Marekani yawaonya raia wake kutembelea Tanzania kuepuka kuambukizwa COVID-19

Marekani yawaonya raia wake kutembelea Tanzania kuepuka kuambukizwa COVID-19

Kuna mtu mkubwa sana ana mashavu mapana na kipara, kafa kwa korona, na yule mzee mwenye blich la kikongo mdogo wake kafa kwa korona na korona ipo vyombo vya usalama vinajuwa na records wanazo.
Unamaanisha corona ileile iliyoua mamilion ya watu kula brazil,na hospitali zao kuletewa na wagonjwa baada ya kupuuza masharti?

Ubazungumzia corona ileile iliyoua watu wengi marekani na italia?

👉Kama ubazungumzia hiyo corona niliyoiongelea hapo juu, kwa ubora wa huruma zetu hosipitalini na technology yetu, sidhani Kama watz tungekuwepo leo.

👉Marekani bado wanatoa takwimu za kila siku?
 
Serekali ilitangaza kuwa imeishinda Corona na miezi inayofuata ikachukua hela za kupambana na corona.Hii inathibitisha ya kwamba ni serekali isiyoaminika na inayodanganya watu wake juu ya mambo ya Corona.Ni serekali ya kihuni ambayo hata yenyewe haijiamini.Halafu nimekuambia ya kwamba mimi kutokuwa na Corona na kutokujikinga dhidi ya Corona haihalalishi wala haithibitishi kuwa Tanzania hakuna Corona.Ulielewa kuhusu hili?
Ww kutojikinga na corona, kutokumfahamu mwenye corona na wewe kutokuwa na corona inathibitisha nini?

Suala la kuchukua fedha za kupambana na corona haimaanishi kuna corona. Unafahamu maana ya mapambano dhidi ya corona nchini? Sisi kutokuwa na corona inamaanisha hakuna namna corona inatuathiri?

Sitakuhoji namna unavyoichukulia serikali yako mpaka utoe madai uliyotoa maana huipendi.
 
Umeuliza swali nililokwishalijibu: "kwa nini afrika COVID-19 imekuwa hafifu..., soma tena niliyoandika hapo juu.

"Umetumia nini kujua hali ya COVID-19 huku Africa ni hafifu tofauti na huko kwengine"?
Hata kama Afrika wanakabiliwa na tatizo la kutokuwa na uwezo wa kupima watu wengi na kujua walioathirika; na pengine hata kutokuwa na uwezo wa kuwa na hakika vifo vinavyosababishwa na COVID-19, moja kwa moja au kuchangia vifo hivyo, ingetokea ikawa na nguvu kama ilivyoonyesha Ulaya na Marekani (kwa kuangalia takwimu), Afrika ingeshuhudia kasi hiyo, leo hii hata baadhi ya serikali zisingekuwepo.
Uwezo wa hospitali zetu ungeelemewa kabisa na watu wangekuwa wanapukutika tu hadi mitaani.

Sasa sijui kama utaelewa nilichoandika hapa.
Nilichokuelewa ni kwamba kutokana na takwimu za covid 19 huko Ulaya na Marekani ndio zilizokufanya uone kuwa covid 19 kwa hizo sehemu ilikuwa ina nguvu sana.

Ndivyo ama sivyo?
 
Nilichokuelewa ni kwamba kutokana na takwimu za covid 19 huko Ulaya na Marekani ndio zilizokufanya uone kuwa covid 19 kwa hizo sehemu ilikuwa ina nguvu sana.

Ndivyo ama sivyo?
Ni sehemu ya jibu.
Hatujazungumzia 'strain variance' ya virus huyo aliyeko huko na huku, na tofauti nyingi nyingine za mazingira zilizopo kati ya huku na kule.
Lakini kinachotakiwa kwa sasa ni wanasayansi wetu kutafiti kwa nini hasa pamekuwepo na maambukizi hafifu Afrika ukilinganisha na Ulaya na Marekani. Lakini kwa bahati mbaya sana, wanasayansi wetu wengi wanawaza tu kwenda kwenye siasa, kwa kuteuliwa au kugombea ubunge. That is our tragedy.
 
Ww kutojikinga na corona, kutokumfahamu mwenye corona na wewe kutokuwa na corona inathibitisha nini?

Suala la kuchukua fedha za kupambana na corona haimaanishi kuna corona. Unafahamu maana ya mapambano dhidi ya corona nchini? Sisi kutokuwa na corona inamaanisha hakuna namna corona inatuathiri?

