Marekani yawaonya raia wake kutembelea Tanzania kuepuka kuambukizwa COVID-19

Basi tueleze hali kuwa mbaya ilisababishwa na nini, "KUPIMA"?
Tulipoacha kupima corona ikaisha?

Inafaa pia ueleze, kwa nini ilibidi 'watu wazikwe usiku' na ilikuaje "wakaacha kuanguka barabarani" unaelezaje mabadiliko hayo - SALA/Maombi?

Mimi naweza kukueleza kwamba, inawezekana 'virus' yule tuliyeanza naye aliendelea kujigeuza na kupungukiwa nguvu kadri alivyozidi kupitia kwenye miili ya watu, ndio maana nikakueleza huko mwanzo uwezekano wa kuwepo 'strain variance' kutoka kwa yule tuliyeanza naye. Hili sio jambo geni kwa virus na hata bacteria. Lililo muhimu hapa ni wataalam wetu kufanya utafiti kujua ukweli ni upi.

Inawezekana pia 'herd' immunity katika jamii iliongezeka, au bahati yetu ya kuwa na jua wakati wote ndio ikawa neeme kwetu.

Inawezekana ikawa ni mchanganyiko wa hayo yote na mengine ambayo bado hatuyajui, mpaka utafiti ufanyike.

Lakini kwa uhakika kabisa, COVID-19 haikuisha Tanzania kwa vile tu tuliacha kupima, au kwa vile sisi Mungu ni ndugu yetu, tulipomwendea akaona atuepushe na janga.
Pia nina uhakika kabisa, kwamba Tanzania haina tofauti yoyote na nchi nyingine za kiafrika, kama Kenya, katika maambukizi na vifo vya watu vilivyotokea hadi sasa.
Kutopima ni ushamba tu wa kuhadaa watu(watalii wengi waje hapa? Matokeo yake yamekuwa kinyume chake. Watu wenye uelewa hawahadaiwi na ujinga wa viongozi tulionao.
 
takwimu zao ambazo umesema ziko karibu na uhalisia ila huku afrika mwenyewe unasema kuwa takwimu zilizopo ziko mbali kabisa na uhalisia
Unaona ulivyopotosha kwa huu mstari maneno niliyoandika, ambayo umeyawekea mkazo hapo juu? Ungekuwa muungwana ungeniomba radhi.
 
Unaona ulivyopotosha kwa huu mstari maneno niliyoandika, ambayo umeyawekea mkazo hapo juu? Ungekuwa muungwana ungeniomba radhi.
Hebu eleza basi nimepotosha vp?hebu fafanua ulichokieleza pengine hatujaelewana.
 
Hebu eleza basi nimepotosha vp?hebu fafanua ulichokieleza pengine hatujaelewana.
Basi bwana. Maneno niliyoandika yapo hapo juu, na ili yaonekane umeyakoleza kabisa katika bandiko lako #408. Haya ndiyo maneno uliyoyafanyia mhtasari na kuyafanya yawe na maana hii:
" umeweza kujua hali yake kutokana na takwimu zao ambazo umesema ziko karibu na uhalisia ila huku afrika mwenyewe unasema kuwa takwimu zilizopo ziko mbali kabisa na uhalisia kama ulivyofafanua"
Hii ndio tafsiri ya maneno niliyoandika?
 
Basi bwana. Maneno niliyoandika yapo hapo juu, na ili yaonekane umeyakoleza kabisa katika bandiko lako #408. Haya ndiyo maneno uliyoyafanyia mhtasari na kuyafanya yawe na maana hii:
Ndio maana nikasema pengine mie sijakuelewa ndio nikakuomba ufafanue ulichoeleza.
 
Kwa hiyo .... Humu ndani mnatuambia tuanze kuvaa masks?? Dah... Is this real? Ee Mwenyezi Mungu Tunaomba Uturehemu.
 
Kwa hiyo .... Humu ndani mnatuambia tuanze kuvaa masks?? Dah... Is this real? Ee Mwenyezi Mungu Tunaomba Uturehemu.
Ni wapi nilipoandika watu wavae mask mkuu wangu 'Msweet'?

Hivi andiko hilo kweli linaelekeza mahali popote watu waanze kuvaa mask?

Lakini napenda ujue pia kwamba, pamoja na COVID-19 kuwa hafifu huku Africa, Tanzania ikiwemo, bado kuna watu wanaokufa kutokana na virus huyo, hata kama kasi ya kuambukiza na kufa sio kali kama ile inayoshuhudia huko Ulaya na Marekani.

Kwa hiyo, njia yoyote ya kujikinga nayo ni jambo jema.
 
Corona ipo Tanzania watu wanakufa lakini kwa kuwa Serikali ilipiga marufuku kuongelea corona inabidi Hosptal waache kusema ukweli
Mimi naishi pembezoni mwa barabara kuu. Yani zamani ambulance ingepita mara moja. Siku hizi ni kila baada ya lisaa ambulance inapita ni vingora vya hatari. Ndugu zetu wanaofanya kwenye idara za afya nao wanatusihi sana tuwemakini. Corona inapukutisha watu wengi sanaa
 
Nani kwao ambao wana Covid zaidi,Tanzania au Marekani,nadhani Tanzania ndio watoe onyo kwa raia wake kutokwenda Marekani kutokana na Marekani kuwa ndio inaongoza kwa maambukizi ya Covid 19,Marekani huu ni WIVU TU
 
Sisi labda tuwaambukize umasikini, Ila wao ndiyo watatuambukiza Corona...




Cc: mahondaw
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…