Kumekuwepo na taarifa kwenye mitandao ya kijamii lakini pia gazeti la Mwananchi limeandika kuwa Serikali ya Marekani imewawekea vikwazo wanasiasa wanne wa Kenya pamoja na familia zao akiwemo Naibu Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua baada ya kupata taarifa kuwa wanasiasa hao walipanga na kufadhili vurugu wakati wa maandamano ya Jumatatu iliyopita.
Wanasiasa wengine katika orodha hiyo ni pamoja na Waziri wa Uwekezaji, Biashara na Viwanda, Moses Kuria, kiongozi wa walio wengi katika Bunge la Kitaifa, Kimani Ichungwa na Mbunge wa Kiharu, Ndindi Nyoro.
Ukweli wa taarifa hii upoje?
Wanasiasa wengine katika orodha hiyo ni pamoja na Waziri wa Uwekezaji, Biashara na Viwanda, Moses Kuria, kiongozi wa walio wengi katika Bunge la Kitaifa, Kimani Ichungwa na Mbunge wa Kiharu, Ndindi Nyoro.
Ukweli wa taarifa hii upoje?
- Tunachokijua
- Machi 29, 2023, habari ya viongozi wa Kenya kuwekewa Vikwazo na Serikali ya Marekani ilianza kusambaa Mtandaoni. Taarifa hiyo inayodaiwa kutolewa na Idara ya Hazina katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani inayodhibiti mali (OFAC), inasema wamechukua hatua hiyo baada ya kubaini kwamba viongozi hao walipanga na kufadhili vurugu Jumatatu iliyopita.
“Vitendo vyao vililenga kunyamazisha ridhaa, kukwamisha uhuru wa kuzungumza na uhuru wa vyombo vya habari, kukiuka utawala wa sheria, kuharibu masoko ya kiuchumi na kuhujumu demokrasia kwa ujumla nchini Kenya,” inaeleza taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Majina ya viongozi waliowekewa vikwazo pamoja na familia zao ni Naibu Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua, Waziri wa Uwekezaji, Biashara na Viwanda, Moses Kuria, kiongozi wa walio wengi katika Bunge la Kitaifa, Kimani Ichungwa na Mbunge wa Kiharu, Ndindi Nyoro.
Uchunguzi wa JamiiForums umebaini kuwa taarifa hiyo sio ya kweli. Pia, msemaji wa Ubalozi wa Marekani jijini Nairobi, Andrew Veveiros ametupilia mbali taarifa hiyo kwa kusema ni taarifa ya kughushi na kuwataka Wakenya kuipuuza.
“Ninaweza kuthibitisha kuwa taarifa inayosambaa mitandaoni ni ya kughushi kwani hakujakuwa na mawasiliano kama hayo kutoka kwa Serikali ya Marekani,” Veveiros alisema wakati akihojiwa na Citizen Digital.
Taarifa hiyo ilileta sintofahamu kubwa nchini humo huku baadhi ya wananchi wakianza kupata hofu kuwa huenda viongozi hao wangekabiliwa na mashitaka makubwa kwenye Mahakama ya Uhalifu wa Kivita (ICC).