Mariam Wangwe na Jukwaa la Wahariri

Status
Not open for further replies.
Sidhani kama mtoa hoja alikuwa na nia mbaya na Dr. Slaa.Alichokuwa anamaanisha si kila neno utamkwa na kila kinywa hata kama ni kweli.

"Sijawahi kujuta kwa kukaa kimya" Luqman akimwambia mwanae
 

Lakini mbona hapa jf tunatamka kila kitu? Tabia ya kufichiana ukweli katika nchi hii ndiyo iliyotufikisha hapa wakuu
 
Anayo sema Dr W. Slaa ni sahihi katika taratibu za kisheria anatambulika msimamizi wa mirathi mmoja tu aliyeteuliwa na familia. Katika tamaduni za wenzetu hao unaweza kuoa wake wengi na hata wanawake kuoana wenyewe wanaita ndoa ntobi sasa kwa ishu hii inaonekana hawa majamaa wameshamteka .Mafisadi bwana sio mchezo na lengo ni kuwasambaratisha watu wanaowaumiza vichwa kama Mzee Slaa. Wanachotakiwa kufanya sio kuzungumza na vyombo vya habari wayamalize wao kama familia kwanza.
 
Umetumwa nini?
Hebu soma hapa usikurupuke na wewe

ndugu yangu mbona wewe ndiye unayekurupuka???
hiyo habari ya gazeti la mwananchi mbona umei-edit??kwanini usii-copy na kui-paste kama ilivyo??wewe una lako jambo tena unataka kupotosha watu.

kwanini umeiondoa kauli ya dr.slaa kama ilivyonukuliwa kwenye gazeti(na mwandishi wa habari)??

yaani watu wengine sijui mkoje?yani akiguswa kiongozi wa chadema au chadema yenyewe povu linawatoka!!!

dr.slaa kwani yeye ni nani hadi asikosee?mara ngapi anachemka na watu tunaelewa kuwa amechemka. tatizo lenu wapambe kila jambo mnapinga tu bila hoja.
Imani yake ya ukatoliki haiingiliani na suala la ndoa ya mtu mwingine.
na mtu huwezi kuitambua/kutoitambua ndoa ya mwenzako kwa misingi ya imani yako isipokuwa kwa mujibu wa sheria na katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania,wala si kwa sheria za katoliki,lutheran,uislamu ama nyingineyo.

ukweli ni kuwa hapo dr.slaa ameyumba.

soma hapa kauli ya dr.slaa uliyoificha:
"Dk Slaa ambaye alisisitiza kwamba hamfahamu Mariam kama mke wa marehemu Wangwe, alisema anasikitishwa na kauli yake ambayo anaamini kuwa imelenga kukichafua chama".
 
Lakini mbona hapa jf tunatamka kila kitu? Tabia ya kufichiana ukweli katika nchi hii ndiyo iliyotufikisha hapa wakuu

Kutokutamka kila kitu haimaanishi kwamba unamficha mtu ukweli na si kila ukweli usemwa ndugu yangu.ndo mana watu wakasema unatakiwa kufikiri kabla ya kusema.kama unaongea kila kitu tena bila hata ya kufikria kwanza basi kuna tatizo.
 
nawewe soma hapa,inaonekana macho yako yanaangalia baadhi ya maneno yanayokufurahisha,yasiyokufurahisha huyaoni.na kwa faida ya wote tunaojadili naomba niiweke habari nzima bila kuipunguza au kuiongeza chochote kama ifuatavyo.

 

TanzaniaNjema,

Nakuheshimu sana, kunawiri au kuanguka kwa Chadema hakunihusu unless unazungumzia upinzani at large. Before Chadema comes into picture tulikuwa na powerful NCCR hapa halafu CUF wamevurunda kwa upuuzi wao na wamekufa kifo cha mende na kama Chadema ( na kwa mwendo huu they will ) wataanguka so be it watakuja wapinzani wengine bado tupo katika evolution stage ya upinzani mpaka hawa wababaishaji watakapoondoka wote then hao manabii wa kweli ndio watakuja. Mimi sina jukumu la kui babysit Chadema they r old enough kujua wanayoyafanya hayana tija kwa taifa.

Tanzanianjema unataka watanzania wote tuwe Chadema? why not CUF, TLP. NCCR waambie hao jamaa zako kwa mwendo huu wanatupeleka siko na hatuko tayari kuburuzwa, eti Chadema yafaa kulindwa kwa hali na mali! r u kidding me?

Chadema hawatafunwi wanajitafuna wenyewe kwa siasa zao chafu za "kushughulikiana" ( political of elimination ) kila wanapotafautiana na wenzao. Safisheni nyumba yenu msitafute mchawi kutoka nje mchawi ( ukabila ) mmeu asisi wenyewe....
 
Namtafuta Mwarabu wa Tabora, tajiri mmoja hivi aliyezaa watoto wawili na Mariam ambaye baada ya kufilisika Mariam alimuacha na kukimbilia kuolewa na Wangwe. Kuna maneno Mariam ameyasema leo, nataka sana kuongea na huyu mwarabu kupata kauli yake. Nisaidie namba yake tafadhali. Hili suala libaki kwenye siasa kwa kuwa kuna kauli nzito imetolewa kuhusu Samuel Sitta na siasa za Tabora.

PM
 
Hii habari mpya tena!! Huyu Mariamu alishaolewa tena na Mwarabu!?
 

MMhh! Pesa ya Rostam Azizi hiyo. Kazi kweli kweli!
 
