Marekani yapanga kufanya mashambulizi dhidi ya magaidi wa JINM nchini Mali

Marekani yapanga kufanya mashambulizi dhidi ya magaidi wa JINM nchini Mali

Richard

Platinum Member
Joined
Oct 23, 2006
Posts
16,890
Reaction score
26,440
1784923785252.png

Bwana Sebastian Gorku akizungumza na waandishi wa habari.

Raisi Donald Trump amekuwa akishauriana na watu mbalimbali ndani ya utawalal wake nai pia kufikiria ombi la nchi ya Mali kusaidiwa kuondoa magaidi wa JNIM ambao wana mahusiano na kundi la Al Qaeda.

JINM ambao kirefu chake ni Jama’at Nusrat al-Islam wal-Muslimin ni kundi la magaidi ambalo limekuwa likisumbua katika eneo kubwa linoizunguka nchi hiyo kubwa katika bara la Afrika kwa eneo na moja ya nchi wazalishaji wakubwa wa dhahabu.

Kundi hilo limekuwa likikiri kufanya mashambulizi hatari ambayo yamesababisha vifo vya watu wengi na pia kuteka watu tangu kianzishwe mwaka 2017. Mashambulzi ya kikundi hichi yamevuka mpaka hadi kuingia nchi jirani ya Niger.

Kwa mujibu wa gazeti la Washington Post ambalo lina mahusiano na watu walo kwenye utawala wa Trump, Marekani ipo katika kupanga namna ya kufanya mashambulizi hayo ili kuzuia mashambulizi ya kikundi cha JINM dhidi ya ndege zake za kijajusi (spy planes) ambazo hufanya doria za mara kwa mara katika eneo zima la jangwa la sahara.

Hata hivyo bado haifahamiki ni kwa namna gani Marekani itafanya mashambulzi hayo kutokana na kuwepo nchini humo kwa vikosi vya African Corps (zamani Wagner Group) ambavyo vilikwenda nchini humo baada ya kuombwa msaada kwa Russia kusaidia kukabuliana na kikundi hicho.

Waziri wa mambo ya kigeni bwana Abdoulaye Diop Alhamisi ilopita amenukuliwa akisema kwamba nchi yoyote yaweza kushirikiana na Mali bila kuingilia uhuru wake. Bwana Diop alitaka misingi mitatu linapokuja suala la kushirikiana na Mali kwamba kwanza ni lazima kuheshimu uhuru wa wake, pili ni kuheshimu maamuzi yoyote ytayotolewa na mali kwa kuzingatia kuwa ni nchi huru na la tatu ni kwamba lazima maslahi ya watu wa mali yazingatiwe.

Nae kaimu msaidizi wa raisi wa Mali bwana Sebastian Gorka na mkurugenzi mwandamizi wa anesimamia kitengo cha kukabiliana na ugaidi katika baraza la usalama la Mali, amesema ushirikiano wa kiusalama na Russia haujawa imara zaidi ya kuzalisha magaidi kwa wingi.

Ikitumia mwanya huo wa kauli kama hizo zinotoka kwa viongozi wa Mali, marekani imesema Mali na nchi nzingine za Niger na Burkina Faso zahitaji kuwekeza zaidi katika vifaa vya kisasa pamoja na huduma zake katika kukabiliana na magaidi hao. Pia Marekani imeshauri nchi za NATO kusaidia juhudi za kukabiliana na magaidi hao na pia nchi ya Mali.

Vyanzo: Washington Post.

Pia msaada wa mwandishi wa habari Mohamed Ag Hamalek kutoka Bamako, Mali.
 
Hao Mali kama wanadai ni nchi huru sasa si wapambane na hao magaidi wao wanashindwa nini hadi waombe msaada kwa maadui wa Urusi ambao ndio walikuwa wanawaamini hapo mwanzo.
 
Hao hao magaidi wote Huwa wana wekwa na USA Russia Israel saudia and the likes halafu baadae wanajifanya kuja kuwasuluhisha ili wawapige Hela
 
Hao hao magaidi wote Huwa wana wekwa na USA Russia Israel saudia and the likes halafu baadae wanajifanya kuja kuwasuluhisha ili wawapige Hela
Ufaransa ndiye mlezi.
 
Fungueni mbongo km jamaa mmoja alivyoeleza hapo... Magaidi wanatengenezwa hao na Westerners, Mrussi anatafutiwa sabbu,
 
Back
Top Bottom