Mariam Wangwe na Jukwaa la Wahariri

Mariam Wangwe na Jukwaa la Wahariri

Status
Not open for further replies.
Mwezi uliopita katika debate moja jamaammoja alisema kwamba vyamavya siasa haswa vya upinzani vinategemea upepo wavyombo vya habari ndio na vyenyewe viibuke vianze kusema na kadhalika ---ni kweli si unaona hii ya mrs wangwe ? Ni vyombo vya habari vimemwandika sasa chadema inataka kuchukulia credita hapohapo

Kama si vyombo vya habari utajuwa vipi reaction ya wananchi?

Sasa utareact vipi kabla hujajuwa wananchi wamezipokea vipi habari hizo?

Ni wajibu wa wananchi ku read between the lines na kuelewa nani ni mpotoshaji na nani mwenye ukweli.....Kipindi hiki cha uhuru wa habari pia tunahitaji analyzers...

Kama habari hizo zina upotoshaji...Then ni wazi hatua za ku counter hizo news mbofu mbofu zitafanyika na hiyo ni baada ya wananchi kupata hizo zinazoitwa habari kutoka kwenye upepo wa vyombo vya habari.

Sasa Shy guy/lady kama wewe ni informer...Then usidhani kila mwananchi ni the same.

Ukiwa na empathy utaweza kushirikisha ubongo wako na kujiweka kwenye nafasi ya mwananchi wa kawaida badala ya kuishi kwenye jamii yako na fikra zako wewe mwenyewe za kishushushu na ku assume kwamba kila mwananchi anaweza kupata habari kabla ya kusikiliza ama kusoma kutoka kwenye huo upepo wa vyombo vya habari.

UPO?
 
Mwaka jana niliwahi kuandika hapa hapa .Kwanza asante sana ndugu Tanzanianjema kwa uchambuzi wako mfupi ila una mwaga nyeti kibao.

When I met late Chacha Wangwe siku hiyo pale Hotel G & G Musoma , ilikuwa jioni moja baada ya wao kuwa wametoka Jimboni kwao .I had sometime kusema na huyu mwanamke nikagundua she was a looser na mtu aliyekuwa anavizia jambo fulani .Alionyesha chuki za wazi juu ya Chadema na hasa Mbowe na huku akitaka kuniaminisha kwamba Chacha alifaa kuwa Mwenyekiti wa Chadema .Alionyesha chuki za wazi kwa Zitto na wakataka kunilisha sumu dhidi ya Zitto lakini wakashindwa maana walishindwa kunijibu maswali yangu.

Yule mama uwezo wake wa kufikiri nafikiri una kikomo kikubwa so leo akianza kuingia hapa na kusema haya sitashanagaa kama Prof Wangwe na Kebe walivyo panda jukwaani na kusema waligundua wao kwamba mbavu zimevunjwa .What a shame .Kwa mtu kama Prof .Wangwe we all know kwamba ni mwana CCM na mshikaji wa karibu wa JK lakini sikutegemea ajivue nguo kisa CCM wapate jimbo .

Huyu Mama ana mengi na ni mty hatari si kwa umma pekee bali hata familia ya Marehemu Wangwe .Ni yeye aliyekuwa na mawazo ya kumwambia wangwe kwamba awe mkombozi wa Chadema maana Mbowe kashindwa kuongoza na kuleta majungu na maneno ya ukabila ambao leo hii pamoja na Wangwe kushindwa kuonyesha Ukabila ndani ya Chadema lakini hata yeye hana kusimamia juu ya ukabila.

Jamani nawaombeni
wana chadema muwe straight foward.
tuambieni tuelewe ninyi mko ktk msimamo upi? yani JE?Marehemu chacha ALIKUA MPIGANIA DEMOKRASIA na HAKI ama ALIKUA MVURUGA DEMOKRASIA NA HAKI.
 
