DaudiAiko
JF-Expert Member
- Dec 2, 2012
- 372
- 310
Kwa muda mrefu Sasa, Chama cha Mapinduzi kimeongoza kwenye dira ya siasa kwa kuwa na Sera zinazo kubalika kwa wananchi na kwa ujumla kufanya vizuri katika kipindi ambacho wawakilishi wake wamekuwa madarakani. Matokeo ya kuwa na rekodi nzuri kama hii ni nzuri kwa wananchi na Chama tawala lakini ni mbaya kwa vyama vya upinzani. Mbaya kwasababu katika kipindi cha miaka kumi iliyopita ushawishi wa vyama hivi kisiasa na nafasi yao kwenye demokrasia vimepungua kwa kiasi kikubwa sana.
Elewa kwamba mifumo iliyopo imechangia kuwa na amani na utulivu hata katika kipindi ambacho vyama vya siasa vingine vinaweza kupotea kabisa. Hata kama siasa za Tanzania ni za vyama vingi, kupotea kwa vyama vya upinzani kuta halalisha siasa za chama kimoja kwa njia ambayo sio ya moja kwa moja. Vyama vya upinzani haswa CHADEMA vimezungumza sana kuhusu maridhiano, lakini je maridhiano yenye tija kwa wananchi ni maridhiano ya aina gani?
Nitatoa mfano mmoja ambao unaohusu vyama vya siasa kuruhusiwa kufanya mikutano ya hadhara. Utagundua kwamba jambo ambalo lingetakiwa kuwa zuri limetumiwa vibaya na wanasiasa haswa wa CHADEMA na ni tishio kwa amani ya taifa. Upinzani bora kwenye nchi zilizokomaa kisiasa haziko hivyo. Natoa mapendekezo yangu ya maridhiano nikiwa na imani kwamba vyama vya upinzani vitabadilika na kwamba siku moja tutakuwa na afya kwenye demokrasia yetu kwa kuwa na vyama vya siasa vinavyofanya shughuli za siasa kwenye mipaka mizuri. Vilevile vyama vya upinzani vinatakiwa kuwa na mchango chanya kwenye masuala ya nchi
Kwanza kabisa, vyama vya upinzani vinatakiwa kuwa na angalau asilimia fulani ya wawakilishi bungeni hata kama vikishindwa uchaguzi kwa asilimia kubwa. Idadi ya wawakilishi ambayo ni ndogo lakini yenye mchango mkubwa na sio kukosoa kila kitu bila kuwa na sababu za msingi ni mwanga kwenye bunge letu. Vyama vya upinzani vingetakiwa kuwa na wawakilishi Ikulu ukizingatia kwamba Ikulu ni taasisi ambayo inatakiwa iweze kupokea mabadiliko ya uongozi yoyote. Vilevile taasisi ya ushirikiano ya siasa inaweza kuundwa kama njia ya kuvishirikisha vyama vya upinzani kwenye maamuzi ya serikali. Uwakilishi kwenye kila wizara pia ni muhimu. Hivi vitakuwa na manufaa kama majukumu haya yatatumiwa vizuri
Mwisho kabisa, naomba tufikirie kuhusu vizazi vijavyo, kuhusu mabadiliko yanayoweza kutatua changamoto kabla hazijatokea. Tuelewe kwamba maridhiano ya kweli yanahusu pande zote mbili. Chama tawala kukubali umuhimu wa mchango wa upinzani kwenye demokrasia yenye afya na vyama vya upinzani kuwa na mchango muhimu na kutekeleza majukumu yao professionally serikalini
Haya ndiyo maridhiano ya kweli na yenye tija kwa wananchi na taifa kwa ujumla