakuwa ni ya lazima dhidi ya nchi adui. Kipo kitabu chenye maelezo juu ya hiki ninachokisema; The Samson Option cha mwaka 1991.

Jambo jingine, unaposema kuwa;


Kwamba vita ikitangazwa ndiyo nitajua Iran nuclear imetolea wapi? hiyo moja kwa moja ni kauli isiyokuwa supported na facts bali ni kama kauli ya kubashiri jambo (Guessing). Kwanini nisubiri vita itangazwe? Ni nini basi maana ya mjadala? Kwanini tusijikite katika taarifa na tafiti zenye kuakisi wakati uliopo ili kujengea hoja?

Unaweza kuwa na hoja nzuri lakini katika njia ya uwasilishaji wako ukaifanya ile hoja kwa namna moja ama nyingine kupoteza 'mashiko'.


Ni kweli kabisa na ninakubaliana na wewe kuwa, makombora hayo ni kwaajili ya kujihami.

IN FACT kila nchi yenye makombora ya nyuklia duniani ni kwaajili hiyo hiyo ya kujihami. Marekani, Urusi, China, Uingereza, Ufaransa n.k. wote hao makombora yao ni kwaajili ya kujihami yaani 'Deterrence'.


Kabla ya kwenda moja kwa moja katika 'Ushindi' wa vita, kuna suala la makabiliano au mapambano katika vita husika baina ya pande mbili hizo.

Katika vita ya kinyuklia, Ili kuweza "kukabiliana" na mashambulizi ya kinyuklia dhidi ya taifa jingine ni lazima taifa husika liwe na uwezo wa kujibu shambulizi/mashambulizi na hapo ndipo ule mfumo wa Nuclear Triad unapofanya majukumu yake.

Kitendo cha nchi kuweza kuyajibu mashambulizi ya kinyuklia kwa silaha hizo hizo za nyuklia ndiyo njia moja wapo ya "kukabiliana" na mashambulizi ya nyuklia kwa maana ya kuweza kupeleka adhari kwa adui aliyekushambulia na kuleta adhari upande wako. Kwahiyo suala si kushinda, bado suala ni "Kukabiliana" kwanza.


Umetaja Jericho III.

Makombora ya Balistiki uhusisha factors nyingi wakati wa kufanyiwa deployment na kisha kusafirishwa kuelekea katika shabaha iliyokusudiwa. Moja ya factors hizo ni 'payload delivery'.

Uzito wa payload ni kitu kinachoathiri mwendo wa makombora haya ya Balistiki na ndiyo maana kimahesabu suala hilo huzingatiwa ili kupata kipimo sahihi cha uwezo wa kombora husika kusafiri na kufanikiwa kuumaliza mwendo wake (Range).

Kwahiyo kutokana na vyanzo mbalimbali kumekuwa na utofauti wa vipimo kulingana na hizo factors mbalimbali. Kuhusu Jericho III na kwa kuzingatia hicho nilichokisema vipo vyanzo vinavyoweka kiwango chake cha juu zaidi cha mwisho wa masafa kuwa ni kilometa 11,500 na vipo vyanzo ambavyo vimeweka chini ya hapo.

Kwahiyo kwa kuzingatia factors hizo, mass of payload, technologies kama warhead miniaturization, pamoja na modifications mbalimbali za hata pia makombora mengineyo kama Jericho II, Beijing is within range. Pia bila kusahau miji mingine mashuhuri kama Shanghai, Shenzhen, Guangzhou n.k. yaweza kuwa targeted.


Sikatai kuhusu majaribio ya silaha kupata hitilafu ama ajali za hapa na pale kutokea katika sites za majaribio ya silaha maana matatizo haya huzikumba nchi zote zenye nguvu kijeshi katika nyakati tofauti tofauti.

ILA, hoja yako hii ina 'hang'. Kwamba Jericho 3 imefeli mara 3 nje ya 9? Lini? Kwa sababu zipi? Na ni kipi chanzo cha taarifa hiyo?


Sawa! Lakini hapa umezungumza kiwepesi sana.

China ni kubwa sana kijiografia ukilinganisha na Israel lakini hilo halimaanishi kuwa Israel haiwezi kukabiliana na mashambulizi kutoka China. Silaha za nyuklia na facilities zake haziwekwi maeneo ya wazi kama uonavyo supermarkets, matawi ya benki n.k. Nuclear facilities pamoja na mifumo mingineyo inayoiwakilisha Nuclear Triad kwa ujumla wake ni highly classified na yenye miundombinu imara sana ya kuilinda dhidi ya mashambulizi ya kinyuklia.