Kabla ya yote ni vizuri kumuuliza huyu mama kuwa iweje alipofika tu kuona mwili wa mume wake akakimbilia card za benki. Hivi amewakilisha hizo card za benki kwa wanafamilia? Hivi uhusiano wake na wake watatu wa wangwe aliozaa nao watoto lukuki na kupambana pamoja hadi alipoukwa ubunge ukoje? Hivi iweje mama huyu na usomi wake wote pamoja na connection yake kifamilia na vigogo wa asasi nyeti nchini akae nyumbani bila ya kazi yoyote miaka yote hiyo? Hivi iweje Marehemu Chacha aanze juhudi za kuvuruga CHADEMA mara tu alipoliingia penzi la mama huyu ambaye ni mwanachama wa damu wa tabaka tawala lilojaa ufisadi?

Hivi sio huyu mama ndiye aliyekuwa akisaidiana na GACHUMA, Binamu wa Marehemu Mzee KEBA aliyesimamia kifungo cha Chacha gerezani wakati ule, na mawaziri wa CCM akiwemo Mama Kabaka kusammbaza sumu za kuwa Chacha aliuawa na maadui ni CHADEMA? Sasa alitegemea nini kutoka kwa viongozi wa CHADEMA wakati ni yeye aliyekuwa akiwalisha sumu ya chuki hadi wanafamilia ambao ukitoa kada KEBA hapo kabla hawakuwa na tatizo na wanaCHADEMA? Labda akamuulize RPC na RC ni kwa nini walimwambia kuwa hawatakuwa responsible na USALAMA wa Mbowe wakati ndio jukumu lao....

I mean kama huyu mama aliweza kuwa kipenzi cha wapinzani hovyo kina MBATIA, MREMA, LIPUMBA waliodandia lifti ya ndege ya MBOWE halafu wakafikia kumgeuka na sasa MTIKILA....ninamini kuwa hii inaweza ikawa missing link inayotafutwa kwa wale wenye kuamini kuwa marehemu Chacha hakufa kifo cha ajali ya kawaida....

Naamini huyu mama ndiye wa kubanwa maana ana mengi ya kufill the gaps haswa kuhusiana na watu ambao Marehemu Chacha Wangwe alikuwa akikutana nao mara kwa mara wiki chache kabla ya kifo chake....

Na pia tuangalie ajira halisi ya mama huyu........

JK,MREMA,LIPUMBA,MBATIA ,MTIKILA ni wana siasa ovyo ni wepi wana siasa safi?
 
Jamani nawaombeni
wana chadema muwe straight foward.
tuambieni tuelewe ninyi mko ktk msimamo upi? yani JE?Marehemu chacha ALIKUA MPIGANIA DEMOKRASIA na HAKI ama ALIKUA MVURUGA DEMOKRASIA NA HAKI.

sasa hivi watakuambia alikuwa mpigania demokrasia ila walivyomsimamisha alipoteza hiyo hadhi alivyoaga dunia akapewa tena hiyo hadhi!
Eeeh MUNGU tusaidie!wanadamu ni wanafiki kweli kweli
 
Hallooooo! anybody home?..

Nilishasema viongozi wa Chadema inawabidi watupe ukweli sisi wananchi na wanachama kuhusiana na Wangwe... Kama hawahusiki ni bora zaidi waende Tarime na kuwahutubia wananchi kile wanachofahamu wao..Na Mbowe awe msitari wa mbele kuwahakikishia wananchi wa Tarime kuhusiana na tuhuma hizi tofauti na mambo anayoyafanya Kikwete ili kuondoa mzizi wa fitna.

