Maria Sarungi: Nilitekwa nikiwa natoka saluni. Lengo lilikuwa ni kunivusha lakini hawakufanikiwa

Maria Sarungi: Nilitekwa nikiwa natoka saluni. Lengo lilikuwa ni kunivusha lakini hawakufanikiwa

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Kama alivyotuahidi jana, siku ya leo Mwanaharakati nguli Afrika Mashariki, Maria Sarungi atazungumza kinaga ubaga kuhusu namna alivyotekwa mpaka kupatikana kwake.

Bado haijaeleweka hadi sasa kama atazungumza kwa kujirekodi video kueleza nini hasa kilitokea, atatengeneza thread ya kuelezea tukio zima au atatoa tamko kupitia space.

Soma pia: Kuelekea 2025 Mwanaharakati Maria Sarungi adaiwa kutekwa na watu wenye silaha Nairobi, wakiwa na Noah nyeusi

Tanzania inasubiri. Kaa karibu na uzi huu kujua kitakachojiri

Presssss.jpeg

==========================================

"Jana niliondoka nyumbani kwenda saluni ili kutengeneza nywele zangu. Nilipofika, wakati namaliza, niliona mwanamke aliingia ndani ya saluni haraka haraka alafu akatoka, alikuwa amevaa mask. Sikufuatilia sana baada ya kuona hivyo"

"Mara nyingi mimi huwa nawasiliana na mume wangu nimpe updates za wap nilipo. Kwa hiyo nikamtaarifu kwamba nataka kuondoka. Nikatumia app ya Little ya kuita gari y kunirudisha. Yule dereva alifika lakini hakuweza kuingia ndani"

"Kwa hiyo nikawa naenda getini ili niweze kuingia kwenye gari na wakati dereva anajaribu kuondoa gari ili kulipeleka barabarani, kuna mwanaume mmoja mweusi alitoka kwenye gari yao na wengine wawili wakaanza kumfokea dereva kwamba afungue mlango. Na mimi nikamwambia dereva asifungue mlango wa gari"

"Baada ya hapo waliweza kufungua mlango na wakaanza kunivuta nje nikaanza kupambana nao ili nisitoke nje ya gari lakini waliweza kunibeba na kuniingiza kwenye gari yao. Nilikuwa napiga kelele sana kuomba msaada baada ya muda wakaanza kujaribu kufiha uso wangu ili nisiwaone"

View: https://www.youtube.com/watch?app=desktop&v=81e_duSZSc0

Maria akizungumzia iwapo Serikali ya Tanzania ilihusika katika utekaji wake:

Wakuu,

Kama alivyotuahidi jana, siku ya leo Mwanaharakati nguli Afrika Mashariki, Maria Sarungi atazungumza kinaga ubaga kuhusu namna alivyotekwa mpaka kupatikana kwake.

Bado haijaeleweka hadi sasa kama atazungumza kwa kujirekodi video kueleza nini hasa kilitokea, atatengeneza thread ya kuelezea tukio zima au atatoa tamko kupitia space.

Soma pia: Kuelekea 2025 Mwanaharakati Maria Sarungi adaiwa kutekwa na watu wenye silaha Nairobi, wakiwa na Noah nyeusi

Tanzania inasubiri. Kaa karibu na uzi huu kujua kitakachojiri
anataka kuzungumza jinsi alivyo jiteka sio?

hata hivyo bado hawezi kufikia wala kuvunja rekodi ya kiwango cha kujiteka cha Abdul nondo wa act 🐒
 
U miongoni mwa maiti zinazotembea paka wewe.
Hivi unadhani mtaendelea na upumbavu mpaka lini✍️
sasa ndungu mpenzi wa movie za kujiteka,

ukimpima huyo mumama wa kujiteka Kenya, anaweza kumfikia Abdul nondo kwa ustadi wa kujiteka Kweli?

Hata hivyo gentleman
kujiteka ni miongni mwa mambo ya hovyo sana kufanywa na mtu mzima ati ili tu awe maarufu au kusingizia wengine waonekane wabaya 🐒
 
Back
Top Bottom