Sitakuhoji namna unavyoichukulia serikali yako mpaka utoe madai uliyotoa maana huipendi.

Mimi kutojikinga na corona, kutokumfahamu mwenye corona na kutokuwa na corona inathibitisha kuwa sina Corona na pia inathibitisha kuwa sijali kuhusu Corona, lakini hili halithibitishi wala halihalalishi na pia halitoi ticket kuwa Tanzania hakuna Corona.Inawezekana wapi mimi mtu mmoja nitumike kama ticket ya kuthibitisha kuwa Tanzania nzima haina Corona,tokea lini anachofanya mtu mmoja kitumike kama ticket ya kuthibitisha kuwa Tanzania nzima hakuna Corona!

Kama ulisikiliza ule mkutano wa EU uliokuwa unajadili juu ya Tanzania yule mwenyekiti wake aliweka wazi kabisa kuwa waliipa Tanzania hela kwa ajili ya kupambana na Corona kama vile kufanya vipimo na kutoa takwimu za maabukizi mapya ya kila siku.Unaposema kuwa fedha zilitolewa kwa ajili ya kupambana na athari za Corona hayo ni maneno yako wala siyo masharti ya fedha za EU.Masharti ya fedha za EU yalikuwa ni pamoja na kutii matakwa ya WHO ya kupambana na Corona kama vile kufanya mass testing na kutoa matokeo pamoja na takwimu kila siku na haya siyo maneno yangu bali ni maneno ya yule Rais wa EU.
 
Ni sehemu ya jibu.
Hatujazungumzia 'strain variance' ya virus huyo aliyeko huko na huku, na tofauti nyingi nyingine za mazingira zilizopo kati ya huku na kule.
Ikiwa huko ulaya na marekani umeweza kujua kuwa corona ni kali kwa kutizama takwimu sasa huku africa pia umejua hali ya corona kwa kutizama takwimu?
 
Ikiwa huko ulaya na marekani umeweza kujua kuwa corona ni kali kwa kutizama takwimu sasa huku africa pia umejua hali ya corona kwa kutizama takwimu?
Sielewi mantiki ya swali lako, lakini ngoja nijaribu kulijibu niwezavyo:

Takwimu ni sehemu muhimu sana kuonyesha tofauti kati ya sehemu mbili au zaidi. Huwezi kutofautisha bila kuwa na takwimu sahihi; na huwezi kueleza sababu za tofauti ya vitu hivyo bila kuwa na takwimu sahihi.

Huwezi kutazamahali tu na kutoa hitimisho bila kuwa na takwimu sahihi.

Ulaya na Marekani wana uwezo mpana wa kufanya vipimo sahihi kwa watu wengi kuliko ilivyo Afrika, kwa hiyo takwimu za huko zipo karibu zaidi na hali halisi ya maambukizi na vifo kuliko ilivyo Afrika. Kama Kenya, kwa mfano, wameweza kupima takribani watu 200,000 tokea ugonjwa uingie nchini humo, hii ni tofauti kabisa na takwimu za jimbo moja la Marekani lenye idadi sawa na Kenya, ambao wanaweza kuwa wamepima zaidi ya mara tano ya watu waliopimwa Kenya. Jimbo hilo hilo linaweza kuwa limeweka kumbukumbu ya waliokufa wengi zaidi ya hao waliokufa Kenya. Hiyo ni kazi ya takwimu. Kuweza kubainisha kwa uhakika zaidi maenezi na athari zinazotokana na maambukizi.

Afrika, kuna nchi zilizojitahidi kukusanya takwimu, kama Kenya, Uganda na Rwanda. Sisi hapa tumeghairi, na kujitangaza tumeishinda COVID-19, kwa njia zipi? Kwa sala! Hali yetu haina tofauti sana na hao wenzetu walioweka juhudi ya kukusanya takwimu na kuweka njia za kuzuia maenezi. Hapa ndipo tunapoweza kusema Afrika hatujaathirika kama walivyoathirika Ulaya, na sababu za tofauti hiyo hatuzijui!

Kwa kutizama takwimu za nchi zilizojitahidi kukusanya takwimu hizo, na hata kutoona maambukizi mengi mitaani zote zinachangia kufikia hitimisho kwamba COVID-19 Afrika ni hafifu kuliko huko kwingine. Hatujui sababu ya uhafifu huo ni nini.

