FRANC THE GREAT
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 5,500
- 8,060
Ndege maalumu za mashambulizi mazito (B-1B Lancer Bombers) zawasili nchini Saudi Arabia
Jeshi la anga la nchini Marekani limetuma idadi isiyojulikana ya ndege maalumu za mashambulizi mazito na zenye kasi kubwa (Supersonic Bombers) aina ya Rockwell B-1 Lancer ama B-1B maarufu na ikijulikana kwa kifupi kama Bone au B-One katika Uwanja wa Ndege wa Kijeshi wa 'Prince Sultan' huko Saudi Arabia, ambapo inaonekana ni mara ya kwanza kwa aina hiyo ya ndege kupelekwa nchini humo au ndege zinginezo za mashambulizi mazito kwenye nchi hiyo.
Hii inakuja wiki mbili baada ya Pentagon kutangaza mipango ya kuanzisha operesheni maalumu katika msingi mkuu wa kujizatiti kijeshi nchini Saudi Arabia kufuatia shambulio kubwa la makombora ya 'Cruise' pamoja na ndege zisizo na rubani, lililohusishwa na taifa la Iran, kwenye vituo viwili vya mafuta nchini humo. mwezi uliopita.
Kabla ya hapo, tayari vikosi vya jeshi la ndege aina ya F-22 Raptor na mitambo ya makombora ya Patriot ya Marekani tayari imewasili katika Kambi ya Kijeshi ya 'Prince Sultan' kama sehemu ya mpango huo mpana.
Picha fupi za 'Video' kutoka Jeshi la Anga la Marekani (U.S. Air Forces Central Command) zilionesha kutua kwa ndege ya B-1B katika uwanja wa ndege wa 'Prince Sultan' mnamo Oktoba 25, 2019, lakini haikueleza idadi kamili ya ndege hizo zilizoelekea Saudia na zitakuwepo huko kwa muda gani.
Ujumbe katika mtandao wa kijamii pia ulisema kwamba ndege hizo zilipaa moja kwa moja kutoka Kiwanja cha Ndege cha Ellsworth huko Dakota Kusini, ikionesha kuwa ndege hizo ni kutoka kitengo chake cha 28 cha mashambulizi maarufu kama 28th Bomb Wing. Video nyingineyo ilionesha ndege maalumu zisizopungua nne (4) za B-1B zikiiacha ardhi ya Ellsworth na kuelekea Saudia.
"B-1B ni ndege maalumu ya masafa marefu na ya kasi kubwa pamoja na mashambulizi mazito (Long-Range Strategic Bomber) inayoweza kupiga adui yoyote katika eneo lolote duniani," Tweets zilisema kama ifuatavyo;
Ndege hizo zenye uwezo wa kubeba mzigo mkubwa zaidi wa silaha za aina zote mbili (zinazoongozwa ama Guided na pia zisizoongozwa au Unguided). Ndege hizi kutoka Kampuni ya Boeing zenye injini nne kila moja za General Electric F101-GE-102 zinaweza kusafiri kwa kasi ya Kilometa takribani 1,448 kwa saa.
B-1 ni uti wa mgongo wa Jeshi la Anga la Marekani kwa muda mrefu, ndege inayoweza kutuma kwa haraka na kwa idadi kubwa ya silaha kwa ufanisi mkubwa mahali popote ulimwenguni.
Military.com | The Drive