Wanabodi,

Binafsi sidhani kama kuna kitu kimeharibika hapa kiasi kwamba lawama ziwe za chama.
Nimesoma maelezo ya Dr.Slaa na inaonyesha wazi kwamba amekuwa akisisitiza kulingana na madai ya Marium kuwa yeye pamoja na viongozi wote wa Chadema walialikwa Hitma (Arobaini) kama watu binafsi..
Na ndio Utaratibu wakidunia huwezi kualika watu msibani kutokana na nyadhifa ama mtazamo wao kichama...Watu hualikwa msibani ama ktk harusi kama watu binafsi na familia zao..
Kuna misiba kibao ya viongozi wa juu CCM wameondoka na hatukuona viongozi wa chama wakihudhulia (Arobaini) wala sio swala la kulaumu hata kidogo kwa sababu hitma haikamiliki kwa kuhudhulia viongozi ama vigogo isipokuwa dua za watu ndio hitma yenyewe.. Again, bado inatuonyesha sisi kuwa waafrika bado kabisa tunaamini na kuabudu zaidi watu badala ya maandiko - neno la Mungu.

Kwa hiyo, hili linajibu swali la Marium anapojaribu kuhusisha msiba na siasa za chama. Na Dr.Slaa aliposema hamtambui Marium kama ni mke wa Marehemu ni mawazo yake Dr.Slaa binafsi na pengine anazo sababu za kuweka madai hayo..Yawezekana kabisa kuwa Marium kaolewa nje ya sheria hizo hizo mnazotaka kumfunga Dr. Slaa..Sina hakika Marium ni dini gani lakini yanipa fikra tofauti hapa kuwa yawezekana wamefunga ndoa Halmashauri ya jiji, kienyeji, msikitini ama kanisani.
Kisheria ni hadi pale ndoa hiyo imekuwa registered ndipo hutambuliwa kisheria kwa sababu hizo option zote za kufunga ndoa hazihalalishi ndoa isipokuwa pale inapokuwa registered. Mara nyingi watu wengi hufikiria kwamba wakienda kuoana katika Ofisi za Halmashauri. msikitini ama kanisani basi ndoa zao zimefuata sheria..
Pili yawezekana kabisa kwamba Marium alitambulishwa kwa baadhi ya viongozi wa Chadema na sio yeye kwani nina hakika kabisa kuwa hata Kikwete leo hii pamoja na kwamba ana mke wa pili wapo viongozi wa juu CCM hawafahamu wala hawajapata kujulishwa..Hivyo siku huyu mkewe akitoa madai fulani yanayokilenga chama ni muhimu afahamu nafasi yake pia inaweza kupingwa na baadhi ya viongozi... Kwa sababu hawamtambui kama ni mke wa rais hata kama habari hizi wamezipata kupitia vyombo vya habari.

Mwisho kama utasoma vizuri habari hii kama ilivyoandikwa, inaonyesha wazi ni viongozi wa Chadema waliosema Dr. Slaa anatakiwa kumwomba radhi Marium.. hivyo kwa nini lawama hizi zinawashukia Chadema kama chama..
Kabla huyu mama hajajitokeza ktk vyombo vya habari kuna mmoja wenu alimfahamu huyu mama kama mjane wa marehemu?...yeye analalamikia viongozi wa Chadema kutohudhuria Arobaini mbona yeye hakuhudhuria mazishi ya mumewe!...kuna kosa hapa duniani kwa mke wa marehemu kutohudhuria mazishi ya mumewe?...unless huyu mama Marium hatambuliwi na familia ya marehemu kwa hiyo kuna utata mkubwa ktk ndoa hii, laa sivyo angekuwepo Tarime kama mjane wa marehemu.
 

Highlighted says it all, kama ni kweli hakuhudhuria mazishi hii kali asipige kelele kwenye 40...
 

Viongozi gani wa CHADEMA waliosema hayo? Hebu tupeni majina na nafasi zao kama ni wasemaji wa CHADEMA. Isije ikawa kama kawaida yao mafisadi wanavika mtu cheo hapo kuwa msemaji wa CHADEMA muhuni tu wa mtaani na wote mnaingia mkenge!

Asha
 

Heee. Jamani, ni kweli kuwa Mariam alimuacha mumewe mwenye watoto naye wawili halafu akaenda kuolewa na mwanaume mwingine aliyekuwa na wake wawili tayari? Au mnataka tu kutunyanyasa kijinsia? Kuna mtu mwenye namba ya Mariam Mwanakijiji afanye naye interview?

Asha
 
Asha Abdalla,
Utanisamehe, kulingana na mwandishi kwani huyo Beatrice ni nani?
Kisha elewa nachozungumza hapa kabla hujarukia ngamia huyu..
Binafsi sioni kosa hata kama ni viongozi wa Chadema kwa sababu ni wao wameliona kosa na wanakumbuka kwamba Marehemu kisha wahi kuwatambulisha..
Kwa hiyo sioni kosa la kuweza kukilaumu chama kizima wakati ni chama hicho hicho kilicho tufahamisha kuhusiana na Marium kutambuliwa kama ni mke wa marehemu.
 

Mkandara,
Nakubaliana karibu na yote uliyoyandika juu ya hili.

Hivi ni kweli huyu mama hakwenda kwenye mazishi ya mumuwe Tarime? Sijawahi kusoma popote kama hakwenda.
 
Mkuu hakwenda...na hawezi kwenda... bahati mbaya Ushahidi haupo ktk maandishi.
 

Jamani, mi sijasoma. Nitajie basi jina la huyo kiongozi wa CHADEMA na nafasi yake. Isije ikawa ni wale wanaojipachika vyeo na kujiita wasemaji wa chama ngazi yao kumbe ni gelesha.

Asha
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…