SI KWELI PreGE2025 Maria Sarungi kupitia X ameandika Oktoba Tunatiki

SI KWELI PreGE2025 Maria Sarungi kupitia X ameandika Oktoba Tunatiki

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
MARIASARUNGI12JUNI2025.jpg
MARIASARUNGI12JUN2025.jpg
 
Tunachokijua
Maria Sarungi ni mwanaharakati kutokea Tanzania, ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kupigania haki za binadamu, utawala wa kisheria unaozingatia misingi ya kidemokrasia ambapo pia amekuwa akitumia mitandao ya Kijamii hasa mtandao wa X.

'No reforms, No election' ni agenda ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA yenye lengo la kushinikiza kufanyika kwa mabadiliko na maboresho ya mifumo ya uchaguzi ikiwemo sheria za uchaguzi ili kuwezesha uchaguzi huru na haki. Maria Sarungi amekuwa ni moja kati ya wanaharakati ambao wamekuwa wakiunga mkono ajenda hiyo ya CHADEMA.

Katika siku za karibuni agenda hiyo imeshika kasi katika mitandao ya kijamii, ambapo watumiaji wa mitandao wamekuwa wakiitaja ajenda hiyo sehemu ya maoni (comments) katika kurasa za watu binafsi, taasisi na vingozi wa serikali, kuonesha kuiunga mkono.

Baadaye upande wa chama tawala (CCM) uliibuka na kampeni ya 'Oktoba Tunatiki' ikieleza kwanini uchaguzi utafanyika mwezi Oktoba na kichaguliwe chama hicho ikiwa hatua ya kujibu mapigo dhidi ya ajenda ya 'No reforms, No election'

Kupitia Mtandao wa Facebook Ipo 'Screen shot' inayosambazwa kuwa Maria Sarungi ambaye amekuwa akiunga mkono ajenda ya 'No reforms no election' alichapisha kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa X, kuonesha kuikubali kampeni ya 'Oktoba tunatiki'


Je, ni upi uhalia wa chapisho hilo?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key word search) umejiridhisha kuwa chapisho hilo si la kweli kwani halikuchapishwa na Maria Sarungi kupitia ukurasa wake mtandao wa X.

Chapisho hilo limetengenezwa na wapotoshaji na kulisambaza mtandaoni ili kupotosha uhalisia. Kumbuka wapotoshaji wanaweza kutumia utambulisho wa mtu mashuhuri kusambaza taarifa isiyo ya kweli ili kuwaaminisha wananchi.

Lakini pia kupitia ukurasa wake wa X, Maria amekanusha chapisho hilo na kwamba hahusiki nalo.

"Mnatafura endorsement yangu kwa nguvu ya nini? Mi nilishaweka msimamo jana hadi Instagram kuwa hii kampeni yenu ni UPUUZI Poleni! #NoReformsNoElection ndo jibu pekee kwa sasa"

Vilevile Chapisho lililotumika kusambaza ujumbe huo ni la kughushi kwani halikuchapishwa na kurasa za The Chanzo.
​
Back
Top Bottom