Pre GE2025 Maria Sarungi kapatikana na karudi nyumbani kwake, ataongea kuhusu suala hilo Januari 13, 2025

Pre GE2025 Maria Sarungi kapatikana na karudi nyumbani kwake, ataongea kuhusu suala hilo Januari 13, 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wakuu,

Kupitia ukurasa wake wa X, Fatma Karume ameweka post ya kuwashukuru wote waliyohakikisha Sarungi anakuwa salama, na kwamba ameambiwa Sarungi amerejea nyumbani kwake.

View attachment 3199978yu
Haisemekani.

Ni kweli mchumba wa marehemu meko na kasongo wamemuachia Maria

Kinachotakiwa inabidi Maria ahamie nchi nyingine hapo Keny sio safe tena
 
Mwanaharakati Maria Sarungi ambaye alidaiwa kutekwa leo nchini Kenya, amepatikana huku akiahidi kuzungumza zaidi kesho baada ya kutulia.

Taarifa ya kutekwa kwa Maria ilitolewa leo Jumapili Januari 12, 2025 na taasisi ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu ikisema: “Maria Sarungi Tsehai, mhariri huru wa vyombo vya habari nchini Tanzania na mtetezi wa haki za binadamu, ametekwa nyara na watu watatu wenye silaha katika eneo la Chaka, Kilimani jijini Nairobi.”

Soma Pia: Mwanaharakati Maria Sarungi adaiwa kutekwa na watu wenye silaha Nairobi, wakiwa na Noah nyeusi

Katika video fupi iliyochapishwa katika ukurasa wa X (zamani Twitter) wa Faith Odhiambo ambaye pia ni rais wa 51 wa Chama cha Wanasheria Kenya (LSK) imemuonesha Maria akiwa na Faith pamoja na watu wengine, huku Maria akiahidi kuzungumza kesho.

“Asanteni sana, nipo salama, Mungu ni mwema. Kesho nitachukua muda, nitaongea,niwashukuru Wakenya, Watanzania na watu wote wa kimataifa..Kwa sababu leo nimeokolewa,”amesema Maria

Hii movie yake mbona kama inaelekea kubuma?!!
 
Back
Top Bottom