PostGE2025 Maridhiano ya Kitaifa: Ni baina ya nani na nani?

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
maridhiano ni msingi muhimu sana miongoni mwa waTanzania wa mirengo yote kuelekea mchakato wa kupata katiba mpya gentleman.

very simple
Naelewa maridhiano ni msingi wa Upatanishi baina ya pande mbili zisokubaliana. Kama ni kuendea mchakato wa Katiba haturidhiani kitu gani?
 
Waliodhulumu na wakiodhulumiwa
 
Naelewa maridhiano ni msingi wa Upatanishi baina ya pande mbili zisokubaliana. Kama ni kuendea mchakato wa Katiba haturidhiani kitu gani?
Gentleman,
maridhiano ni tendo la hiyari baina ya pande zinazolenga au zinazotegemea kufikia lengo fulani mahususi la pamoja.

ndio maana hata wewe na mwenzi wako, mlianza uchumba hatimae mkaridhiana na kujenga msingi imara kuelekea ndoa na kua na familia bora yenye furaha na amani.

Lakini mnaweza kufanya biashara na rafiki yako, lakini hatimae baada ya mambo kua safi, mkaamua kuridhiana kuanzisha kampuni kabisa n.k

So,
waTanzania wote katika umoja na mshikamano wao, wanaelekea kwenye maridhiano ya hiyari ya kitaifa, yenye lengo moja tu, kujenga msingi imara kuelekea mchakato wa kupata katiba mpya bila mkwamo wowote, kama ilivyo wahi kutokea siku zingine huko nyuma. Full stop.

hayo ya sijui ya upatanisho wa pande mbili, tatu au nne, nadhani mkayafanye tu kibinafsi kwenye nyumba za ibada kila moja kwa imani yake kadiri alivyo mkosea Mungu na itapendeza zaidi πŸ’
 
Yote nakusoma vizuri kabisa isipokuwa nambie hizo pande 2 au zaidi ni zipi na kuna kutokuelewana nini mpaka yafanyike maridhiano kabla ya mchakato wa Katiba! Mfano, wapo wasiotaka jambo fulani - hilo jambo ni lipi na hao ni kina nani?
 
Ni hadaa za kisiasa tu.
 
Yote nakusoma vizuri kabisa isipokuwa nambie hizo pande 2 au zaidi ni zipi na kuna kutokuelewana nini mpaka yafanyike maridhiano kabla ya mchakato wa Katiba! Mfano, wapo wasiotaka jambo fulani - hilo jambo ni lipi na hao ni kina nani?
Gentleman,
habari ya pande mbili umeileta wewe gentleman,
mimi nimeongeza tu hata kama zikiwa pande tatu au nne, basi napendekeza maridhiano hayo yakafanyike kwenye nyumba za ibada kadiri ya mapenzi ya wanaopenda upatanisho au maridhiano hayo.

Lakini,
maridhiano ya hiyari miongoni mwa waTanzania wote, hayavuki kwenye kujenga msingi imara kuelekea mchakato muhimu sana wa kupata katiba mpya ya waTanzania wote πŸ’
 
Kwan ni nani analeta pingamizi la mchakato wa katiba mpya mpka mridhiane nae?
 
Kwan ni nani analeta pingamizi la mchakato wa katiba mpya mpka mridhiane nae?
Gentleman,
hakuna na mchakato muhimu sana wa kupata katiba mpya hakuna pingamizi lolote.
Maridhiano ya hiyari ya kitaifa ni muhimu sana ili kuepuka mkwamo kama uliowahi kutokea siku zingine kwenye mchakato kama huo. Full stop πŸ’
 
Gentleman,
hakuna na mchakato muhimu sana wa kupata katiba mpya hakuna pingamizi lolote.
Maridhiano ya hiyari ya kitaifa ni muhimu sana ili kuepuka mkwamo kama uliowahi kutokea siku zingine kwenye mchakato kama huo. Full stop πŸ’
Ule mkwamo ulitokea bunge la Katiba Mpya baina ya rais wa wakati huo JK, Wajumbe wa CCM na UKAWA, Je haya maridhiano yatawahusu wao?
 
Ule mkwamo ulitokea bunge la Katiba Mpya baina ya rais wa wakati huo JK, Wajumbe wa CCM na UKAWA, Je haya maridhiano yatawahusu wao?
maridhiano hayo ni ya kujenga msingi imara wa kuepusha mkwamo wowote unaofanana na ule kutokea tena.

this time tunakwenda kwenye maridhiano yatakayoenda kuondoa kila aina ya changamoto kwanza kabla ya mchakato kuanza ili hatimae tukianza ni one way mpaka tunamaliza.

habari sijui ya jk sijui warioba, sijui CCM, sijui ukawa n.k sahau gentleman. Tunakwenda kutengeneza katiba mpya ya waTanzania wote πŸ’
 
Mtoto wa Shule i think hupo darasa la pili.
Naomba urudi kwenye kauli za Barozi H.Polepole aliposema "Tusikubali kuingia kwenye maridhiano baada ya uchaguzi, Ni wapuuzi pekee uingia kwenye maridhiano baada ya uchaguzi", hapa naomba nieleweke kwamba sipo hapa kutetea chama chovhote cha siasa wala kukiunga mkono bali naomba nieleweke ninachosema ni ukweli wa hali iliyokuwepo.

CCM ilishapanga au ilishakuwa na mpango wa maridhiano baada ya uchaguzi ndio maana Vigogo wa CCM kama polepole aliekuwai kuwa Katibu mkuu wa chama hicho anasema ujumbe wa ndani kabisa wa chama chao, na hii inagokana kwamba kwakuwa yeye alikuwa katibu wa chama ni rahisi sana kwake kupata taarifa na mipango ya chama kwa sababu yeye pia kwa cheo chake cha ukatibu ndio msukaji na muundaji wa mipango hiyo.

CHADEMA ilishakataa hilo kabra hata alijaanza kwa kuweka "No Reforms, No Election", hii ina maana kwamba Kama maridhiano yangu kuwa ni muhimu kwa taifa basi yafanyike kabra ya uchaguzi.

Embu naomba tujiulize pamoja, hivi kati ya ccm na chadema, watanzania mbali mbali, asasi za kiraia nani anaetaka na kuyaimba maridhiano......?
Jibu unalo na sitakii kukitetea chama chochote hapo.

Mimi binafsi yangu naona swala sio kuvutana bali kugambua takwa la hayo maridhiano, je takwa la maridhiano ni nini....? Kuanzia hapo tutafikia muhafaka wa kitaifa,
 
Ccm ndio wanaohubiri maridhiano.
 
Kwa hiyo wale wauaji hawaguswi popote?..
 
Umezunguka wee lakini hujajibu swali, maridhiano kati ya nani na nani?
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Wewe kweli chizi, so hapo awali misingi imara haikuwepo mpaka mtake kuijenga sasa? Tunaridhiana nini kama hatuna tofauti?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…