Hivyo basi, bado kunaiwezesha nchi husika kufanya 'second strike' yaani kujibu mashambulizi hata kama asilimia kubwa ya taifa hilo litakuwa limeadhiriwa na mashambulizi ya adui.

Nimalizie kwa kusema kuwa; udogo ama ukubwa wa nchi kijiografia si kigezo cha msingi cha kuweza kukitumia kama advantage ya kuhimili mashambulizi ya kinyuklia, bali ni uwezo wa nchi husika wa kuweza kujibu mashambulizi endapo itakaposhambuliwa isitoshe main purpose ya silaha za nyuklia ni kupiga shabaha 'strategic' zitakazoleta adhari kubwa zaidi kwa mustakabali wa nchi lengwa.

Ahsante!
Mkuu tumalize mjadala, nchi yenye nuclear triad itakuwa na ICBM,Submarines Launched Ballistic Missile na Strategic bombers, Mkuu Israel haina uwezo wa kukabiliana na nchi kama China au India, unadai kuwa ina Missile yenye kwenda 10000km lakini mpaka payload yake iwe chini kidogo ya 1000kg uwezo wa jericho 3 (range) ni 4800km to 6500km ikiwa full(1000kg), sasa nchi kama China wana Missile ya uwezo wa payload 2500 kg, hivi missile yenye payload ya 2500kg athari yake ni sawa na 1000kg? zote ni nuclear warhead.
Dont you see?

Hapo tayari unaona Dongfeng-41 ya china ina range kubwa(15000km) pia uwezo wa kupakia mzigo ni two times ya Jericho 3.

--Israel inaingia x450 ya China, hivi mfano Israel irushe jericho 3(1000 kg payload) zenye damage kwenye radius ya 20km maximum, jericho 3 ziwe 40 kwa wakati mmoja, na china irushe df-41(payload 2500kg) ziwe 40 pia damage radius ya 20km, zikitua zote same time nani kaumia? Dont you see Israel yooote imeishia? ndege zote,raia wote wameisha, damage kwa china itakuwa imepigwa 1 ya 450, ila Israel itakuwa imepigwa 1/1 yaani imeisha.

Israel licha ya wewe kudai ni Nuclear triad mimi nina mashaka na hilo, ili uwe nuclear triad lazima uwe na ICBM, Submarine LBM, na Strategic Bomber LBM, sasa Hebu nambie Israel ina bomber gani?

Tunajua USA ina hizo B-2 na B-52 na n.k ,
UK ina strategic bombers kama Victor
Germany, France, Russia wote hao wana strategic bombers zao
China ina strategic bomber zake (Xian-H6 series) na moja ya strategic bomber latest ni Xian-H6N, Xian H-6N nia air launched ballistic missile hio, inaenda thousand miles pasipo kuwa refueled, nikisema ni air launched ballistic missile ni kwamba inaweza kurusha ballistic missile tokea angani baada ya hapo missile huwa inajilipua kama rocket na kuendelea na safari yake, sasa kama ina range kubwa hivyo unadhani Missile itashindwa kumalizia umbali uliobakia?

Ukiachilia hio Xian-H6N China ina Bomber moja deadly saaana inaitwa H-20, kama B-2 ya USA ambapo ni stealth hio, hio ndio latest kabisa.
Ukiachilia hio H-20 wana bomber ingine ni stealth hio inaitwa JH-XX pia ni stealth na ni hatari sana, hazina utofauti kwenye size na ile B-2 ya USA.

1981 Israel iliishambulia Iraq kwenye nuclear reactors zao na umbali ulikuwa ni 1100km haikutumika bomber yeyote, na hata ndege zilizoenda hazikuwa refuelled.

Sasa mkuu nikuulizze kwa nini Israel haina bomber? na hapo ndio napata mashaka kama kweli ni nuclear triad, Israel itatumia hizo F-15 na F-16 kushambulia adui zake within a range ya eneo hilo(middle east) japo F-15 itabeba nuclear bomb lakini haliwezi kuwa na damage kama litakalo bebwa na strategic bomber kama H-20 pia F-16,F15 even F-35 bado hazina uwezo wa range sawa na strategic bomber kama hizo za China.

Na hapo umejua kabisa Israel vita na China itapigwa asubuhi saa 2 na nusu, Israel imejipanga kupambana na majirani zake middle east, ila China inaeza pambana na nchi sehemu yeyote ile Asia na World wide kwa ujumla.

Sasa endelea kujua jericho 3 kama inaenda 6500km eti ndio inaeza pambana na nchi kama China au India, never happen.
 
