Mlango-Bahari wa Hormuz umefungwa kutokana na vita kati ya Marekani, Israel na Iran, na jamii ya kimataifa imeanza kutafuta njia mbadala baharini. Hivi karibuni Marekani inafanya mawasiliano ya kidiplomasia na Eritrea, ambayo ni nchi muhimu ya njia za meli za Bahari Nyekundu.
Kabla ya hapo, mwaka 2021, serikali ya Joe Biden ya Marekani iliweka vikwazo vikali dhidi ya Eritrea, ikidai “Eritrea imekiuka haki za binadamu” na “kuchochea vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini Ethiopia”. Kwenye ripoti za vyombo vya habari vya nchi za Magharibi, Eritrea inaitwa “Korea Kaskazini ya Afrika,” ikikosolewa vikali kwa mfumo wake wa kipekee wa uandikishaji wa wanajeshi na mazingira yake ya kisiasa yaliyofungwa mlango.
Lakini sasa, wakati Mlango-Bahari wa Hormuz unafungwa kutokana na vita kati ya Marekani, Israel na Iran, Marekani imebadilisha kabisa sera yake kuhusu Eritrea. Mshauri mkuu wa masuala ya Afrika wa Rais wa Marekani Massad Boulos amesema Marekani inapanga kuondoa baadhi ya vikwazo dhidi ya Eritrea, ili kupata faida katika eneo la Bahari Nyekundu. Maafisa wa Marekani wanaona kwamba, licha ya “rekodi mbaya ya haki za binadamu”, Eritrea ina umuhimu wa kimkakati kwa Marekani katika eneo la Bahari Nyekundu.
Mabadiliko haya makubwa ya sera ya Marekani kuhusu Eritrea yanafichua mantiki ya msingi ya sera ya Marekani kuhusu Afrika. Marekani inatumia vipimo viwili kwa nchi za Afrika: nchi zinazofuata matakwa yake na zenye manufaa, zinatendewa kama wageni wa heshima, hata kama zina “rekodi mbaya ya haki za binadamu”, na nchi zinazokataa kuitii zinakabiliwa na “fimbo kubwa”.
Afrika Kusini ni mfano mwingine. Kama nchi iliyoendelea zaidi kiviwanda barani Afrika, imeilaani Marekani kutokana na sera yake ya mageuzi ya ardhi yenye lengo la kurekebisha dhuluma kutokana na ukoloni na ubaguzi wa rangi. Marekani inadai “sera hiyo inadharau wakulima weupe”, na kusimamisha misaada ya mradi ya kuzuia UKIMWI, kumfukuza balozi wa Afrika Kusini nchini Marekani, na hata kukataza Afrika Kusini kuhudhuria mkutano wa G20 uliofanyika hivi karibuni huko Miami. Lakini ukweli ni kwamba Marekani imefanya hivyo kwa kuwa Afrika Kusini inaiunga mkono Palestina katika jukwaa la kimataifa, ilikataa kuilaani Russia, na kutetea utaratibu wa BRICS.