Binafsi ninaamini kabisa Mbowe hana Ubavu wa kutoa roho ya mtu kwa sababu ya Uenyekiti wa chama. Chadema hawana nguvu ya mafia ya kuhakikisha wanamuondoa mtu duniani kwa sababu ya siasa za chama na kama wangeweza basi Kabourou na Tambwe wangekuwa watu wa kwanza kufungiwa kazi..
Pamoja na yote haya hizi tuhuma ziku zote huzaa maafa zaidi ndani ya chama. Ni wakati muafaka wa viongozim wa Chadema kuwa mbele ya tuhuma hizi na kama inawezekana chama kifanye uchunguzi ake binafsi kwa kutumia vyombo vya kimataifa kuhakikisha kwamba Mbunge wa Chadema hawezi kuondolewa uhai wake hivi hivi bila kueleweka...Sijali kabisa kama huyu mama kaongopa ama unasema ukweli wala sitaki kujua how credible madai yake... Ukweli ni kwamba Chacha Wangwe mbunge wa Chadema aliuawa!...
Tukumbuke slogan ya chama...
 
Mkandara imani yako ni sawa na yangu ila sasa nangoja Chadema kutema cheche hadharani tusikie ukweli ni upi
 
Tanzania njema naomba unijibu nini usaliti wa Mrema..Kwasababu huwa naheshimu mchango na hoja zako ila hapa naomba ufafanuzi tafadhali.
 
wanachadema
watupe jibu moja kua-

Wangwe alikua mpigania demokrasia ama alikua mvuruga demokrasia??

Maana mbinjuko wanaomugeuzia mama chacha inaleta tafsri ya kwamba mama anaendeleza alipokoma marehemu chacha.Sasa tunaomba tu mtuambie msimamo wenu.
 
This is among my favourite thread kwa leo!mambo yanasisimua ila ushadidi wa kutosha ndo hamna!ni spaculations tu........ na imani ndio vinatawala!tumesha sikia ripoti za madaktari na polisi!sisi yetu macho! tunasubiri mahakama iaamue juu ya hatima ya malya kama aliusika kwenye kifo hiki au laa!
 
Humble servant,
Mkuu sisi sote tulisikia report ya daktari lakini kinachotatanisha ni kwamba tuhuma za kwanza kabla ya uchunguzi ilikuwa CCM wahusika na CCM walihaha hadi report ilipotoka...wakatushauri wananchi kuwa ukweli ndio huo lakini ajabu ni kwamba hao hao CCM wakaanzisha tuhuma mpya kwamba Mbowe ni mhusika baada ya report ya daktari na kwa bahati mbaya hadi baadhi viongozi wa vyama vya Upinzani wakaingia mkenge huo..
Ni baada ya report ya daktari tumemsikia Mtikila, na sasa mke wa marehemu yote hii inaonyesha wazi kwamba hakuna mtu anayekubali report ile kuwa na ukweli mtupu bali imepikwa.. Kisha tukitazama upande wa pili yaani wa Chadema wenyewe wao toka siku ya kwanza aliyokufa hawakuamini kwamba Chacha Wangwe alikufa kifo cha kawaida na wameendelea kudai hivyo hata baada ya report ya daktari...

Sasa mkuu hawa wote ni wasomi wanaoelewa vizuri nini maana ya report ya daktari lakini wote wamepuuza report hiyo na kutuletea hadithi mpya kila siku.. Kwa hiyo ina maana hakuna hata kiongozi mmoja anayeamini kwamba Wangwe amekufa kifo cha kawaida kwa sababu wanajua kilichotokea haswa pamoja na kwamba kuna report ya daktari..
Sisi kama wananchi tunahaki ya kufahamu ukweli na kama wataendelea kuficha kwa kuogopa watu fulani ama nguvu fulani basi inaonyesha wazi hatuna viongozi ambao wako tayari kujitoa mhanga kusema ukweli itakapo fikia mambo makuwa zaidi..
 
huyu mama naona anatumiwa au anatafuta umaarufu wa kisiasa!!!
 
JK,MREMA,LIPUMBA,MBATIA ,MTIKILA ni wana siasa ovyo ni wepi wana siasa safi?

Mkamap... wanasiasa safi ni Makamba na Msekwa wanaotumwa na JK kudhibiti fujo na ambao wanataka kuturudisha kwenye "Chama kushika utamu"
 
Niliwahi kuweka Active Users, mtu mmoja akaniona wa ajabu, lakini kwa watafiti walielewa nina maana gani na hapa leo hebu angalieni, members 10 guests 20.

