Maria Sarungi alipewa na nani siri ya Ziara ya Rais Samia Nchini Marekani wiki moja kabla ya kutolewa Taarifa rasmi?

Maria Sarungi alipewa na nani siri ya Ziara ya Rais Samia Nchini Marekani wiki moja kabla ya kutolewa Taarifa rasmi?

Hata Mimi niliona post yake mapema wiki iliyopita kwamba eti wa huko Marekani waandae mabango maana Rais anakuja.

Kuna shida kubwa sana kwenye circe ya Rais na sijui kama Rais mwenyewe anafahamu kama Kuna watu wanavujisha Siri za Ikulu.

Nadhani safisha safisha iendelee.
Aliyekuwa ana vujisha siri za awamu iliyopita sasa anaonja joto ya jiwe na uchungu wa siri zao kuvuja
 
Mfuate Maria Sarungi Nairobi umuulize nani amempa taarifa chawa wa mama Abdul.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Unaweza ukaona kama ni jambo dogo lakini kwa jicho la tatu hili ni jambo kubwa sana linalopaswa kudhibitiwa kwa uharaka juu ya Mtu au watu au kikundi cha watu kinachoweza kuwa kinavujisha siri na taarifa za siri ambazo hazijawa rasmi na kutolewa kwa Umma.

Nasema hivi kwa kuwa wiki moja iliyopita Maria Sarungi niliona katika mtandao wake wa Twitter maarufu kama X akitoa taarifa kuwa Jumatano hii yaani kesho Rais wetu atatua Nchini Marekani.

Ambapo Maria Sarungi alieleza mambo mengine ambayo mimi binafsi nayachukulia kama uzushi na muendelezo wa tabia yake ya kuendelea kuchafua wale wote alio na hasira nao na chuki binafsi. Kwa kuwa amekuwa akiongea na kuandika vitu pasipo ushahidi wa aina yoyote ile na hata yeye amekuwa akikiri kuwa hana ushahidi.

Sasa Leo taarifa rasmi imetolewa ambapo imeonyesha kuwa Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi atakuwa Marekani siku ya kesho baada ya kuondoka hii leo.hii ikimaanisha kuwa taarifa iliyotolewa na Maria Sarungi wiki moja iliyopita juu ya safari ya Mheshimiwa Rais kwenda Marekani ilikuwa sahihi japo naamini maneno mengine ni ya uongo,uzushi na uchonganishi pamoja na kutaka kuwapaka watu matope hasa wale ambao ana chuki nao binafsi na kutumika na kutumiwa na watu walio nyuma ya pazia.

Swali langu ni je nani anayevujisha siri na kumpatia Maria Sarungi? Kwa Malengo gani? Kwa maslahi gani kwa Taifa letu?

Huyo mtu anataka nini? Anataka kujenga taswira ipi? Anamtumikia nani na kupokea maelekezo kutoka kwa nani?

Hata hivyo naipongeza sana awamu ya sita kwa namna ilivyodhibiti kwa kiasi kikubwa kudhibiti uvujaji wa siri za ikulu ukilinganisha na awamu iliyopita. Najuwa suala hili litafanyiwa kazi na wahusika na hatimaye kukibaini kirusi na kukiweka pembeni.

Hongereni sana wahusika kwa kazi hiyo ya kudhibiti uvujaji wa taarifa za siri.naamini hata hili mmeshaanza kulifanyia kazi na muhusika au kirusi hicho kitabainika na kunaswa na hatimaye kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria ,miongozo,taratibu na miiko ya kazi yake.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.

PIA SOMA
- Rais Samia kuondoka leo Oktoba 29 kuelekea Marekani kuhudhuria mjadala wa Norman E. Borlaug

Kujua taarifa kuna tatizo gani? Kuna sehemu ya katiba inayozuia kupata taarifa hizo? halafu, watanzania wako zaidi ya milioni 60. Tusitegemee kila mtu aunge mkono juhudi.
Naturally, kuna upinzani wa kila mtu anachofanya. Shida iko wapi? Au shida ni wewe kutotambua ukweli huo?
 
Back
Top Bottom