"...sasa huku Afrika pia umejua hali ya corona kwa kutazama takwimu"?
Hili swali lako ni kama lina kejeli, lakini sijui wewe unataka tujue kwa kutumia njia gani, ikiwa ni pamoja na kujua kama virus aliyeko kule na huku ni huyo huyo na kama mashambulizi yake yana nguvu sawasawa, kazi ambayo inahitaji kufanyiwa utafiti.
 
Wewe unaeleza utofauti wa hali ya corona kwa huko Marekani na huku afrika ila kwa huko Marekani umeweza kujua hali yake kutokana na takwimu zao ambazo umesema ziko karibu na uhalisia ila huku afrika mwenyewe unasema kuwa takwimu zilizopo ziko mbali kabisa na uhalisia kama ulivyofafanua,sasa kwa muktadha huo utawezaje kulinganisha hizi sehemu mbili na useme afrika corona sio kali wakati upimaji wenyewe ndio huo na nchi zengine hawapimi kabisa kama Tanzania?

Kuna watu humu wanasema Tanzania inaongoza kwa maambukizi kushinda afrika mashariki yote,wengine wanasema hakuna corona,wengine wasema corona ipo na watu wanakufa sana tu ila kimya kimya. Wote hao wanaongea hivyo hawana takwimu,sasa na wewe unasema kuwa afrika corona si kali kuliko Ulaya na Marekani.
 
zilizopo ziko mbali kabisa na uhalisia
Nionyeshe nilipoandika hayo maneno niliyoku'quote' hapo juu.
sasa kwa muktadha huo utawezaje kulinganisha hizi sehemu mbili na useme afrika corona sio kali wakati upimaji wenyewe ndio huo na nchi zengine hawapimi kabisa kama Tanzania?
Husomi ukaelewa kilichoandikwa, kama sio kutaka kupindisha kilichoandikwa maksudi. Nimeweka mifano kadhaa kueleza tofauti zilizopo, wewe unaweka kivyako.

Basi sasa na wewe eleza unayojua.
Kuna watu humu wanasema Tanzania inaongoza kwa maambukizi kushinda afrika mashariki yote,wengine wanasema hakuna corona,wengine wasema corona ipo na watu wanakufa sana tu ila kimya kimya. Wote hao wanaongea hivyo hawana takwimu,sasa na wewe unasema kuwa afrika corona si kali kuliko Ulaya na Marekani.
Wewe unasemaje? Hakuna corona?
Wote hao wanaongea hivyo hawana takwimu
Wewe unazo? Kutokana na maandishi yako ni kama huamini takwimu!
sasa na wewe unasema kuwa afrika corona si kali kuliko Ulaya na Marekani.
Bila ya shaka yoyote. Kilichobaki tu ni kufahamu sababu ni zipi.
 
Nionyeshe nilipoandika hayo maneno niliyoku'quote' hapo juu.

Husomi ukaelewa kilichoandikwa, kama sio kutaka kupindisha kilichoandikwa maksudi. Nimeweka mifano kadhaa kueleza tofauti zilizopo, wewe unaweka kivyako.

Basi sasa na wewe eleza unayojua.

Wewe unasemaje? Hakuna corona?

Wewe unazo? Kutokana na maandishi yako ni kama huamini takwimu!

Bila ya shaka yoyote. Kilichobaki tu ni kufahamu sababu ni zipi.

"Ulaya na Marekani wana uwezo mpana wa kufanya vipimo sahihi kwa watu wengi kuliko ilivyo Afrika, kwa hiyo takwimu za huko zipo karibu zaidi na hali halisi ya maambukizi na vifo kuliko ilivyo Afrika. Kama Kenya, kwa mfano, wameweza kupima takribani watu 200,000 tokea ugonjwa uingie nchini humo, hii ni tofauti kabisa na takwimu za jimbo moja la Marekani lenye idadi sawa na Kenya, ambao wanaweza kuwa wamepima zaidi ya mara tano ya watu waliopimwa Kenya. Jimbo hilo hilo linaweza kuwa limeweka kumbukumbu ya waliokufa wengi zaidi ya hao waliokufa Kenya. Hiyo ni kazi ya takwimu. Kuweza kubainisha kwa uhakika zaidi maenezi na athari zinazotokana na maambukizi.