Currently Active Users Viewing This Thread: 30 (10 members and 20 guests)
Halisi, Bonnie1974, cola, Jeni, kwayu, mburahati, nono, sabasaba, WildCard
 
Jamani jamani msipuuze ya huyo mama. Huenda pia chacha kachukuliwa msukule na akina Wilbrod....Hivi hamjui kuwa huyo Wilbrod kabla ya kuwa mbunge na kiongozi wa kiroho alikuwa ni mcheza mazingaombwe!!Ni bingwa sana wa masuala ya akina kalumanzila!!!!
 
Mkamap... wanasiasa safi ni Makamba na Msekwa wanaotumwa na JK kudhibiti fujo na ambao wanataka kuturudisha kwenye "Chama kushika utamu"

Hapana wanasiasa safi ni Mbowe, Zitto, Slaa et al wanapotofautiana na kiongozi mwenzio "wanamshughulikia"
 
Hapana wanasiasa safi ni Mbowe, Zitto, Slaa et al wanapotofautiana na kiongozi mwenzio "wanamshughulikia"

Masatu uwezo ni mkubwa mno wa kuchambia hoja .Wewe si kama makapu wewe ni mzee wa kijiwe hiki.This is extreme kwa kweli .Unata tuhuma nzito amabazo sitaki kuamini kwamba upasha baraza joto .
 
Hapana wanasiasa safi ni Mbowe, Zitto, Slaa et al wanapotofautiana na kiongozi mwenzio "wanamshughulikia"

Fafanua "kushughulikia" maana kushughulikia kupi?

Nadhani kama ni suala la kushughulikia, shahidi mkuu atakuwa Mudhihir M. Mudhihir aliyekuwa na Wangwe dakika chache kabla ya kuondoka anajua jinsi alivyoambiwa na marehemu kwamba ameamua kuwasaliti waliompa fedha abadili msimamo wake kisiasa ndani na nje ya Bunge. Mazungumzo hayo Mudhihir hawezi kuyapinga maana aliowaambia baada ya kifo cha Wangwe wamebaki na kumbukumbu hiyo muhimu. Zaidi yataletwa kadiri munavyozidi kutumia kifo cha Wangwe kuwachezea akili Watanzania, kifo ambacho kama ni kupangwa kilipangwa kwa malengo yanayoendelea sasa ya kuzima moto wa vita ya UFISADI
 
Hizi ni ngano ulizotunga wewe mwenyewe. Mh Mudhihir amekaririwa na vyombo vya habari kuwa walikuwa wanataniana na Mh Wangwe kuhusu Yanga kutopeleka timu uwanjani dhidi ya Simba. Na yeye Mh Mudhidhir akamrudishia kuwa hajui kuvaa suti ( alifunga buttons zote ) wakacheka na Mh Wangwe akaenda zake and the rest is history.

Hii ya kwako mpya, mkuu umenoa try again...
 
Masatu uwezo ni mkubwa mno wa kuchambia hoja .Wewe si kama makapu wewe ni mzee wa kijiwe hiki.This is extreme kwa kweli .Unata tuhuma nzito amabazo sitaki kuamini kwamba upasha baraza joto .
Na hayo makapu ndio nini?
 
Hizi ni ngano ulizotunga wewe mwenyewe. Mh Mudhihir amekaririwa na vyombo vya habari kuwa walikuwa wanataniana na Mh Wangwe kuhusu Yanga kutopeleka timu uwanjani dhidi ya Simba. Na yeye Mh Mudhidhir akamrudishia kuwa hajui kuvaa suti ( alifunga buttons zote ) wakacheka na Mh Wangwe akaenda zake and the rest is history.

Hii ya kwako mpya, mkuu umenoa try again...

Hongera. Umeelewa na unafahamu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom