WOWOWO
JF-Expert Member
- Aug 3, 2011
- 599
- 456
Kwa sisi wafuatiliaji wa siasa za upinzani Tanzania lakini na uhusiano kati chama dola na dola na chama dola na upinzani lakini mazingira ya siasa za Tanzania kwa ujumla wake tunafahamu kwamba siasa za Tanzania zinaishi katika state machinery ambayo ina players wengi. Lakini msingi na kazi endelevu ni kudumisha chama dola na mfumo uliopo.
Hakuna ubishi kwamba kwa muda mrefu sana vyama vya upinzani vimekuwa vya msimu. Vikiibuka na kuwa machahari na kutoweka katika chaguzi zinazofuata. Kwa CHADEMA hili limekuwa ni tofauti. Kwa miaka mingi tangu kisajiliwe kimedumisha ukuaji thabiti. Kikitishia mfumo na chama dola. Hatua iliyopo, CHADEMA imekifikisha CCM katika kuepuka na kuogopa kabisa sanduku la kura. Ni hatua ya vyombo vyote vya dola kupambana na CHADEMA na si CCM tena.
Hata hivyo, nyuma ya CHADEMA na uimara wake ni kuungwa mkono na makundi mengi ya kiraia. Ni kuwa na timu ya viongozi wanaokuwa wakishikamana na kuepuka kutofautiana. Ni kuepuka minyukano na mipasuko. Hii hutishia CCM na watu wa mfumo. Na kazi mara nyingi hulenga hapa.
Maria Sarungi kwa kipekee. Ni kama ndiye aliyesimama katikati hapa. Kazi yake ni kuratibu ukaribu ndani ya viongozi wa CHADEMA. Kutengeneza timu iliyo nje kwa udi na uvumba na kisha kuinjinia mitafaruku. Hii ilitokea kwa Zitto Kabwe. Utamwona na shangwe wakati wa Dr. Slaa na sasa wakati wa Tundu Lissu. Na mara nyingi hii hutokea ama wakati wa uchaguzi wa ndani ya CHADEMA au kuelekea mwaka wa uchaguzi mkuu. Historia inaonesha hajawahi kukipenda CHADEMA, wala kushiriki harakati zao isipokuwa hutaka kuwa mwendeshaji na mwamuzi wa mambo yao. Hapa ndipo hunasa vijana wanaokuwa na “njaa” ya maisha.
Kwa bahati mbaya ukaribu anaokuwa na viongozi hao hujenga picha yuko katika harakati za mapambano, anamiliki hakimiliki yake na kile pekee anachokiona ndicho kinakuwa sahihi. Kinacholeta utata ni viongozi kuamini “informal setup” na kuanguka kwenye mtego huo. ZZK aliangukia katika pambio hizo, akaondoka na asiinuke tena, CHADEMA ikabaki. Dr Slaa naye aliona hivyohivyo kwamba CHADEMA kitayumba, lakini kipo palepale kikiwa kikuu na tishio. Hili kwa Lissu pia linaweza kuhitimishwa hivyo. Walau angekuwa katika institutionalized setup kama kweli ana ideals ili sasa zijenge continuity kwa wale wanasiasa anaoamini kwamba wako katika mrengo na muono wake. Hafanyi hivyo. Wakianguka, kazi imekamilika hutengana nao, kisha anasaka wengine.