Marekani yatumia vipimo tofauti katika suala la dawa za kusisimua misuli

Marekani yatumia vipimo tofauti katika suala la dawa za kusisimua misuli

Yoyo Zhou

Senior Member
Joined
Jun 16, 2020
Posts
126
Reaction score
215
无标题.jpg
Michezo ya 33 ya Olimpiki ya Majira ya joto inafanyika huko Paris, nchini Ufaransa. Mwanariadha wa Marekani Erriyon Knighton alikimbia kwa sekunde 19.99 katika mchuano wa mita 200 kwa wanaume uliofanyika hivi majuzi, na kusaidia timu ya Marekani kuingia nusu fainali kwa nafasi ya kwanza. Hata hivyo, mchezo huu umesababisha utata mkubwa, na vyombo vingi vya habari vinauita "mchezo usio wa haki zaidi".

Miezi minne iliyopita, Knighton alithibitishwa kutumia dawa ya kusisimua misuli aina ya Trenbolone, na kwa mujibu wa kanuni za Shirika la Kupambana na Matumizi ya Dawa za Kusisimua Misuli Duniani (WADA), Knighton anapaswa kuzuiwa kushiriki kwenye michezo kwa zaidi ya miaka minne. Hata hivyo, Shirika la Kupambana na Matumizi ya Dawa za Kusisimua Misuli la Marekani (USADA) lilitangaza kabla ya Michezo ya Olimpiki ya Paris kwamba, sababu ya dawa hiyo kukutwa kwenye mwili wa Knighton ni kwamba alikula nyama iliyochafuliwa, hivyo hatapewa adhabu yoyote.

Lakini vyombo vya habari bado vina mashaka mengi. Trenbolone ni dawa maarufu ya kusisimua misuli michezoni, na inaweza kuongeza kwa haraka nguvu ya mlipuko ya wanariadha na kuwasaidia kupata matokeo mazuri. Zaidi ya hayo, USADA lilifanya uchunguzi zaidi ya siku 60 baada ya tukio hilo, na kisha kuumaliza kwa haraka, na ushahidi uliotolewa haukuwa wa kutosha.

Lakini kwa wanariadha wa China, Marekani imetumia kipimo kingine kikali. Kabla ya kufunguliwa kwa Michezo ya Olimpiki ya Paris, Marekani ghafla ilikashifu WADA kwa "kupendelea" timu ya kuogelea ya China, na hata kudai kuwakamata wanariadha wa China.

Je, wanariadha wa kuogelea wa China walifanya nini? Katika Mashindano ya Kitaifa ya Kuogelea ya China yaliyofanyika mwaka 2021, wanariadha 23 walituhumiwa kutumia Trimetazidine, ambayo ni moja ya dawa za kusisimua misuli. Lakini baada ya kufanya uchunguzi kwa makini, iligundulika kuwa tukio hilo lilitokana na uchafuzi wa jiko kwenye hoteli, ambapo wanariadha hao walikuwa wanakaa. Licha ya wanariadha hao, mamia ya wanariadha wengine walioshiriki kwenye mashindano hayo hawakugunduliwa dawa hiyo mwilini. Aidha, kipimo cha dawa hiyo kwa wanariadha hao 23 ni kidogo sana, na hakitoshi kuathiri haki ya michezo. Hatimaye ilihitimishwa kuwa, tukio hilo lilisababishwa na uchafuzi wa chakula, na wanariadha waliohusika hawatawajibishwa, na WADA ilikubali matokeo ya uchunguzi wa kesi hiyo.

Lakini Marekani ilikataa uamuzi huo. Kabla ya kufunguliwa kwa Michezo ya Olimpiki ya Paris, Marekani ilitaka WADA kufanya kipimo kikali dhidi ya timu ya China. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirika la Kimataifa la Kuogelea, waogeleaji wote 31 wa China wanaoshiriki kwenye Michezo ya Olimpiki ya Paris walifanywa ukaguzi wa dawa za kusisimua misuli kwa mara 256, wakati huohuo, wanariadha wa Marekani walipimwa mara 50 tu.

Marekani ndiyo mzalishaji na muuzaji mkubwa zaidi wa dawa za kusisimua misuli duniani, na katika ligi za kitaaluma za michezo nchini humo, kuna matukio mengi ya kutumia dawa hizo zinazopigwa marufuku. Ripoti za vyombo vya habari zimeeleza kuwa, idadi kubwa ya wanariadha nchini Marekani wanatumia kinyemela dawa hizo, au kwa kisingizo cha magonjwa mbalimbali. Wakati huohuo, China ina msimamo thabiti dhidi ya dawa za kusisimua misuli. Kwa mujibu wa data iliyotolewa Julai na WADA, ikilinganishwa na nchi nyingine duniani, China imefanya zaidi ukaguzi, lakini kiwango cha kugundulika kwa matumizi ya dawa hizo ni cha chini zaidi. Hata ikilinganishwa na Marekani, China imefanya ukaguzi mara tatu zaidi ya Marekani, lakini kesi za kugundua matumizi ya dawa hizo ni moja ya sita ya Marekani.
 
Back
Top Bottom