Pre GE2025 Maria Sarungi kapatikana na karudi nyumbani kwake, ataongea kuhusu suala hilo Januari 13, 2025

Pre GE2025 Maria Sarungi kapatikana na karudi nyumbani kwake, ataongea kuhusu suala hilo Januari 13, 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mwanaharakati Maria Sarungi ambaye alidaiwa kutekwa leo nchini Kenya, amepatikana huku akiahidi kuzungumza zaidi kesho baada ya kutulia.

Taarifa ya kutekwa kwa Maria ilitolewa leo Jumapili Januari 12, 2025 na taasisi ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu ikisema: “Maria Sarungi Tsehai, mhariri huru wa vyombo vya habari nchini Tanzania na mtetezi wa haki za binadamu, ametekwa nyara na watu watatu wenye silaha katika eneo la Chaka, Kilimani jijini Nairobi.”

Soma Pia: Mwanaharakati Maria Sarungi adaiwa kutekwa na watu wenye silaha Nairobi, wakiwa na Noah nyeusi

Katika video fupi iliyochapishwa katika ukurasa wa X (zamani Twitter) wa Faith Odhiambo ambaye pia ni rais wa 51 wa Chama cha Wanasheria Kenya (LSK) imemuonesha Maria akiwa na Faith pamoja na watu wengine, huku Maria akiahidi kuzungumza kesho.

“Asanteni sana, nipo salama, Mungu ni mwema. Kesho nitachukua muda, nitaongea,niwashukuru Wakenya, Watanzania na watu wote wa kimataifa..Kwa sababu leo nimeokolewa,”amesema Maria
 

Attachments

  • Screenshot_20250112-204405.png
    Screenshot_20250112-204405.png
    269.2 KB · Views: 2
Thanks Kenyan government.. Wameshindwa kumvusha boda?
Probably she is already fixed.
Anaweza kuanza kukaa kimya au God forbid, a fixed dose will work it's magic like a slow puncture...
 
Mungu ni mwema, shukrani kwa kelele za Watanzania wote.
shukrani pia lile shirika pale kenya wameeleza wazi kuwa mkosoaji wa serikali ya saa 100 ametekwa na mijanaume mitatu ikiwa na bastora naona ruto aliingia kazini
 
Back
Top Bottom