Marekani yawatahadharisha raia wake wanaotaka kuitembelea Tanzania dhidi ya Ugaidi na uhalifu

sidhani kama hii ni mara ya kwanza wao kutoa angalizo hili..

ila bado ni boko maana Rwanda ambao juzi walikuwa wanatafunana hawapakwi sifa hizi mbaya
 
Hivi vitu ni vya kawaida sana. Marekani huwa lazima wa rate nchi za africa hivi
 
Ha ha ha haaaa... Unajua kabisa Marekani siyo sawa na sisi, kwa msingi huo kwakua marekani ni mjumuisho wa majimbo kadhaa, basi na sisi tuunganishe Africa nzima halafu tuangalia matukio ya kiuhalifu yanayotokea kila siku ndo tuweke, ila kuweka matukio ya majimbo mbalimbali kwamba Marekani ni hatari ukilinganisha na Tanzania ni kujitoa ufahamu tu, Tanzania kwa marekani ni kajimbo kamoja tu.
 
Tanzania ilitakiwa itoe onyo kwa raia wake wanaotarajia kwenda USA
 
Tatizo serikali wenyewe ndio wanakuza haya Mambo kwa kusema upinzani wasifa ye mikutano maana Kuna Mambo ya kihalifu huenda yakajitokeza kulingana na taarifa za Kiinteligensia
 
Hawa wapumbafu wako bize na mataifa mengine wakati kwao hakuna amani.
 
Hivyo vita vyenu piganeni wenyewe. Mnataka kuwashirikisha wananchi ili wafe wakilinda milo yenu. Pambaneni wenyewe na hao wamarekani
 
Hao siyo magaidi, hao ni special unit for special task... wanafanya kazi kwa commands... hawana interest na kile wanachokifanya...


Cc: mahondaw
Nakuelewa sana mkuu, ila elewa matokeo ya wanachokifanya tafsiri yake ni ugaidi.

Vipi kama kikitokea kikundi kikaanza kuteka viongozi wa serikali kwa mtindo huohuo kwa mfululizo itakuwaje?

Matukio kama kushambuliwa kwa Tundu lisu na yule mfanyabiashara wa Mwanza tuyatafsirije?

Serikali yoyote duniani ikikosana na wananchi wake matokeo yake ni kutengeneza mianya ya kuruhusu makundi ya kigaidi kujijenga na kuingia kwenye nchi husika

Kwa sasa kuna mgawanyiko mkubwa miongoni mwa watanzania jambo ambalo linayafanya mataifa ya magharibi yachekelee tu yakijua kwamba siku yakiamua kufanya hii nchi isitawalike ni rahisi sana.

Kama chadema waliweza kupata zaidi ya kura milioni 6 unafiki kundi hilo lote linachukuliaje vitendo wanavyotendewa viongozi wao na baadhi ya wanachama wenzao? Kundi hilo ni watanzania na wapo karibia kila kaya hapa nchini, kuna hawa wastaafu wanatungiwa sheria za kipumbavu, kuna watu wa kanda fulani waliambiwa na kiongozi wa nchi kwamba, ndani ya utawala wake maendeleo kwao watasubiri, wengine walipewa upendeleo kwa kuwa ndio walimuweka madarakani eti!
Kuna kauli nyingi tata ambazo Watanzania wanazo vichwani mwao.

Mambo hayo yote yameleta mgawanyiko mbaya kwenye jamii ya Watanzania huku yakifumbiwa macho alafu leo hii litokee tatizo waanze kutaka wananchi wawe wamoja ilihali wameshawekwa kimatabaka.
Mataifa yaliyoshindana na mataifa ya magharibi yakashinda, kwanza kabisa yalianza kuwaunganisha wananchi wao ndipo yakaanza kupigana vita vya kujikomboa kutoka kwao.

Tunachokiona Tanzania ni tofauti.

Kwanza serikali iliyopo madarakani imefarakana na wananchi kwa kiasi kikubwa hadi kufikia asilimia kubwa ya wananchi kutamani mataifa hayo kuingilia kati
 
Vita vya kinini

We nyau ?!
 

Sipingani na ulichoongea ila principal ya kutawala watu kirahisi ni kwamba... kwanza wajaze uoga, pili divide them kwa namna yoyote ile, tatu tengeneza sheria zitakazo ku favour wewe zaidi kuliko wao... ukifanikiwa hayo, yoyote atakayekwenda kinyume unamfanya vile unavyotaka na kusiwe na chochote... huo siyo ugaidi... huo unajua mwenyewe unaitwa...

Tanzania ugaidi bado sana...


Cc: mahondaw
 
Mmmhhh Mbona sasa wanatutisha..!! au ndiyo wale waliokutana Zenji wakidai mwaka 2019 ni mwaka wa kudai Demokrasia.? hawachelewi kurushiana risasi then wenyewe alafu wasingizie polis!

Ila ni mbaya kwa wawekezaji sijui hawataki waje...!
Sasa bwana mkubwa kama una ushahidi kuwa huwa wanarushiana risasi halafu wanazingizia polisi kwanini usiupelekw kwenye vyombo husika badala ya kicheza BAIKOKO hapa jukwaani?!
 
hakuna jipya hapo,kiufupi wamewataka mashoga wasije Tanzania
 
Naona hata wewe hapa tayri umeshika mimba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…