Mimi nachojua waarabu walipigwa....kuhusu walipigwaje hayo jua wewe..
Kwani intellijensia sio uimara wa kijeshi??
Unaweza toa sababu kwanini Israel walishinda mpaka kesho kutwa lakini hata kama wangekuwa wanapigania uhai wao kama uwezo (inteligency,military,tactics) wasingekuwa navyo hata kama morali ya kupigania existence ingekuwa kubwa kiasi gani WASINGESHINDA...
Lakini ukweli ni kuwa saivi Israel kawapiga gep wengi Kwenye technology ya kivita saiv...so the next Israeli war will be total obliteration of enemies
Wangewamaliza Hizbullah Kwanza Wakati wa Vita Ya 2006

Waache wajiingize Vitani Waone Kitakacho Wkut
Kila leo wanawatwanga HAMAS Na HAMAS Wanapambana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Eti eeeh [emoji23][emoji23][emoji23][emoji2][emoji2][emoji2]
Marekani na Trump wanajua wanachokifanya.Wamemuua makusudi huyo kamanda wa Iran ili Iran itaharuki na kujiingiza kwenye vita kichwakichwa.Kumbuka marekani anadai Iran wanakaribia kutengeneza silaha za nuklia.Marekani inajua kuishambulia Iran bila sababu yeyote ingelaaniwa na dunia yote na Trump angepata upinzani hata ndani ya marekani toka kwa Democratic. Sasa hivi Iran akishambulia maslahi yeyote ya marekani mashariki ya kati au popote duniani ,marekani itapata sababu ya kuishambulia Iran pamoja na vinu vyake Vya nyuklia pasipo kupingwa na dunia:

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe kweli akili zako mchichapori..
Sababu ya kupigana haikufanyi ushinde vita ila uwezo wa kupigana ndo unakufanya ushinde..
Unaponiambia israel alishinda kwasababu anapigania existence unaongea pumba
Israel alipigana nao waarabu directly yaani Egypt ,jordan,Syria lakini kwa Iran na Iraq...iran hakupigana directly na wasaidizi wa Iran
Kwanza sadam alikuwa punga unaweza ukapewa silaha ukashindwa kuzitumia
Halafu kuhusu military technology Israel is by far the best as of now.. Hata hayo mabeutiful equipments ambayo bwana trump anajisifia kuspend 2tril dollars over. .mengi yametengenezwa na kampuni za Israel..hizo new drones za mmarekani zimetengenezwa israel hata zile drones ambazo Iran alitumia kumpiga Iraq alipewa na muisrael(yes Iran alisaidiwa na Israel) sasa hawa jamaa usiwachukulie simpo na sio kila technologia waliyo nayo wameiuza ...siku kikinuka ndo utashangaa mtume na maria Iran hionekani Kwenye ramani
Kama walichemka kwa Hizbullah 2006 unahisi wataweza nn hawa wapuuzi ?!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa inasubiria nini kuifuta kwenye ramani ya dunia. Israel inajilinda aingie basi mle aifute aone moto wake maamaee. Siyo mchezo pale kumbuka yakobo baba wa Israel alipigana na malaika wa Mungu sasa waje hawa Shia
Leta facts Israel inaweza sio porojo sijui Yakobo kafanyaje, hivi unajua Tel Aviv ni gays paradise? Unajua kuwa sheria ya Israel inaruhusu askari wao kuwa gay?inaruhusu wanawake kusagana, wanaume kubetuana, sheria hadi wana jeshi wanaruhusiwa, sasa bakia na story zako hizo wakati wenzio wanafanya ushetani.
 
Leta facts Israel inaweza sio porojo sijui Yakobo kafanyaje, hivi unajua Tel Aviv ni gays paradise? Unajua kuwa sheria ya Israel inaruhusu askari wao kuwa gay?inaruhusu wanawake kusagana, wanaume kubetuana, sheria hadi wana jeshi wanaruhusiwa, sasa bakia na story zako hizo wakati wenzio wanafanya ushetani.
GOD BLESS ISRAEL, AMERICA, THE KURDS AND SAUDI ROYAL FAMILY.

Kamoooonnn sema AMEN!😆😆😆
 
Huyu alikuwa ndio mchora ramani wa Iran kwa shughuli zao zote nje ya Iran, kuanzia kushambuliwa kwa Visima vya Mafuta vya Saudi Arabia mpaka kuteka meli na bila kusahau kashikashi la Ubalozi wa Marekani. Tungoje tuone Iran atafanya nini,sasa hivi kichapo kwake kipo wazi wazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Samahani, kwani mkuu jamaa kafia nchini kwake iran ama? Na je ni helikopta au droni?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili jamaa kweli lilikuwa linachochea vurugu kwenye ubalozi wa Marekani nchini Iraq.Mbona baada ya kuwawa vurugu zimekoma ?
 
Back
Top Bottom