Maelezo yako hayo yanaonesha kuwa takwimu za covid19 kwa huku afrika ziko mbali na uhalisia kwa maana kama uwezo wetu wa kupima watu corona ni mdogo sana yani kwamba hadi sasa tumepima watu wachache sana kuliko idadi ya watu waliyopo. Kwa muktadha huo hauoni kuwa kutumia hizo takwimu kusema kwamba corona si kali sana afrika kuliko Marekani na Ulaya inakuwa si sahihi?

Yani tuposhindwa kuelewana ni pale ambapo wewe ushapitisha kuwa corona ya afrika si kali sana ila mie bado nataka kujua kuwa wewe umewezaje kujua corona kwa afrika si kali?

Mwanzoni huko nilikwambia kuwa wkt Tanzania tunapima na kutoa takwimu ilikuwa inaonekana hali ni mbaya hadi kukawa na clip zile watu wakizikwa usiku mara sijui wengine wakianguka barabarani. Kuna watu walikimbilia mikoani huko kwa sababu Dar hali ni mbaya zaidi kukatokea hadi uvumi wa hospitali kuelemewa na wagonjwa wa corona.
 
Maelezo yako hayo yanaonesha kuwa takwimu za covid19 kwa huku afrika ziko mbali na uhalisia kwa maana kama uwezo wetu wa kupima watu corona ni mdogo sana yani kwamba hadi sasa tumepima watu wachache sana kuliko idadi ya watu waliyopo. Kwa muktadha huo hauoni kuwa kutumia hizo takwimu kusema kwamba corona si kali sana afrika kuliko Marekani na Ulaya inakuwa si sahihi?
Kama huna uelewa wa maambukizi ya milipuko utasema hivyo; lakini hata kuchukua sampuli katika jamii na kuzifanya 'representative' ya jumuia pia huna ufahamu nao? Hii ni sehemu muhimu ya takwimu na kujua kasi ya maambukizi. Wewe yote haya huoni kuwa ni 'takwimu' inayotoa taarifa muhimu kuhusu maambukizi na vifo?

Nimejaribu kufikiri ni nini hasa unachotaka nikiandike, pengine ndipo utakaporidhika.
Watu wakidondoka kwa maelfu mitaani ndio utajua kwamba COVID-19 ipo? Kwa vile tu watu hawaanguki na kufa na wewe kuwashuhudia, basi kwako hakuna COVID-19 Afrika?
Yani tuposhindwa kuelewana ni pale ambapo wewe ushapitisha kuwa corona ya afrika si kali sana ila mie bado nataka kujua kuwa wewe umewezaje kujua corona kwa afrika si kali?
Hata 'intuition' tu ingekuonyesha kwamba kama maambukizi yaliyotokea Ulaya na Marekani yangetokea hapa Afrika, licha ya takwimu zilizopo zinazokusanywa na nchi zinazofanya hivyo hata mtu asiyekuwa na uelewa angejua kwamba corona ni ugonjwa hatari sana.

Hebu nieleze, ni nchi ngapi Afrika zimejaza wagonjwa mahospitalini na kushindwa kuhimili jinsi ya kuwahudumia, hasa kutokana na ufinyu wa uwezo na uchache wa hospitali hizo? Hilo peke yake haliwezi kukuonyesha kwamba Corona yetu ni tofauti na ile inayoshambulia Ulaya na Marekani? Tusilojua ni nini tofauti hiyo, au kinachosababisha iwe hivyo!

Ngoja nimalize kwa kukueleza hili: Hata 'sampuli' zinazochukuliwa na nchi zinazopima, zinatoa picha juu ya "kasi ya maambukizi katika jamii".
Kasi hiyo inaweza kulinganishwa na kasi iliyopo katika nchi za Ulaya na Marekani. Hiyo inakupa picha ya tofauti kati ya sehemu hizi mbili. Hali ni hiyo hiyo hata katika vifo vinavyotokea.

Chukulia kwa mfano: katika watu elfu moja Africa, ni watu wangapi wameshambuliwa na COVID-19 katika muda maalum. Huwezi kulinganisha tarakimu hizo na zile zinazopatikana Ulaya na Marekani kwa kiasi hicho hicho cha watu katika jamii?
Ni hivyo hivyo hata katika vifo.

Lakini wewe hujaeleza chochote, unauliza maswali tu! Tueleze na wewe tuelewe unachojua.
 
Back
Top Bottom