Marekani yawatahadharisha raia wake wanaotaka kuitembelea Tanzania dhidi ya Ugaidi na uhalifu

America watu wanauwawa kuliko nchi yoyote east Africa halafu leo wanaleta kidomodomo.
Naona Tanzania,Kenya na Uganda zimewekwa level moja,halafu eti Rwanda hakuna hatari yoyote.
Mwenye akili ataona shida ilipo.

Hata hapa nchini ccm inafanya mikutano bila usumbufu wowote, unashangaa US kufumbia macho huko kwao? Hii ndio karma, ukiwafanyia wengine wasichotaka, usilie siku na ww ukifanyiwa hayo hayo.
 
 
Kwani wamekutangazia wewe au wamewatahadharisha wamarekani.
Mimi nakushangaa sana mtu kama wewe unaona sawa Nchi kutangazwa vibaya lakini unatetea wanaokutangaza. Wakati mwingine toeni vichwa katika ma buts ya viongozi wenu
 
 
Hizo sifa sasa
Wamezidi nao hao USA
Sisi raia mbona hatuoni hivyo vitu,kwanini walishindwa kutoa hilo tamko enzi za kikwete Makanisa,misikiti na watalii walikuwa wanalipuliwa?
Waseme agenda yao wazi tuwahue.!
 
aisee hii ni hatari sasa.

kutokana na utoto wa viongozi wetu, my gut feeling is US wanaweza kuwa wameamua kuwa funders wa ugaidi kama njia ya kuuondoa uongozi huu uliojaa utoto.

Watanzania tusisubiri tufikishwe huko.... hii shughuli ya kuweka uongozi makini nchini mwetu ni jukumu letu sisi wenyewe!
 
Mimi nakushangaa sana mtu kama wewe unaona sawa Nchi kutangazwa vibaya lakini unatetea wanaokutangaza. Wakati mwingine toeni vichwa katika ma buts ya viongozi wenu
Nani anasababisha tutangazwe vibaya halafu ni wapi nimeona sawa kutangazwa vibaya, usiendeshwe na mihemuko.
 
KIkwete alipoulizwa swali kuhusu ushoga na mwandishi wa habari alitoa jibu simple na lililoeleweka "Jamiiyetu watanzania haijawa tayari kuruhusu jambo hilola ushoga". Baada ya jibu hilo hakukuwa na mjadala wowote kwa kuwa alishaufunga kiakili
 
Sijui huduma gani muhimu Bashite anayompa Jiwe hadi ikafikia hatua hii
 
Reactions: Qwy
Hakuna issue yeyote zaid ya ushoga tu na hapo tumewashika pabaya america

Ww ndio unaona hilo tu, sisi wapinzani tunaona mengi. Ngoja tuone mwisho wa hii chokochoko. Hapa ndio watawala watafahamu siasa za kunyanyasa wengine zina gharama zake.
 
Beberu time [emoji1] [emoji1]
 

Matumizi ya nguvu hayatatatua tatizo, tenda haki kwa watu wote nchi itakuwa na amani na utulivu.
 

Ni kweli, lakini hata hapa sio peponi. Tunaona ukatili wa wazi dhidi ya wapinzani wakati wa uchaguzi. Watu wameachwa na vilema kisa hawaikubali ccm. Basi acha hao wazungu waje watoe msaada kwa wale wanaoumizwa kisa hawaikubali ccm.
 
 
Ni kweli, lakini hata hapa sio peponi. Tunaona ukatili wa wazi dhidi ya wapinzani wakati wa uchaguzi. Watu wameachwa na vilema kisa hawaikubali ccm. Basi acha hao wazungu waje watoe msaada kwa wale wanaoumizwa kisa hawaikubali ccm.
Ninachokisema mimi sitetei haya matukio lakini usisahau Marekani kila mwezi watu weusi wanauawa na polisi hivyo wanatakiwa kuwa wa mwisho kutusema sisi lakini wenzetu wengine humu kwasababu wanaichukia serikali basi wanaona ni sawa tu tutangazwe vibaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…